Afrika Mashariki kukumbwa na ukame katika miezi ijayo

Ethiopia, Uganda, Rwanda, Kenya, Burundi, na Tanzania zitaathiriwa na hali ya ukame, utabiri huo unasema.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi, Martha Saranga & Rashid Abdallah

  1. Afrika Mashariki kukumbwa na ukame katika miezi ijayo

    DFC

    Chanzo cha picha, EARTH.ORG

    Maelezo ya picha, Ethiopia, Uganda, Rwanda, Kenya, Burundi, na Tanzania zitaathiriwa na hali ya ukame.

    Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Nchi za Jumuiya ya IGAD, kinasema kuwa eneo la Afrika Mashariki litapata hali ya ukame kuliko kawaida kati mwezi wa Januari na Machi 2025.

    Katika utabiri wake uliotolewa Jumatatu, kinasema Ethiopia, Uganda, Rwanda, Kenya, Burundi, na Tanzania zitaathiriwa na hali ya ukame.

    Kanda hiyo pia itarekodi joto zaidi kuliko kawaida wakati wa msimu wa Januari hadi Machi 2025. "Joto la kawaida huenda likarekodiwa katika maeneo machache ya kaskazini mwa Uganda na magharibi mwa Sudan," imesema ripoti.

    Kwa mujibu wa kituo hicho, katika kanda nzima, kusini magharibi mwa Tanzania na kusini magharibi mwa Uganda pekee ndizo zitakumbwa na hali ya mvua kuliko kawaida katika kipindi hicho, jambo linaloashiria kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia nchi katika ukanda huo.

    Mataifa ya Pembe ya Afrika ni miongoni mwa yaliyoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwani ukame, mafuriko, na wadudu waharibifu huwa jambo la kawaida huku kukiwa na joto la juu la nyuzi joto 32, kulingana na kituo hicho.

    Zaidi ya watu milioni 64 walihitaji msaada wa kibinadamu katika Pembe ya Afrika mwishoni mwa Novemba kutokana na migogoro na majanga ya hali ya hewa, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na IGAD walibainisha katika ripoti ya hivi karibuni.

  2. Timu za Afrika Mashariki kukutana kisiwani Pemba katika Kombe la Mapinduzi

    FC

    Chanzo cha picha, TFF

    Maelezo ya picha, Kikosi cha Zanzibar Heroes kikiwa katika mazoezi ya kujiandaa na kombe la Mapinduzi

    Michuano ya Kombe la Mapinduzi, inafungua pazia leo visiwani Zanzibar, ambapo Kilimanjaro Stars kutoka Tanzania bara itakutana na timu ya taifa ya Zanzibar Heroes usiku wa leo, katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

    Timu nyingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni Burkina Faso kutokea Afrika Magharibi na Harambe Stars kutoka Kenya, ambao watacheza kesho katika uwanja huo huo.

    Timu ya taifa ya Burundi na Uganda The Cranes zilijitoa katika mashindano hayo dakika za mwisho na kuifanya michuano hiyo kubaki na timu nne pekee.

    Kombo la Mapinduzi hufanyika kama sehemu ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12 mwaka 1964, yaliyoondoa utawala w Kisultani katika visiwa hivyo ambavyo kwa sasa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  3. Elon Musk akosolewa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu magenge ya wabakaji

    vc

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Elon Musk

    Ukosoaji wa Elon Musk dhidi ya serikali ya Uingereza namna inavyoshughulikia magenge ya wabakaji “sio sahihi na ni upotoshaji," amesema Katibu wa masuala ya Afya, Wes Streeting.

    Bilionea Musk amechapisha msururu wa taarifa kwenye tovuti yake ya kijamii ya X, akimshutumu Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer kwa kushindwa kushughulikia magenge ambayo yaliwabaka wasichana wadogo, na kutaka waziri wa ulinzi Jess Phillips afungwe jela.

    Alipoulizwa kuhusu maoni hayo, Streeting alisema "serikali hii inachukulia suala la unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto kwa umakini mkubwa."

    Amemwalika Musk "kujitayarisha na kufanya kazi nasi" dhidi ya magenge ya ubakaji.

    Kiongozi wa Conservative, Kemi Badenoch ametoa wito wa uchunguzi kamili kuhusu kile alichokiita "kashfa ya magenge ya ubakaji" Uingereza.

    Lakini chama hicho pia kimemkosoa Musk kwa "kuchapisha taarifa ambazo sio sio sahihi" na kujitenga na wito wake wa kutaka Phillips afungwe.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Israel imethibitisha kuwa inamshikilia mkuu wa hospitali ya Gaza Abu Safiya

    XYV

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa hospitali hiyo alizuiliwa wakati wa uvamizi wa Israel Ijumaa iliyopita

    Israel imethibitisha kuwa inamshikilia mkurugenzi wa hospitali ya Gaza Dr Hussam Abu Safiya baada ya hapo awali kuliambia shirika lisilo la kiserikali la eneo hilo kuwa halina taarifa zake, na hivyo kuzua wasiwasi kuhusu afya yake.

    Taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) ilisema "kwa sasa anachunguzwa na vikosi vya usalama vya Israel" ana kwa ana.

    Taarifa hiyo haikutoa ufafanuzi kuhusu mkanganyiko huo lakini ilisisitiza kwamba anashukiwa kuwa "gaidi" anayeshikilia cheo" katika kundi la Hamas, Wapalestina wenye silaha wanalopigana na Israel huko Gaza.

    Dk Abu Safiya alikamatwa wakati jeshi la Israeli likiwalazimisha wagonjwa na wafanyikazi wa afya kuondoka katika hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza Ijumaa iliyopita, kwa madai kuwa kituo hicho ni "ngome ya magaidi wa Hamas".

    Siku ya Alhamisi IDF iliwaambia Madaktari wa shirika la kutetea Haki za Kibinadamu Israel (PHRI) kwamba "haijamkamata wala kumshikilia mtu huyo".

    PHRI iliwasilisha ombi katika Mahakama Kuu ya Israel siku ya Alhamisi, ikitaka kufahamishwa mahali alipo Dkt Abu Safiya kufichuliwa. Ilisema mahakama iliipa IDF wiki moja kutekeleza.

    Wakati huo huo mkuu wa Amnesty Agnès Callamard alisema mamlaka ya Israel lazima "ifichue haraka aliko".

    Alisema Israel imewazuilia "mamia ya wahudumu wa afya wa Kipalestina kutoka Gaza bila kufunguliwa mashitaka" na kusema "wameteswa na kutendewa vibaya na kuzuiliwa bila mawasiliano".

    Hata hivyo Israel inakanusha kuwatesa wafungwa.

    Awali familia ya Dkt Abu Safiya iliambia Idhaa ya Kiarabu ya BBC kwamba wanaamini anazuiliwa katika kambi ya kijeshi ya Sde Teiman kusini mwa Israel, ambapo majeshi ya Israel yamewachukua wafungwa wengi kutoka Gaza kwa mahojiano.

    Hapo awali wafichuaji waliambia BBC na vyombo vingine vya habari vya kimataifa kuhusu hali ngumu sana inayowakabili wafungwa walioko.

    Israel imesema wafungwa wote huko wanahifadhiwa "kwa uangalifu na ipasavyo".

    IDF iliamuru kila mtu ndani ya hospitali ya Kamal Adwan kuondoka Ijumaa iliyopita asubuhi, na kutoa muda wa takribani dakika 15 kwa hospitali hiyo kuwahamisha wagonjwa na wafanyikazi ndani ya eneo hilo, wahudumu wa afya waliambia BBC.

    Mji wa Beit Lahia, iliko hospitali hiyo umekuwa chini ya vizuizi vikali vya Israel vilivyowekwa kwenye maeneo ya kaskazini mwa Gaza tangu Oktoba.

    Umoja wa Mataifa umesema eneo hilo limezingirwa kwa karibu huku jeshi la Israel likizuia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa misaada katika eneo hilo ambalo wastani wa watu 10,000 hadi 15,000 wamesalia.

    XYZ

    Chanzo cha picha, Reuters

    Siku ya Jumamosi, IDF ilisema iliwakamata wapiganaji 240 huko Kamal Adwan na kusema Dk Abu Safiya alikuwa miongoni mwa wafanyikazi wa afya waliochukuliwa kuhojiwa.

    Picha za video zilimuonyesha akitembea kuelekea kwenye gari la kivita la Israel kabla ya kupelekwa kuhojiwa. Msemaji wa jeshi la Israel alithibitisha kukamatwa siku hiyo hiyo, akisema daktari huyo alikuwa amehamishwa kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano.

    Dk Abu Safiya hapo alikamatwa na vikosi vya Israel wakati wa uvamizi wa awali katika hospitali hiyo mwezi Oktoba, lakini aliachiliwa muda mfupi baadaye. Wakati wa operesheni hiyo ya Israel mtoto wa kiume wa Dkt Abu Safiya mwenye umri wa miaka 15 aliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani. Picha za baadaye siku hiyo zilimuonyesha akiongoza dua ya mazishi ya mwanawe katika eneo la hospitali.

    Mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya afya vya Gaza yamesababisha kulaaniwa zaidi.

    Siku ya Jumanne Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema mashambulizi ya Israel katika hospitali na kandokando ya hospitali yamechangia kuharibu mfumo wa afya wa Gaza kabisa" na kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

    Ujumbe wa Israel mjini Geneva ulisema vikosi vya Israel vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria za kimataifa na "kamwe havitalenga raia wasio na hatia".

    Israel ilianzisha kampeni ya kuiangamiza Hamas kujibu mashambulizi ya kundi hilo,mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 walichukuliwa mateka.

    Zaidi ya watu 45,580 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo.

    Unaweza pia kusoma;

  5. Venezuela yatoa donge nono kwa atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa mgombea wa urais

    xyz

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Edmundo González (kulia), mgombea urais aliye uhamishoni, pamoja na kiongozi wa upinzani María Corina Machado (kushoto) Julai 2024.

    Serikali ya Venezuela imetangaza zawadi ya dola za kimarekani 100,000 (£81,000) kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa mgombea urais wa upnde wa upinzani Edmundo González aliye uhamishoni.

    Alitoroka nchini Venezuela mwezi Septemba na akapewa hifadhi ya kisiasa nchini Uhispania baada ya Venezuela kuamuru akamatwe, wakimtuhumu González kwa njama na kughushi nyaraka.

    González ameapa atarejea Venezuela kabla ya kuapishwa kwa Rais Nicolas Maduro Ijumaa ijayo, akiishutumu serikali kwa kuiba kura.

    Muda mfupi baada ya kitita hicho kutangazwa, González alisema anasafiri kwenda Argentina kuanza ziara yake Amerika Kusini, ambapo atakutana na Rais mkosoaji mkali wa Maduro, Javier Milei siku ya Jumamosi.

    Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeiamuru Venezuela "kujizuia kuharibu" hesabu za kura za uchaguzi wa rais wa Julai 2024.

    Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE) inayoungwa mkono na serikali ilimtangaza Maduro, kuwa mshindi lakini ilishindwa kutoa hesabu za kura ili kuunga mkono ushindi huo.

    Upinzani, kwa msaada wa mashahidi walioidhinishwa ulikusanya na kuchapisha zaidi ya 80% ya hesabu za kura, unasema hizo zinathibitisha kuwa mgombea wake, González, alikuwa mshindi kwa kupata wingi wa kura.

    González hakuwa maarufu sana nchini Venezuela alipojiandikisha kama mgombeaji wa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo mwezi Machi. Hakuwahi kugombea nyadhifa za umma hapo awali na hata hakujulikana sana katika duru za upinzani.

    Lakini miezi kadhaa baada ya kuamua kugombea wadhifa wa juu, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya chini wa zamani alimshinda Maduro katika kura za maoni.

    Venezuela imeshuhudia mgawanyiko kati ya serikali na wafuasi wa upinzani ukizidi kuwa mkubwa katika muongo mmoja uliopita.

    Sauti ya maridhiano ya González wakati wa kampeni ya urais ilikuwa tofauti kabisa na ile ya Maduro, ambaye alionya kuhusu "umwagaji wa damu" iwapo González atashinda.

    Uchaguzi wa marudio wa 2018 uliomuweka Maduro madarakani ulipuuzwa na wengi kuwa haukuwa huru na wa haki.

    Unaweza pia kusoma:

  6. Mauritius yamkamata gavana wa zamani wa benki kuu

    dx

    Chanzo cha picha, BOM

    Maelezo ya picha, Harvesh Kumar Seegolam

    Polisi nchini Mauritius imemkamata gavana wa zamani wa benki kuu ya nchi hiyo siku ya Ijumaa kuhusiana na uchunguzi wa kesi ya utapeli, vimeripoti vyombo vya habari vya ndani katika taifa la kisiwa cha Bahari ya Hindi.

    Mwezi uliopita, kitengo cha polisi cha Mauritius cha kupambana na utakatishaji fedha kilitoa amri ya kukamatwa kwa Harvesh Kumar Seegolam kutokana na kesi hiyo, bila kutoa maelezo zaidi. Seegolam alikuwa nje ya nchi wakati agizo hilo lilipotolewa.

    "Gavana wa zamani wa Benki ya Mauritius, Harvesh Seegolam, alikamatwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa Plaisance Ijumaa ya Januari 3," imeripoti Le Défi Media Group.

    Msemaji wa polisi amethibitisha kukamatwa kwake lakini alikataa kutoa maelezo yoyote. Na pia wakili wa Seegolam, hajaeleza chochote.

    Kukamatwa huko pia kuliripotiwa na vyombo vingine likiwemo gazeti la kila siku la l'Express.

    Kukamatwa kwa gavana huyo wa zamani ni hatua ya kwanza kubwa ya serikali ya Waziri Mku, Navin Ramgoolam, ambaye amesema serikali iliyopita ilighushi pato la taifa, nakisi ya bajeti na takwimu za deni la umma kwa miaka mingi.

  7. Ukungu watatiza shughuli za maisha na usafari India

    xyz

    Chanzo cha picha, ANI

    Ukungu mzito umetanda Delhi na maeneo ya kaskazini mwa India, na kusababisha changamoto za ucheleweshaji wa safari na taharuki.

    Zaidi ya safari 100 za ndege zilicheleweshwa katika uwanja wa ndege wa Delhi siku ya Ijumaa asubuhi, kwa mujibu wa shirika la habari la PTI. Mamia ya safari za garimoshi pia zimepangwa upya, au kuchelewa.

    Mamlaka ya hali ya hewa nchini India imesema kuwa hali ya ukungu huenda ikaendelea kwa siku chache zijazo.

    Ukungu mzito ni kawaida katika kipindi hiki cha mwaka huko Delhi na maeneo mengine ya kaskazini mwa India, wakati eneo hilo likikabiliwa na wimbi la baridi kali.

    Picha na video zilionyesha miji kadhaa iliyogubikwa na ukungu mzito.

    Takriban viwanja vya ndege tisa kikiwemo kile cha Delhi vimeripotiwa kutoonekana vizuri Ijumaa asubuhi, Idara ya Hali ya Hewa ya India (IMD) ilisema.

    Uwanja wa ndege wa Delhi umetoa ushauri kwa abiria, na kuwataka kuchukua tahadhari kutokana na kuahirishwa kwa safari.

    "Wakati kutua na kupaa kukiendelea kwenye uwanja wa ndege wa Delhi, safari za ndege ambazo hazifuati mfumo wa CAT III zinaweza kuathiriwa," taarifa ya uwanja wa ndege ilieleza ikirejelea mfumo wa rada ambao huwezesha kutua wakati kuna muonekano hafifu sana.

    Mashirika kadhaa ya ndege pia yametoa taarifa kuwataka wasafiri kuangalia ratiba za ndege kabla ya kupanga safari zao.

    IMD inachukulia hali ya ukungu kuwa "mzito" ikiwa mwonekano unapungua chini ya 200m na ​​"mzito sana" ikiwa utashuka chini ya 50m.

    Idara ya hali ya hewa imesema kuwa Delhi inaweza kupata mvua nyepesi hadi wastani mnamo 6 Januari, ambayo huenda ikapunguza zaidi joto.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Watu wawili wafariki baada ya ndege ndogo kuanguka katika jengo la California

    xzy
    Maelezo ya picha, Wawili wafariki baada ya ndege ndogo kugonga paa la kiwanda huko California

    Watu wawili wamefariki na wengine 18 kujeruhiwa baada ya ndege ndogo kuanguka katika jengo la kibiashara kusini mwa California, maafisa wanasema.

    Watu kumi walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha, Idara ya Polisi ya Fullerton ilisema katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii X Alhamisi, huku wengine nane wakitibiwa majeraha na kuruhusiwa kuondoka eneo la tukio.

    Ndege hiyo yenye injini moja aina RV-10 ilianguka saa 14:15PST (20:15GMT), kwa mujibu wa mamlaka ya Usafiri wa Anga.

    Maafisa hawajatoa maelezo zaidi kuhusu namna ajali hiyo ilivyotokea.

    Haijabainika iwapo watu wawili waliofariki walikuwa wafanyakazi au abiria ndani ya ndege hiyo.

    Polisi wanasema wanahamisha majengo katika eneo hilo, na kuutaka umma kukaa mbali na eneo la ajali.

    Mbunge Lou Correa, ambaye anawakilisha eneo la Kaunti ya Orange, lenye umbali wa maili 25 (40km) kusini mwa Los Angeles, alisema kuwa jengo lililoangukiwa na ndege hutumika kwa biashara ya kutengeneza samani.

    Picha za angani za eneo la tukio zinaonyesha baadhi ya mabaki ya ndege ndani ya jengo hilo.

    Ajali hiyo pia ilizua moto ambao ulizimwa na maafisa wa zima moto.

    Picha za usalama zilizorekodiwa kutoka kwenye jengo hilo, kando ya barabara zinaonyesha mlipuko mkali, vimeeleza vyombo vya habari vya eneo hilo.

    "Watu wanatetemeka kutokana na hali hiyo," shahidi Mark Anderson aliambia KRCA-TV.

    "Ilikuwa ni kishindo kikubwa tu, na kisha mmoja wa watu akatoka nje na kusema, 'Ee Mungu wangu, jengo linawaka moto.'

    Mahali ambapo ndege ilianguka ni karibu na Uwanja wa Ndege wa Manispaa wa Fullerton, takriban maili 6 (kilomita 10) kutoka Disneyland.

    Ndege hiyo inaonekana kurejea katika uwanja wa ndege muda mfupi baada ya kupaa, kulingana na KRCA-TV.

    Takriban watu 100 hatimaye walihamishwa kutoka kiwanda cha samani cha Michael Nicholas Designs, kwa mujibu wa gazeti la Orange County Register.

    Juanita Ramirez, mfanyakazi, aliambia gazeti hilo kwamba alisikia kishindo kikubwa kabla ya kuona mlipuko mkubwa wa moto ukiruka kuelekea kwake.

    Hii ni ndege ya pili kuanguka katika eneo hilo katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, kwa mujibu wa CBS, mshirika wa BBC nchini Marekani.

    Mnamo tarehe 25 Novemba, ndege nyingine ilianguka kwenye mti karibu na eneo la ajali hii.

  9. Mashirika ya kiraia Kenya yataka kesi za utekaji nyara zipelekwe ICC

    EWD

    Mashirika mawili ya kiraia nchini Kenya yameiomba mahakama kuu ya nchi hiyo kumshurutisha Mwanasheria Mkuu, Dorcas Oduor kupeleka kesi za utekaji nyara na kupotea kwa watu katika taifa hilo la Afrika Mashariki, katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa uchunguzi na hatua zaidi, limeripoti gazeti la The Standard.

    Kituo cha Sheria na Kituo cha Haki za Kijamii cha Mathare vilisema hapo jana kwamba, ni wazi kuwa Polisi inashindwa kutekeleza jukumu lake la kulinda watu katika jamhuri hiyo.

    "Inavyoonekana ni kuwa Jeshi la Polisi halina uwezo wa kufanya upelelezi, mahakama hii ina wajibu wa kuwalinda na kuwatetea watu wa Kenya kwa kupeleka suala la kupotea kwa watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai."

    Takribani watu 82 ambao wanaelezwa kuwa ni wakosoaji wa serikali wametekwa nyara tangu maandamano kuhusu mapendekezo ya nyongeza ya ushuru yalitikisa nchi hiyo Juni 2024, kulingana na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya.

    Polisi wamekanusha kuhusika na kusema watachunguza kutoweka kwa watu hao.

    Pia unaweza kusoma:

  10. Ndege 22 zisizo na rubani zimedunguliwa usiku kucha - Urusi

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wizara ya Ulinzi ya Urusi inadai kuwa ndege zisizo na rubani 22 za Ukraine zilidunguliwa katika maeneo sita ya Urusi usiku kucha, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo mbali na mipaka ya Ukraine.

    Ujumbe mfupi kutoka kwenye mitandao ya kijamii ya wizara hiyo unasema kuwa ndege 10 zisizo na rubani zilidunguliwa katika eneo la Bryansk, nne kila moja katika mikoa ya Oryol na Rostov, mbili katika mkoa wa Belgorod, na droni moja kila moja katika mikoa ya Volgograd na Lipetsk.

    Huku hayo yakijiri, Katika mji mkuu Kyiv, nyumba ya kibinafsi iliwaka moto baada ya na kuangukiwa na uchafu kutoka kwa droni iliyoungua.

    Kulingana na mkuu mpya wa utawala wa kijeshi wa Kyiv, Timur Tkachenko, moto huo uliozuka katika wilaya ya Darnitsky kusini mashariki mwa mji mkuu, tayari umezimwa.

    "Waokoaji walizima moto, habari kuhusu waathiriwa wa tukio hilo bado hazijatolewa."

    Ndege nyingine isiyo na rubani ya kamikaze ya Urusi ilitunguliwa kwenye wilaya ya Goloseevsky kusini mwa Kyiv, kulingana na meya wa Kyiv Vitaliy Klitschko.

    Urusi na Ukraine: Soma zaidi

    • Jaribio la kumkamata rais wa Korea Kusini Yoon lasitishwa baada ya mzozo mkali

      h

      Chanzo cha picha, Reuters

      Maelezo ya picha, Wachunguzi wanasema wataamua juu ya hatua zinazofuata baada ya kufanya upya tathmini

      Wachunguzi wa Korea Kusini wamesitisha jaribio la kumkamata rais aliyesimamishwa kazi Yoon Suk Yeol baada ya mvutano mkali wa saa sita na timu ya usalama nje ya nyumba yake.

      "Tumebaini kwamba kukamatwa hakuwezekani," ilisema ofisi ya upelelezi wa ufisadi (CIO), ambayo imekuwa ikichunguza tamko la amri ya sheria la kijeshi la muda mfupi lililotolewa na Yoon.

      "Hatua zinazofuata zitaamuliwa baada ya kutathminiwa upya," CIO ilisema, na kuongeza kuwa "kukataa kutekeleza mchakato wa kisheria" kwa Yoon "kunasikitisha sana".

      Wafuasi wa Yoon, ambao wamepiga kambi mbele ya makao ya rais kwa siku kadhaa, walishangilia kwa wimbo na densi huku hatua ya kusitisha kukamatwa kwake ikitangazwa. "Tumeshinda!" waliimba.

      CIO ilisema kuwa wasiwasi juu ya usalama wa timu uwanjani ni sababu nyingine katika uamuzi wao wa kusitisha jaribio la kukamatwa.

      Wachunguzi wana hadi Januari 6 kumkamata Yoon kabla ya hati ya sasa kuisha. Wanaweza, hata hivyo, kutuma maombi ya hati mpya na kujaribu kumweka kizuizini tena.

      Tangu asubuhi na mapema, makumi ya gari za polisi zilijipanga barabarani nje ya makazi ya Yoon katikati mwa Seoul.

      CIO ilisema kuwa wasiwasi juu ya usalama wa timu uwanjani ni sababu nyingine katika uamuzi wao wa kusitisha jaribio la kukamatwa.

      Wachunguzi wana hadi Januari 6 kumkamata Yoon kabla ya hati ya sasa kuisha. Wanaweza, hata hivyo, kutumpa maombi ya hati mpya na kujaribu kumuweka kizuizini tena.

      Tangu asubuhi na mapema, makumi ya gari za polisi zilijipanga barabarani nje ya makazi ya Yoon katikati mwa Seoul.

      Unaweza pia kusoma:

    • Mwanaume wa Marekani aliyewauwa watu 15 New Orleans alitekeleza shambulio peke yake, FBI yasema

      g

      Chanzo cha picha, FBI

      Mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Marekani aliyewauwa watu 15 kwa kugonga lori kwenye umati wa watu waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya mwaka mpya huko New Orleans alikuwa ameahidi utiifu kwa Islamic State na alionekana kurekodi ambapo alilaani muziki, dawa za kulevya na pombe.

      Aamsud -Din Jabbar, mzaliwa wa Texas mwenye umri wa miaka 42 ambaye aliwahi kuhudumu nchini Afghanistan, alitekeleza peke yake k shambulio hilo, FBI ilisema Alhamisi, ikibadilisha tathmini ya awali kwamba anaweza kuwa na washirika.

      Aliuawa katika makabiliano ya risasi na polisi baada ya shambulio hilo, ambalo pia lilijeruhi makumi ya watu na limetajwa na FBI kama kitendo cha kigaidi.

      "Ilikusudiwa na ni kitendo kiovu," Naibu mkurugenzi msaidizi wa FBI Christopher Raia aliuambia mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, akithibitisha hitimisho la ofisi hiyo kwamba Jabbar alihamasishwa na Islamic State, kundi la wanamgambo lenye wapiganaji nchini Iraq na Syria.

    • Msomali anayesafiri kwa pikipiki hadi ncha ya kusini mwa Afrika alivyofurahishwa na kabila la Tanzania

      g

      Chanzo cha picha, Faisal

      Faysal Abdullahi Abdi ni kijana mdogo wa Kisomali ambaye yuko katika safari ya pikipiki kwenda nchi za Kiafrika.

      Safari hii ni safari ya kujifunza na kupata uzoefum Faisal aliiambia BBC.

      Faisal alianza safari hii kutoka Nairobi, akapitia mikoa ya Somalia ya Kenya Kaskazini Mashariki, Mombasa, kisha Tanzania, ambako alienda hadi Malawi alipo sasa.

      "Ninajaribu kukumbuka safari yangu na kuwanufaisha vijana wa Somalia. Ninatumia mitandao ya kijamii na kutuma taarifa kuhusu safari yangu baadaye kwa maandishi na matangazo," Faisal Abdullahi Ali alisema kwa BBC.

      Faisal alisema kuwa aliamua gharama ya safari hii na anaifadhili yeye mwenyewe.

      Katika safari hii, anataka kufikia ncha ya kusini kabisa ya bara la Afrika Kusini.

      "Sehemu ya kuvutia zaidi ya safari yangu ilikuwa Kabila la Hadzabi, kabila pekee duniani ambalo liko mbali na ustaarabu na linaishi kwa kutegemea uwindaji ," alisema Faisal.

      Safari ya kufurahisha

      h

      Chanzo cha picha, Fasal

      Kabila hili linaishi kaskazini mwa Tanzania na ni moja ya makabila ambayo bado yanaishi katika misitu ya mbali ya nchi hiyo.

      Faisal alisema kwamba amependezwa na maisha ya watu hawa.

      "Wanapoishi na kile wanachovaa kinavutia, kwahivyo unajiuliza je tuliishi hivi zamani?" Alisema Faisal.

      Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu wanaosafiri kwa pikipiki katika mabara na nchi zinazotaka kufikia malengo tofauti.

      Baadhi ya watu hawa wanataka kuweka rekodi mpya katika uwanja wa usafiri, wakati wengine wanatengeneza habari ili kutangaza, wakati wengine wanataka kupata uzoefu.

      g

      Chanzo cha picha, Faisal

      Maelezo ya picha, Faisal ni kijana MwanaYouTube aliyezaliwa na kukulia huko Garisa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

      Unaweza pia kusoma:

    • Kizaazaa kikubwa mjini Seoul huku wachunguzi wakijaribu kumkamata rais wa Korea Kusini

      h

      Chanzo cha picha, AFP

      Ofisi ya Juu ya upelelezi wa uhalifu wa viongozi wa Umma inayopeleleza makosa ya ufisadi ilitangaza kwamba itaanza kutekeleza agizo la kukamatwa kwa Rais Yoon Seok-yeol saa 8:07 za asubuhi asubuhi Ijumaa tarehe 3, lakini jaribio hilo limezuiwa.

      Inaarifiwa kuwa wachunguzi na maafisa wa polisi wapatao 80 kutoka Shirika la Uchunguzi wa Ufisadi walioingia kwenye lango kuu la makazi ya Yongsan wako kwenye mtafaruku, wameshindwa kuingia ndani ya jengo hilo kutokana na kizuizi cha ulinzi.

      Magari yaliyokuwa yamewabeba wachunguzi wa taasisi ya uchunguzi wa rushwa yaliondoka katika eneo la Serikali ya Gwacheon mwendo wa saa 6:14 asubuhi na kufika karibu na makazi ya Rais huko Hannam-dong mwendo wa saa 7:20 asubuhi.

      Kwasababu lango kuu lilikuwa limefungwa na magari, wachunguzi wapatao 80 kutoka Ttasisi ya uchunguzi wa rushwa na polisi waliingia ndani ya nyumba hiyo kwa miguu. Majibizano mengine yalizuka na wafanyakazi wa usalama, lakini waliingia lango kuu bila mzozo wowote mkubwa.

      Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi, ilishindwa kuingia ndani ya jengo hilo kutokana na walinzi kuwazuia.

      Wachunguzi wana hadi tarehe 6 Januari kumkamata Yoon, kabla ya hati hiyo kuisha muda wake.

      h

      Chanzo cha picha, EPA

      Maelezo ya picha, Gari lililokuwa limebeba wachunguzi wa shirika la uchunguzi wa Ufisadi liliwasili karibu na Makazi ya Rais huko Yongsan mwendo wa saa 7:20 asubuhi.

      Sio mara ya kwanza kushindwa kumkamata Yoon

      Mnamo tarehe 2, polisi walikadiria kuwa maelfu hadi 10,000 walikusanyika karibu na makazi ya rais huko Hannam-dong, Yongsan-gu, Seoul. Wawakilishi Yoon

      Hapo awali, ofisi ya Upelelezi wa ufisadi ilipokea hati ya kukamatwa na hati ya upekuzi kutoka kwa mahakama mnamo tarehe 31 mwezi uliopita baada ya Rais Yoon kushindwa kujibu agizo la kujisalimisha mara tatu.

      Ingawa hakukuwa na ajali kubwa katika eneo la tukio, baadhi ya wafuasi walipambana na polisi na washiriki wa maandamano ya kupinga mashtaka waliokuwa karibu, wakipaza sauti zao, au kulala chini barabarani na kuchukuliwa na polisi, na kusababisha hali ya migogoro.

      Unaweza pia kusoma:

    • Hujambo na karibu kwa matangazo haya ya mubashara ya Imuaa tarehe 03.01.2025

    Trending Now