Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Chelsea kuharakisha usajili wa Messi
Chelsea inaweza kuharakisha mipango ya kumsajili winga wa Ufaransa Rayane Messi, 18, kutoka Strasbourg huku Bayern Munich, Barcelona na Paris St-Germain pia zikimtaka. (Teamtalk)
Maajenti kutoka Manchester City, Liverpool, Arsenal, RB Leipzig, Borussia Dortmund na Barcelona wanamfuatilia kwa karibu beki raia wa Uingereza na timu ya Newcastle, Lewis Hall mwenye umri wa miaka 21. (Caughtoffside)
Manchester City pia inaweza kumsajili beki wa Uhispania, Pedro Porro, 26, kwa bei ya chini sana kuliko thamani yake ya pauni milioni 80 kutokana na hali ya kifedha ya Tottenham ikiwa watashushwa daraja. (Football Insider)
Sunderland wako tayari kulipa euro milioni 15 (£12.9m) ili kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania, Thiago Pitarch, 18, kutoka Real Madrid. (Fichajes)
Klabu nchini Uingereza na kote Ulaya zimewasiliana na Liverpool kuhusu kipa wa Georgia mwenye umri wa miaka 25, Giorgi Mamardashvili. (Teamtalk)
Tottenham inawasiliana na makocha wanane kuchukua nafasi ya kocha Igor Tudor ambaye yuko chini ya shinikizo, huku Sean Dyche, Mauricio Pochettino na Roberto de Zerbi wakiwa miongoni mwao. (Talksport)
Crystal Palace wanatarajiwa kushindana na Leeds kumpata mshambuliaji wa Derby, raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 25, Patrick Agyemang. (Football Insider)