Tetesi za Soka Ulaya: Camavinga kuondoka Madrid, Arsenal yaanza mazungumzo na Lukeba

s

Chanzo cha picha, Getty Images/bbc

Muda wa kusoma: Dakika 2

Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England vimefunguliwa milango ya matumaini ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 23, baada ya Real Madrid kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili yake dirisha la majira ya kiangazi. (Marca)

Arsenal wameanza mazungumzo na RB Leipzig kuhusu kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Castello Lukeba, 23. (L'Equipe)

Chelsea, Liverpool na Manchester United zinatarajiwa kupambana kusaka saini ya kiungo wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 22. (Football Insider)

Chelsea na Manchester United pia zinatajwa kuwa katika ushindani mwingine wa uhamisho, huku zote zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mshambuliaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 19 Said El Mala kutoka 1. FC Köln. (Caughtoffside)

Aston Villa wanashindana na vilabu kadhaa barani Ulaya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Julian Brandt, 29, wa Borussia Dortmund, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu huu wa kiangazi. (Fichajes)

Newcastle United wanaweza kumrejesha kiungo wao wa zamani akicheza timu za vijana, Elliot Anderson, 23, anayekipiga sasa Nottingham Forest, ikiwa Bruno Guimarães, 28, au Sandro Tonali, 25, ataondoka klabuni hapo. (Teamtalk)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alisson Becker

Mlinda mlango wa Brazil Alisson Becker, 33, wa Liverpool amewekwa kwenye malengo makuu ya Juventus katika dirisha la majira ya kiangazi. (Gazzetta dello Sport)

Manchester United na Liverpool zinaongoza mbio za kumsajili winga wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, wa RB Leipzig, baada ya Bayern Munich kujiondoa kwenye mbio hizo. (Christian Falk)

Manchester City wanataka kuhakikisha kiungo mshambuliaji wa England Phil Foden, 25, anasalia klabuni hapo zaidi ya mkataba wake wa sasa unaomalizika mwaka 2027, na wanataka kuharakisha mazungumzo ya mkataba mpya. (Football Insider)

Manchester United wako tayari kulipa karibu euro milioni 100 (£86.7m) ili kumnasa winga wa Hispania Nico Williams, 23, kutoka Athletic Club. (Fichajes)

Liverpool wanakaribia kumsajili beki chipukizi wa Scotland Dara Jikiemi, 16, baada ya kukataa kusaini mkataba wa miaka mitatu Celtic. (Teamtalk)