Tunapoingia siku ya 13 ya uvamizi wa Warusi nchini Ukraine, haya hapa ni baadhi ya matukio makuu kutoka saa 24 zilizopita:
• Ukraine inasema mashambulizi ya Urusi yanawazuia raia kuondoka kwa usalama katika miji yao iliyozingirwa
• Makumi ya maelfu ya watu kote Ukraine hawana kawi na, katika mji wa bandari wa Mariupol, wanakosa chakula na maji.
• Duru ya tatu ya mazungumzo ya amani kati ya Russia na Ukraine yamalizika kwa makubaliano madogo. Raundi ya nne itafanyika Jumanne
• Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimeapa kuendelea kupandisha gharama kwa Urusi kwa uvamizi wake wa "bila sababu" dhidi ya Ukraine.
• Urusi ilitishia kupunguza uagizaji wake wa gesi asilia Ulaya kama kulipiza kisasi kwa vikwazo vya Magharibi
• Katika hotuba yake ya hivi punde ya video, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema atakaa Kyiv "ilimradi tu kushinda vita hivi"
• Coca-Cola na McDonalds ni miongoni mwa makampuni yanayokabiliwa na uwezekano wa kususia wateja kwa kushindwa kwao kujiondoa nchini Urusi.
• Ukraine inasema imemuua kamanda mkuu wa jeshi la Urusi katika vita karibu na Kharkiv - madai hayo hayajathibitishwa na BBC
Kiongozi wa kijeshi wa Urusi auawa vitani, yasema Ukraine
Kamanda wa ngazi za juu katika jeshi la Urusi ameuawa wakati wa mapigano karibu na Kharkiv, kulingana na wizara ya ulinzi ya ujasusi ya Ukraine.
BBC haiwezi kuthibitisha dai hilo kwa uhuru; Maafisa wa Urusi hawajatoa maoni yoyote.
Kulingana na taarifa kutoka wizara ya ulinzi ya Ukraine, Vitaly Gerasimov alikuwa jenerali mkuu, na naibu kamanda wa kwanza wa Jeshi la 41 la Wilaya ya Kati ya Kijeshi ya Urusi.
Idadi ya maafisa wakuu wa jeshi la Urusi pia waliuawa na kujeruhiwa, inasema.
Ujasusi wa Ukraine unasema Gerasimov alishiriki katika vita vya pili vya Chechnya na operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Syria. Alipokea medali "kwa kuirejesha Crimea".
Maafisa wa Ukraine walituma picha ya mtu waliyesema kuwa ni Gerasimov kwenye ukurasa wa Twitter, yenye neno "Amefutwa" kwa herufi nyekundu chini kabisa.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine