Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
U najua mtumba (nguo chakavu) inaweza kubadilisha maisha yako?
Petri Alava alikuwa akivaa suti zilizobanwa na viatu vya ngozi kufanya kazi, akisimamia mashirika makubwa ya kuuza kila kitu kuanzia magazeti hadi vifaa vya bustani.
Sasa anaendesha kampuni yake ambapo soksi ni utamaduni wa kawaida kualiwa na kutembelea kwenye sakafu ya ofisi, na anajivunia kuvaa fulana ya shingo ya mviringo iliyosokotwa kutokana na nyuzi za nguo zilizochakatwa upya.
Kampuni yake, Infinited Fiber, imewekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia ambayo inaweza kubadilisha nguo ambazo zingeweza kuchomwa au kutupwa kwenye madampo, na kuwa nyuzi mpya za kutengeneza nguo mpya.
Inaitwa Infinna, nyuzinyuzi hizo tayari zinatumiwa na chapa za kimataifa zikiwemo Patagonia, H&M na Inditex, ambayo inamiliki Zara. "Ni nyuzi za nguo zenye ubora wa hali ya juu, ambazo zinaonekana na kuhisi asilia - kama pamba," asema Bw Alava, akisugua kitambaa chake cha bluu bahari katikati ya vidole vyake. "Na ni kutatua tatizo kubwa la taka." Duniani kote, wastani wa tani milioni 92 za taka za nguo huundwa kila mwaka, kulingana na shirika lisilo la faida la Global Fashion Agenda, na takwimu hii inatarajiwa kuongezeka hadi zaidi ya tani milioni 134 ifikapo 2030, ikiwa utengenezaji wa nguo utaendelea katika mkondo wake wa sasa. .
Bw Alava anaeleza kuwa bidhaa hiyo huzalishwa kwa kuanzia kupitia mchakato wenye hatua nyingi ambao huanza na kuchana nguo kuukuu na kuondoa vifaa kama vifungo na pini paoja na rangi, na kuishia kutengenezwa nyuzi mpya, iliyozalishwa upya.
Nyuzi hii iliyokamilishwa inaweza kwa urahisi "kuingia kwenye michakato ya kawaida ya uzalishaji nguo" inayotumiwa na chapa za High Street, kuchukua nafasi ya pamba na nyuzi zingine, kutengeneza kila kitu kuanzia mashati na magauni hadi suruali za jeans.
Sehemu kubwa ya sayansi inayohusika katika kutengeneza nyuzinyuzi imekuwapo tangu miaka ya 1980, anasema Bw Alava, lakini maendeleo ya haraka ya kiteknolojia katika miaka michache iliyopita hatimaye yamefanya uzalishaji mkubwa kuwa ni jambo linalowezekana zaidi.
Sambamba na hilo, anaamini chapa za High Street zimezingatia zaidi "kutafuta kwa uaminifu kubadilisha matumizi yao ya nyenzo", wakati watumiaji wa chapa za Milenia na Gen Z wanazidi kuwa na wasiwasi juu ya ununuzi endelevu.
"Ni watu tofauti, watumiaji tofauti, na ni kwa watu wa rika langu," anacheka.
Kampuni hiyo tayari imevutia watu wengi katika teknolojia yake na kwamba ilitangaza hivi majuzi kuwa inawekeza kiasi cha €400m (£345m; $400m) kujenga kiwanda chake cha kwanza kikubwa cha kiwango cha kibiashara katika kiwanda cha karatasi ambacho hakitumiki huko Lapland.
Lengo ni kuzalisha tani 30,000 za nyuzinyuzi kwa mwaka mara tu itakapofanya kazi kwa uwezo kamili mwaka wa 2025. Hiyo ni sawa na nyuzinyuzi zinazohitajika kutosha kuzalisha takriban fulana milioni 100.
"Nadhani athari inaweza kuwa kubwa sana, ikiwa utafikiria juu ya mfumo mzima wa nguo, ni nini kilichopo kwa sasa na ni kiasi gani cha taka za nguo tulizonazo," anahoji Kirsi Niinimäki, profesa mshiriki katika utafiti wa mitindo katika Chuo Kikuu cha Aalto, umbali mfupi tu kutoka makao makuu ya Infinited Fiber.
"Ni mfano mzuri sana wa jinsi tunavyoweza 'kuunga biashara'… kwa kuanza kuhamia uchumi wenye mzunguko."