Uingereza haitajiunga na Marekani na Israe katika mashambulizi dhidi ya Iran - Waziri Mkuu
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema kwamba Marekani imeomba ruhusa ya kutumia kambi za Uingereza ili kuweza kusitisha mashambulizi ya makombora ya Iran kwenye vyanzo vya kuhifadhia makombora au maeneo yanatayarishwa katika ufyatuaji makombora.
Waziri mkuu anasema alikubali ombi hili jipya "ili kuzuia Iran kufyatua makombora kote katika eneo hilo" na kuwaua raia.
Hata hivyo, amesisitiza kwamba Uingereza haiungi mkono mashambulizi ya Marekani na Israel.
Waziri mkuu anasema Ufaransa na Ujerumani pia ziko tayari kuruhusu shughuli za Marekani kwenye kambi zao ili kuharibu uwezo wa Iran wa kurusha makombora.
Starmer pia amesema vituo vya Uingereza huko Cyprus havitumiwi na ndege za kivita za Marekani
Starmer ameongeza kuwa jana usiku ndege isiyo na rubani ilishambulia RAF Akrotiri huko Cyprus. Anasema kwamba ni muhimu kwake kusema kwamba kambi zetu huko Cyprus hazitumiwi na ndege za Marekani za mabomu.
Waziri Mkuu anaongeza kuwa shambulizi dhidi ya RAF haukuwa kutokana na uamuzi wowote tuliochukua.
Soma zaidi: