Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Baba mkwe wa El Chapo Guzman afungwa miaka 10
Baba mkwe wa mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya , Joaquin Guzman, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kupenyeza bangi nchini Marekani.
Ines Coronel Barreras alipatikana na makosa katika mahakama moja ya Mexico, baada ya polisi kutwaa magari silaha na zaidi ya kilo 250 za bangi.
Marekani ilimwekea vikwazo miaka minne iliyopita, na kusema kwamba ni mojawepo wa vigogo wa genge la Sinaloa.