Wabunge wa chama tawala cha Korea Kusini cha People Power Party (PPP) 107 kati ya 108 wa chama tawala, 107 wameondoka bungeni kabla ya kura ya kumuondoa madarakani tais wa nchi hiyo. Wabunge sasa waliztarajiwa kupigia kura hoja ya kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol anayezongwa na kashfa.
Huenda chama hicho kilitumia mkakati wa kususia upigaji kura ili kuzuia watu kuasi, kwani kura ya kumuondoa ni kupitia kura zisizojulikana.
Ahn Cheol-soo, profesa aliyegeuka kuwa mwanasiasa ambaye aliwania urais mwaka wa 2012, 2017 na 2022, ndiye mwanachama pekee wa PPP ambaye amesalia katika kiti chake.
Ahn amekuwa akisema mara kwa mara kuwa atapiga kura ya kufunguliwa mashtaka ikiwa rais hatajiuzulu kwa hiari kabla ya upigaji kura.
Wabunge wa wengi wa vyama vya upinzani wamekusanyika bungeni . Walikimbia mara tu wabunge walipoanza kuondoka, wakijaribu kuwazuia kuondoka.
Walikuwa wakiimba "wasaliti" na "rudi tena kupiga kura".
Kuna hasira kubwa. Ni mwanachama mmoja tu au wawili wa chama tawala ambao bado wamesalia ndani ya ukumbi, ikimaanisha kuwa kura hii sasa haitapigwa, amesema mwandishi wa BBC mjini Seol.
Nje ya bunge, kulikuwa na umati wa watu huku Wakorea wengi zaidi wakikusanyika kwenye barabara ya bunge la ttaifa. Polisi wameimarisha hali ya usalama.
Maandamano hayo yapo karibu na kituo cha treni ya chini ya ardhi, na vizuizi vikubwa vinaweza kuonekana kwenye kituo cha usafiri mapema huku watu wakimiminika.
Mamlaka iliamua kufunga kituo hicho, na polisi wamepanga mistari kwenye maeneo mbalimbali kuongoza umati wa watu wanaoandamana.