Moja kwa moja, Mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Iran yanaanza nchini Pakistan

Televisheni ya Taifa ya Iran yaonya kuwa mazungumzo yanaweza kufutwa ikiwa masharti ya Tehran hayatatimizwa.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Afisa wa Marekani anakanusha madai kwamba Washington imekubali kuachia mali ya Iran

    Vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba afisa mmoja wa Marekani amekanusha kuwa mali Iran iliyofungiwa imeachiwa, licha ya ripoti za awalikudai hilo.

    Spika wa Bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf, ambaye anaongoza ujumbe huo, alikuwa amesema sharti hilo lazima litimizwa kabla hata mazungumzo kuanza.

    Vyanzo vya habari ndani ya serikali ya Pakistan na ujumbe wa Iran vimeiambia BBC kuwa Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alikutana na maafisa wakuu wa Iran.

    Picha ya Sharif akikutana na Makamu wa Rais wa Marekani JD pia Vance ilitolewa.

  2. Vance akutana na Waziri Mkuu wa Pakistan

    .

    Chanzo cha picha, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistan

    Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amekutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif.

    Alisaidiwa na mjumbe maalum Steve Witkoff na Jared Kushner, na Sharif alionyesha matumaini kwamba mazungumzo haya yatatumika kama hatua ya kuelekea amani ya kudumu katika eneo hilo, kulingana na taarifa kutoka ofisi ya mawaziri wakuu wa Pakistan.

    Hapo awali ujumbe wa Iran pia ulikutana na Sharif.

    Endelea kuwa nasi kwa taarifa za hivi punde kuhusu mazungumzo ya amani kati ya Iran na Marekani

  3. Mazungumzo yanaweza kufutwa ikiwa masharti ya Tehran hayatatimizwa - ripoti

    Mwandishi kituo cha habari cha serikali ya Iran IRINN ambaye anaripoti moja kwa moja kutoka Islamabad ameonya kwamba mazungumzo huenda yakafutwa ikiwa masharti ya Iran hayatazingatiwa.

    Alisema kujiondoa kwenye mazungumzo ambayo hayaheshimu "maslahi na matakwa " ya Iran kunaweza kutazamwa kama "mafanikio" kwa kile maafisa wanachokielezea kama "diplomasia ya uthubutu".

    Mapema asubuhi ya leo, mwandishi huyo pia alisema wajumbe wa Iran walitarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif kwanza, ambapo maelezo zaidi - ikiwa ni pamoja na muda wa mazungumzo yoyote na ujumbe wa Marekani - yanaweza kuwekwa wazi.

    Ripoti zinasema kuwa Iran inaweza kuendelea mbele bila mazungumzo ikiwa masharti yake hayatatekelezwa.

    Maelezo zaidi:

  4. Wapatanishi wa Iran wakutana na Waziri Mkuu wa Pakistan

    Wajumbe wa Iran, akiwemo Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf (katikati) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi (kushoto) waliwasili Islamabad mapema leo.

    Chanzo cha picha, Iranian Foreign Ministry/EPA

    Maelezo ya picha, Wajumbe wa Iran, akiwemo Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf (katikati) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi (kushoto) waliwasili Islamabad mapema leo.

    Chanzo katika serikali ya Pakistan kimeiambia BBC kwamba Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, amekutana na ujumbe wa Iran wakati wa chakula cha mchana.

    Kama ilivyokuwa katika mazungumzo ya awali, kuna uwezekano wa Pakistan kukutana na maafisa wa Marekani na baadaye na ujumbe wa Iran ili kubaini kama kuna hatua yoyote inayoweza kufikiwa katika mapendekezo yao.

    Spika wa bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf, ambaye anaongoza ujumbe huo, amesema Marekani lazima ikubali kuachia mali ya Iran kabla hata mazungumzo kuanza.

    Ripoti kutoka Iran zinaashiria kwamba hili limefanyika, lakini hilo halijathibitishwa na upande wa Marekani, na litakuwa suala gumu kumshawishi Donald Trump nchini Marekani.

    Soma zaidi:

  5. Katika picha: Hali ilivyo mjini Islamabad

    Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabadtaifa hilo likijiandaa kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran baadaye leo.

    Tayari wajumbe wa pande zote mbili wamesili mjini humo.

    Hiz hapa mkusanyiko wa picha zinazoonyesha hali ilivyo.

    Maafisa wa usalama wakishika doria kwenye barabara inayoelekea Hoteli ya Serena ambako mazungumzo yanatarajiwa kufanyika leo, Islamabad, Pakistan, Aprili 11.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Maafisa wa usalama wakishika doria kwenye barabara inayoelekea Hoteli ya Serena ambako mazungumzo yanatarajiwa kufanyika leo, Islamabad, Pakistan, Aprili 11.
    Bango lililo na ujumbe "Pakistan, Mlinzi wa Amani," likiwa na picha za viongozi wa kisiasa wa Pakistan, Mkuu wa Jeshi Asim Munir, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, na Waziri Mkuu wa zamani Nawaz Sharif, Lahore, Pakistani, Aprili 11.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Bango lililo na ujumbe "Pakistan, Mlinzi wa Amani," likiwa na picha za viongozi wa kisiasa wa Pakistan, Mkuu wa Jeshi Asim Munir, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, na Waziri Mkuu wa zamani Nawaz Sharif, Lahore, Pakistani, Aprili 11.
    Maafisa wa polisi wakikagua magari kama sehemu ya hatua za usalama kwenye barabara inayoelekea Red Zone, eneo la ofisi ya serikali ambapo mazungumzo yanatarajiwa kufanyika, Islamabad, Pakistan, Aprili 11.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Maafisa wa polisi wakikagua magari kama sehemu ya hatua za usalama kwenye barabara inayoelekea Red Zone, eneo la ofisi ya serikali ambapo mazungumzo yanatarajiwa kufanyika, Islamabad, Pakistan, Aprili 11.
    Mwanamume akiwa ameshikilia rundo la magazeti yenye kichwa cha habari "Islamabad iko tayari kwa mazungumzo muhimu," Lahore, Pakistan, Aprili 11.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mwanamume akiwa ameshikilia rundo la magazeti yenye kichwa cha habari "Islamabad iko tayari kwa mazungumzo muhimu," Lahore, Pakistan, Aprili 11.
    Msafara wa magari unaoaminika kuwabeba maafisa wa Saudia kushiriki katika mazungumzo hayo, Islamabad, Pakistan

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Msafara wa magari unaoaminika kuwabeba maafisa wa Saudia kushiriki katika mazungumzo hayo, Islamabad, Pakistan
  6. Rais wa Djibouti Guelleh ashinda muhula wa sita madarakani

    AFP via Getty Images

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh

    Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh ameshinda uchaguzi uliosusiwa na upinzani, baada ya kupata zaidi ya asilimia 97.81 ya kura zilizopigwa, data rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Jumamosi ilionyesha.

    Kura ya Ijumaa ilimkutanisha mpinzani mmoja pekee na aliyemaliza muda wake, Mohamed Farah Samatar. Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani zilionyesha kuwa aliibuka wa pili kwa 2.19% ya kura 168,233 zilizopigwa.

    Guelleh alishinda uchaguzi uliopita wa 2021, ambao pia uliosusiwa na wagombea wengi wa upinzani, kwa zaidi ya 97% ya kura.

    Alikuwa ametangaza kujiuzulu mwaka huu, lakini marekebisho ya katiba mwezi Novemba yaliondoa ukomo wa umri wa juu wa miaka 75 kwa wagombea urais.

    Wakosoaji wamepuuza matokeo ya uchaguzi huo wakisema haukua na ushindani, huku wafuasi wakihoji kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 ameleta utulivu katika taifa hilo la kimkakati la Pembe ya Afrika.

    Mpinzani maarufu Daher Ahmed aliiambia BBC kwamba wanasusia uchaguzi nchini Djibouti kwa sababu hawaruhusiwi kuwa na uchaguzi huru na wa haki, jambo ambalo wanaamini linadhoofisha mchakato wa kidemokrasia na uhalali wa matokeo ya uchaguzi.

    Kampeni ya Rais Ismail Omar Gelleh ilijikita zaidi katika kuleta utulivu huku kukiwa na mvutano wa kikanda, hasa unaohusishwa na migogoro katika Mashariki ya Kati, wakati Samatar amejikita katika mageuzi ya kiuchumi na elimu.

    Rais huyo amekuwa madarakani tangu mwaka 1999 na ndiye rais wa pili wa nchi hiyo tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1977.

  7. Guterres atoa wito kwa Iran na Marekani kufanya mazungumzo kwa 'nia njema'

    António Guterres

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anakaribisha mazungumzo ya amani ya Marekani na Iran yaliyopangwa na kuzitaka pande zote mbili kuingia katika mazungumzo hayo kwa "nia njema".

    Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa, msemaji wa katibu mkuu Stephane Dujarric alisema Guterres "anatoa wito kwa wahusika kuchangamkia fursa hii ya kidiplomasia kushiriki mazungumzo kwa nia njema kuelekea makubaliano ya kudumu."

    "Katibu Mkuu anasisitiza kwamba hakuna njia mbadala inayofaa kwa utatuzi wa mizozo ya kimataifa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Umoja wa Mataifa," Dujarric alisema.

    Mjumbe binafsi wa Guterres yuko katika eneo hilo kusaidia juhudi za kidiplomasia, aliongeza.

    Soma zaidi:

  8. Makamu wa Rais wa Marekani Vance awasili Pakistan kwa mazungumzo ya amani

    .

    Chanzo cha picha, POOL

    Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amewasili mjini Islamabad muda pamoja na ujumbe wa Marekani, chanzo cha usafiri wa anga kimeiambia BBC.

    Anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo na Iran baadaye leo, pamoja na mjumbe maalum Steve Witkoff na Jared Kushner.

    Vance na timu yake ya wapatanishi waliondoka Marekani kuelekea Pakistan jana, na kabla hajaondoka, makamu wa rais aliwaambia waandishi wa habari kuwa "anatazamia mazungumzo yenye tija", lakini akaonya Iran "isijaribu kuichezea" Marekani kwania haitakubali.

    Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani Mohammad Ishaq Dar amepongeza dhamira ya Marekani ya kufikia amani ya kudumu ya kikanda na kimataifa alipompokea JD Vance mjini Islamabad.

    Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, Dar imenukuliwa ikisema anatumai Iran na Marekani "zitajadiliana kwa amani, na kusisitiza hamu ya Pakistan ya kuwezesha pande husika kufikia suluhisho la kudumu la mzozo huo".

    Tutakufahamisha yote yatakayojiri nchini Pakistan. Endelea nasi.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Katika Picha: Jinsi wanaanga wa Artemis II walivyorejea duniani

    Shirika la anga la Marekani NASA limetoa picha za wanaanga wakirejea duniani kwa chombo cha Orion.

    Picha zinaonyesha msururu wa matukio kutoka walipotua kwa myavuli kwenye bahari ya Pacific hadi walipotembeakuelekea kwenye ndege ya USS John P Murtha iliyokuwa ikisubiri kuwapeleja katika kituo cha matibabu ili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

    .

    Chanzo cha picha, NASA/Joel Kowsky

    .

    Chanzo cha picha, NASA/Bill Ingalls

    .

    Chanzo cha picha, NASA/Joel Kowsky

    .

    Chanzo cha picha, NASA/Bill Ingalls

    .

    Chanzo cha picha, NASA/Bill Ingalls

  10. Wanaanga wa Artemis II waatua salama baada ya kukamilisha safari ya kihistoria mwezini

    .

    Chanzo cha picha, NASA

    Kikosi cha wanaanga wa Artemis II kimerejea salama duniani baada ya kukamilisha safari yao kihistoria mwezini.

    NASA ilitoa picha nzuri zilizopigwa kutoka upande wa mbali wa Mwezi wakati wa misheni hiyo.

    Mojawapo ya kuvutia zaidi ni picha hii, ambayo Nasa imeiita Earthset.

    Inaonyesha Dunia ikiwa nyuma ya upeo wa Mwezi - picha maarufu ya Earthrise iliyopigwa wakati wa misheni ya Apollo 8.

    Picha nyingine inaonyesha Mwezi ukilifunika Jua. Wanaanga walipata fursa ya kipekee ya kujionea tukio hilo kwa karibu dakika 54 walipokuwa wakipita nyuma ya Mwezi.

    Kutoka ndani ya chombo cha Orion wanaanga waliweza kuona Dunia inayokaa kama mwezi mwandamo ikiongezeka kwa ukubwa polepole nyuma yao walipokuwa wakiendelea na safari yao ya nje ya maili 250,000 (400,000km).

    Kufikia umbali huo kutoka duniani hadi Mwezini kungewachukua siku nne.

    Hakuna mtu ambaye ameenda mbali sana na dunia, isipokuwa wanaanga wa Artemis II

    Maelezo zaidi:

  11. Natumai hujambo.

Trending Now