Safari za meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz zinapaswa kuendelea: Xi Jinping

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa China Xi Jinping anasema "safari za kawaida za meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz "zinapaswa kuendelea".
Alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman siku ya Jumatatu.
Xi alisema kuwa njia hiyo muhimu ya baharini inapaswa kubaki wazi kwa matumizi ya kawaida, kwa sababu ni kwa manufaa ya nchi za eneo hilo pamoja na jamii ya kimataifa kwa ujumla.
Kwa upande mwingine rais wa Marekani Donald Trump na Xi wanatarajiwa kukutana nchini China mwezi Mei, baada ya safari hiyo kuahirishwa awali kutokana na vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Unaweza kusoma pia:





