Tassia: Jengo laporomoka Kenya nini kilichotokea?
Watu wawili wamethibitishwa kufariki baada ya jengo la ghorofa sita kuanguka asubuhi ya leo katika eneo la Embakasi jijini Nairobi, Kenya huku wengine kadhaa wakihofiwa kunaswa chini ya kifusi cha jengo hilo.
Shughuli za uokoaji zinaendelea. Ripoti zinasema watu kadhaa wameokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.