BBC News, Swahili - Habari
Habari Kuu
Moja kwa moja, Iran yasema itajibu mapigo hadi Tel Aviv iwapo Marekani itathubutu kuishambulia
Onyo hilo limetolewa na mshauri mkuu wa kiongozi wa juu wa Iran, Ali Shamkhani, ambaye alisema kuwa shambulio lolote la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran litachukuliwa kama tangazo la vita.
Je, Marekani inajiandaa kuishambulia tena Iran?
Marekani, yenye jeshi lenye nguvu zaidi duniani, tayari imeshawahi kuonyesha uwezo wake wa kuishambulia Iran. Mnamo Juni mwaka jana, ilitekeleza operesheni iliyopewa jina Operation Midnight Hammer, iliyolenga vituo vya nyuklia vya Iran.
Sarafu 10 dhaifu zaidi duniani 2026
Dola ya Marekani ndiyo sarafu inayouzwa zaidi duniani hata kama, sio sarafu yenye nguvu zaidi duniani (haki hizo za thamani ya juu kwa sasa zinakwenda kwa sarafu ya Dinari ya Kuwait).
Kwa nini timu za England zinatawala Ulaya?
Ligi Kuu ya England, inaendelea kuonyesha nguvu yake barani Ulaya baada ya timu tano za England kumaliza ndani ya nafasi nane bora katika hatua ya ligi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kufuzu moja kwa moja kwa hatua ya mtoano.
Tetesi za soka Ulaya: Juventus yamtaka Kolo Muani & Zirkzee
Washambuliaji Randal Kolo Muani wa Tottenham na Joshua Zirkzee wa Manchester United wanawindwa na Juventus, muda wa Luis Enrique kama kocha wa Paris St-Germain unaweza kuongezwa, huku Harry Maguire akisubiri mazungumzo kuhusu mustakabali wake Manchester United.
Je, unaweza kulala ndani ya dakika mbili?
Watu wengine huwa na wakati mgumu kulala, wakati wengine hawawezi kulala kabisa. Mamilioni ya watu kote ulimwenguni wanakabiliwa na tatizo hili.
Tamu na chungu ya maridhiano Tanzania
Serikali inaona maridhiano kama mchakato unaohitaji utulivu na utaratibu. Upinzani unaona kama haki iliyochelewa kutendeka. Katikati ya mitazamo hiyo miwili, Watanzania wanasalia wakijiuliza maridhiano haya ni ya nani, kwa ajili ya nani, na kwa gharama gani?
Mwanamke amshikilia mwanamke mwanzake mateka kwa miaka 25
Wixon alimpa mwathiriwa chakula kidogo na hakumruhusu kutoka nje ya nyumba na alilazimika kuoga kwa siri usiku.
Namna Urusi inavyotumia wanaosakwa na Interpol kuwawinda wakosoaji wake ughaibuni
Maelfu ya faili zilizotolewa na mtoa taarifa wa Interpol zinafichua kwa mara ya kwanza ukubwa wa unyanyasaji unaoonekana kufanywa na Urusi dhidi ya shirika la polisi la kimataifa ili kuwalenga wakosoaji wake nje ya nchi.
Madaktari wafanikiwa kurejesha uume uliokatwa Ethiopia
Sehemu ya sentimita tano ya uume ilikuwa imehifadhiwa katika hali ya baridi na kuongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha kufanikiwa kwa upasuaji huo.
Marekani yapeleka meli kubwa ya kivita mashariki ya kati kuna nini?
Manowari ya kubeba ndege inayotumia nishati ya nyuklia ya Lincoln imekuwa ikihudumu chini ya Jeshi la Wanamaji la Marekani tangu 1989 na ni mojawapo ya meli kubwa na za kisasa zaidi za kubeba ndege katika Jeshi la Wanamaji la Marekani.
Tetesi za soka Ulaya: Chelsea yagoma kumuuza Cole Palmer
Brighton wamekataa ombi la Nottingham Forest la kumsajili Lewis Dunk, Chelsea wanamchukulia Cole Palmer kama mchezaji “asiyeuzwa”, na Raheem Sterling anatarajiwa kuondoka Stamford Bridge.
Sikiza / Tazama
Unataka kupunguza gharama za data?
Soma mtandao wetu wa maandishi kwa gharama ndogo za data.
Gumzo mitandaoni
'Nusu ya marafiki zangu waliuawa' - wasichana wanaorejea katika shule iliyojikuta katikati ya vita
Pacha ambao wanafunzi wenzao waliiuawa katika shabulio la makombora wanasema vifo vyao vimewafanya waazimie kumaliza masomo yao.
Je, ni kweli Marekani 'inaifadhili' Nato kwa asilimia 100?
Rais wa Marekani alitoa msururu wa madai yaliyopingwa, kuanzia hali ya Greenland hadi matumizi ya Nato.
Mpasuko wa 'chungwa' ndio kifo cha chama cha Raila Odinga - ODM?
''Chungwa'' ni nembo ya chama cha Orange Democratic Movement nchini Kenya ambalo limekuwepo kwa miongo miwili sasa, na ambalo kwa sasa baadhi ya wafuasi wake na hata wachambuzi wa kisiasa wanasema kwamba huenda likapasuka vibaya.
Aliwahi kuwakosoa viongozi wa Afrika wanaong'ang'ania madaraka. Sasa ataongoza muhula wa saba
Raia wa Uganda walio na umri wa chini ya miaka 40 - na ambao ni zaidi ya robo tatu ya watu - wamemfahamu rais mmoja tu.
Jinsi roketi ya utafiti wa hali ya hewa ya Norway ilivyokaribia kusababisha vita vya nyuklia
Kwa mara ya kwanza katika historia, kiongozi wa taifa alilazimika kuamsha kile kilichojulikana kama kifaa cha nyuklia, mfumo maalumu wenye maagizo na teknolojia ya kuidhinisha shambulio la nyuklia.
Maoni: Utawala wa kimabavu huporomoka polepole, lakini wa Iran haujafikia huko
Waandamanaji nchini Iran na wafuasi wao nje ya nchi wana matumaini kwamba utawala wa Kiislamu jijini Tehran uko katika hatua ya kuporomoka. Hilo ni kweli?
Sababu zilizofanya Somalia iwe na ghadhabu kali dhidi ya UAE
Serikali ya Mogadishu imeituhumu UAE kwa kudhoofisha mamlaka na uhuru wa Somalia.
'Ananyanyaswa na kufuatiliwa kila hatua': Nyota wa muziki anayemkabili rais wa muda mrefu wa Uganda
Kwa mvuto wake wa kipekee, uthubutu na uwezo wa kujiweka karibu na wananchi wa kawaida, nyota wa muziki Bobi Wine ametingisha siasa za Uganda.
Rais Trump ana lengo gani hasa na Iran?
Wakati ukandamizaji wa Iran dhidi ya maandamano ya kupinga serikali ukiendelea, rais wa Marekani anatafakari ni jinsi gani bora ya kushughulikia hilo.
Kuolewa nikiwa na miaka 40: ''Hakuna kikomo cha umri wa kupata upendo wa kweli"
"Wazo la mara kwa mara kwamba mwanamke mmoja baada ya miaka 35 au 40 ni 'hakamiliki,' 'ana madai makubwa' au 'amepoteza maisha' linaacha alama, kwa sababu linapuuzia mafanikio mengine, ukomavu, na safari ya maisha," anashughulikia.
Jinsi majasusi na makomando wa Marekani walivyomnasa Maduro
Operesheni hiyo ya aina yake iliyopewa jina la "Operation Absolute Resolve" inaonyesha jinsi vikosi vya Marekani vilivyoingia kwenye makazi ya Rais wa Venezuela na kumteka.
Ni nchi zipi zinaweza kulengwa na Trump baada ya Venezuela?
Trump ametoa vitisho vingi dhidi ya mataifa mengine katika siku za hivi karibuni.
BBC News Swahili sasa ipo WhatsApp
Vipindi vya Redio
Listen Next, Dira Ya Dunia, 18:29, 29 Januari 2026, Muda 1,00,00
Kipindi cha habari, makala na mahojiano cha kila siku kuanzia saa kumi na mbili unusu jioni Afrika Mashariki
Sikiliza, Amka Na BBC, 06:59, 29 Januari 2026, Muda 29,30
Kipindi cha habari, mahojiano na makala kila siku saa kumi na mbili na saa moja asubuhi Afrika Mashariki
Sikiliza, Amka Na BBC, 05:59, 29 Januari 2026, Muda 29,30
Kipindi cha habari, mahojiano na makala kila siku saa kumi na mbili na saa moja asubuhi Afrika Mashariki
Sikiliza, Dira Ya Dunia, 18:29, 28 Januari 2026, Muda 1,00,00
Kipindi cha habari, makala na mahojiano cha kila siku kuanzia saa kumi na mbili unusu jioni Afrika Mashariki
Dira ya Dunia TV
Kipindi cha habari motomoto, kinachowaweka watazamaji karibu zaidi na yanayojiri duniani

























































