UEFA-Mfumo mpya wa Upigaji wa Mikwaju ya Penalti

Mfumo wa sasa ukiwa unatoa changamoto kwa wapigaji
Maelezo ya picha, Mfumo wa sasa ukiwa unatoa changamoto kwa wapigaji

Shirikiksho la kandanda barani Ulaya UEFA Lipo katika mikakati ya kufanya majaribio mfumo mpya wa upigaji wa mikwaju ya Penalti mitano mitano ili kuondoa faida ya timu inayoanza kupiga Penalti hizo.

Chelsea

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, mfumo mpya wa mikwaju ya penalti

Mfumo huo mpya, ambao unatambuliwa kama ABBA, utatumika kwa timu ya kwanza itayotambulika kama timu A kupiga penalti ya kwanza na kisha timu B kupiga penalti ya pili na ya tatu na kisha timu B kupiga penalti ya nne na ikifuatia zamu ya timu A kupiga Penalti ya 5 na ya 6 kwa kupokezana hivyo kila moja kukamilisha Penati 5.

Mfumo huo umependekezwa na IFAB ambacho ni chombo pekee chenye mamlaka ya kubadili sheria za soka.