Hatari ya kuwa mwanahabari ukiwa Urusi - Steve Rosenberg

.
Muda wa kusoma: Dakika 6

Katika kipindi chake cha televeshini nchini Urusi, mwanahabari maarufu anaishambulia Uingereza.

Nashukuru sio yeye wakubonyeza kitufe cha kulipua mabomu ya nyuklia.

"Bado hatujaishambulia London wala Birmingham," anasema Vladimir Solovyov.

"Bado hatujawaondoa Waingereza wote kwenye dunia hii "

Alionekana kukatishwa tamaa.

"Bado hatujaifurusha BBC na yule Steve Rotten-berg, anatembea kama kichakuro kinachoenda haja, ni adui wa taifa hili! "

Karibu katika dunia yangu: Kile anachokipitia mwanahabari wa BBC nchini Urusi

Filamu ya BBC Panorama, inaangazia maisha ya wanahabari wa BBC mjini Moscow, wakati ambapo Ikulu ya Kremlin inaendeleza vita vyake nchini Ukraine, kudhibiti hali nchini humo, huku wakijaribu kujenga uhusiano na rais wa Marekani Donald Trump.

Kuitwa kichakuro hakunisumbui mimi. Ni wanyama wazuri na wanaweza kustahimili magumu wanayopitia, kitu ambacho nakihitaji kama mwanahabari hapa.

Ila kuitwa 'adui wa Urusi' hiyo inaniuma.

.

Chanzo cha picha, Solovyov Live, VGTRK

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nimeishi na kufanya kazi mjini Moscow kwa zaidi ya miaka thelathini. Nikiwa kijana nilipenda sana lugha, fasihi na muziki wa Urusi.

Katika chuo kikuu cha Leeds, niliongoza kwaya ambayo iliimba ngoma za jadi za Urusi. Katika shindano moja la muziki, nilitunga wimbo kwa lugha ya Kirusi kuhusu sanamu ya mtu wa theluji, ambaye alivaa nguo nyingi hadi akayeyuka.

Kama sanamu ya theluji , Urusi niliyoijua ilionekana kuyeyuka mnamo Februari 2022. Katika uvamizi wake dhidi ya Ukraine, nchi kubwa zaidi duniani ilikuwa imechagua njia yenye 'giza.'

"Operesheni maalum ya kijeshi" ya Rais Putin iligeuka kuwa vita vya umwagaji damu ambavyo havijawahi kutokea barani Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.

Tukifikiria siku za nyuma, haya hayakuanza tu ghafla: Urusi ilikuwa imetwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014; tayari ilikuwa imetuhumiwa kufadhili, kuchochea na kuratibu uasi mashariki mwa Ukraine.

Uhusiano na nchi za Magharibi ulikuwa umedorora. Hata hivyo, uvamizi kamili nchini Ukraine, ulikuwa tukio la kihistoria lililobadilisha mwelekeo wa mambo mengi.

Katika siku zilizofuata, sheria mpya kandamizi zilipitishwa, ili kuwanyamazisha upinzani na kuadhibu yeyote anaye kosoa mamlaka ya Urusi.

Majukwaa ya BBC yalizuiwa. Ghafla, kuripoti kutoka Urusi ikawa ni 'kama kutembea juu ya kamba nyembamba kwenye uwanja uliojaa mabomu.'

Changamoto ilikuwa kuripoti kwa usahihi na uaminifu kuhusu yaliyokuwa yakitokea bila kujipata matatani.

Mnamo mwaka 2023, kukamatwa kwa mwandishi wa Wall Street Journal kulionyesha kwamba kuwa na pasipoti ya nchi ya nje "sio kinga ya kukuepusha kufungwa jela."

Evan Gershkovich, raia wa Marekani, alihukumiwa kwa mashtaka ya ujasusi. Alikaa gerezani kwa miezi kumi na sita. Yeye, mwajiri wake pamoja na mamlaka za Marekani walilaani kesi hiyo na kusema kwamba haikuwa na msingi wowote.

Katika ofisi ya BBC jijini Moscow, tupo timu ndogo zaidi. Kwa pamoja tunajaribu kukabiliana na changamoto za kila siku za kuripoti habari zinazohusu Urusi.

Mtayarishaji wa vipindi na taarifa Ben Tavener na mimi mara nyingi tunakumbana na kile kinachoitwa "ukaguzi wa ziada" tunaposafiri kuingia na kutoka Urusi.

Waandishi wa habari kutoka nchi zilizotajwa kuwa "zisizo rafiki" na Urusi (ikiwemo Uingereza) hawapewi tena vibali vya mwaka mmoja.

Viza zetu za uandishi wa habari pamoja na kadi za vibali zinahitaji kusasishwa kila baada ya miezi mitatu.

Wale ambao walikuwa wanatusaidia kupata taarifa n ahata kwenye uchambuzi wengi wao kwa sasa hawatoi ushirikiano.

Pengine wanafikiria wakati wa mvutano na wasiwasi wa kimataifa kama nyakati hizi, kuhusishwa na BBC kunaweza kuhatarisha maisha yao.

n

Chanzo cha picha, Steve Rosenberg

Hata hivyo, pamoja na vyombo vingine vya habari vya kimataifa ambavyo bado vipo nchini Urusi, tumekuwa tukipokea mialiko ya kuhudhuria mikutano ya waandishi wa habari ya Urusi.

Wakati mwingine mimi hupata fursa ya kumuuliza maswali Rais Putin.

Hata swali moja tu na jibu lake katika mkutano na waandishi wa habari kunaweza kutoa mwanga kuhusu namna rais huyo anavyofikiria.

Vladimir Putin anaongozwa na hisia za chuki dhidi ya Magharibi: suala la NATO kutaka mataifa ya mashariki kujiunga nao, na kile anachokiona kuwa ni miaka mingi ya Urusi kutoheshimiwa na viongozi wa Magharibi.

Wakosoaji wake wanamtuhumu kuwa na hulka za kiimla, wakisema anajaribu kuongeza ushawishi wake nchini Urusi.

"Je, kutakuwa na 'operesheni mpya maalum za kijeshi'?" nilimuuliza Rais Putin mwezi Desemba kama sehemu ya swali pana kuhusu mipango yake.

"Hakutakuwa na operesheni zozote ikiwa mtatuheshimu. Ikiwa mtaheshimu maslahi yetu…" alijibu kiongozi huyo wa Kremlin.

Hilo linaibua swali: iwapo Vladimir Putin ataamua kuwa maslahi ya Urusi hayajaheshimiwa, nini kitafuata?

Urusi inaona kuwa Marekani imeanza kuiheshimu baada ya kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House.

Katika mkutano wa kilele wa Alaska uliofanyika mwezi Agosti, rais wa Marekani alimkaribisha kwa heshima kubwa kiongozi wa Urusi. Alimwalika Putin mjini Anchorage, na kumrejesha katika ulingo wa kimataifa baada ya kutengwa kwa muda mrefu, ingawa mkutano huo haukufanikiwa kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.

Sio kila kitu kinaenda sawa kwa Moscow. Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa Urusi, alikamatwa hivi karibuni na majeshi ya Marekani.

Marekani pia ilizuia meli ya mafuta ambayo ilikuwa na bendera ya Urusi iliyokuwa ikihusishwa na mafuta ya Venezuela katika Bahari ya Atlantiki hatua ambayo Moscow ilaani vikali.

Moscow inaamini kwamba uhusiano mzuri na utawala wa Trump unaweza kuwasaidia kumaliza vita vya Ukraine kwa masharti yenye kunufaisha Urusi.

Kwa sasa, hotuba nyingi za kupinga mataifa ya Magharibi katika vyombo vya habari vya serikali ya Urusi hazielekezwi sana dhidi ya Marekani, bali zaidi dhidi ya Umoja wa Ulaya na Uingereza.

Namna nyakati zilivyobadilika

Mnamo mwaka 1997 niliitwa kwenye kipindi cha televisheni cha The White Parrot Club, kipindi maarufu cha vichekesho nchini Urusi kilichokuwa na kasuku mweupe anayeitwa Arkasha.

Watu mashuhuri wa Urusi waliketi katika meza hiyo wakifanya utani kwa lugha ya Kiingereza na kuzungumza kwa upendo kuhusu Uingereza.

Lakini katika kipindi cha miaka thelathini, tumetoka kutoka kwa "kasuku weupe" hadi kwa "kichakuro kinachoenda haja."

Cha kusikitisha zaidi, tumetoka katika kipindi cha kutarajia kuwa na urafiki kati ya mataifa ya mashariki na magharibi, hadi vita vya zaidi ya miaka minne haswa nchini Ukraine.

Namna ambavyo vita hivi vitamalizika havitaathiri tu mustakabali wa Ukraine na wa Urusi, bali pia mustakabali wa Ulaya.

.

Chanzo cha picha, FP via Getty Images

Kipindi cha miaka minne iliyopita, kumekuwa na wakati ambapo nimeshangazwa sana. Sitawahi kusahau mazungumzo yangu na mwanamke mmoja kwa jina Vera kwenye mkutano wa kisiasa wa kumuunga mkono Putin mwaka 2022.

Niliimuuliza kama ana mtoto wa kiume. Na akasema kuwa alikuwa naye.

"Je, huna hofu, kwamba anaweza kuingizwa jeshini na kutumwa Ukraine?," nilimuuliza.

"Ningependelea mtoto wangu afe akipigana Ukraine kuliko kumwona akiwa tu nyumbani akitaabika," Vera alijibu. "Angalia ni vijana wangapi hapa hawana kazi na wanatumia muda wao kunywa pombe?," alijibu.

Pia, kumekuwa mambo mazuri. Siku chache baada ya mwanahabri wa kipindi kimoja cha televesheni, Vladimir Solovyov kusema kuwa mimi ni "adui wa Urusi," Warusi kadhaa walikuja kwangu kunisifu na kutaka kupiga picha na mimi.

Ni kama nembo ya Urusi: tai mwenye vichwa viwili. Kichwa kimoja kinanguruma na kukuita " kichakuro anayejisaidia haja kubwa."

Mwingine anasema: "Asante kwa kuwa hapa."