Israel yawaamuru raia kuondoka mara moja kusini mwa Lebanon
Jeshi la Israel limeonya wakazi wa miji na vijiji vyote kusini mwa Lebanon waondoke eneo hilo. Wameambiwa wahame kaskazini mwa mto Litani. Onyo hili limekuja kabla ya operesheni za kijeshi zinazotarajiwa kuanza mda wowote kuanzia sasa.
Watu watano wamefariki mjini Baalbek, mashariki mwa nchi hiyo, wakati Israel ilipofanya mashambulizi ya anga kabla ya alfajiri kote Lebanon.
Lebanon imekuwa ikilengwa baada ya Hezbollah kuanza kurusha makombora kuelekea Israel.
Pia kuna taarifa kwamba jeshi la Syria limepeleka nguvu za ziada katika mpaka wake na Lebanon.
Iran 'ilijaribu kumuua' Trump, asema Waziri wa Ulinzi wa Marekani
Chanzo cha picha, EPA
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth, ambaye amezungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, pamoja na Mwenyekiti wa Wakuu wa Wafanyakazi wa Marekani Dan Caine amesema kuwa "Iran ilijaribu kumuua Rais Trump", Hegseth alisema, na "Rais Trump alithibitisha" hilo.
Alisema kwamba siku ya Jumanne, Marekani "ilimwinda na kumuua" "kiongozi aliyejaribu kumuua Rais Trump".
Mnamo mwaka 2024, serikali ya Marekani ilimshtaki raia wa Afghanistan kuhusiana na njama ya Iran ya kumuua Trump kabla ya kuchaguliwa mwaka huo.
Idara ya Sheria ilidai kwamba Farhad Shakeri, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 51, alikuwa amepewa jukumu la "kutoa mpango" wa kumuua Trump.
Serikali ya Marekani ilisema wakati huo kwamba Shakeri inaaminika kuwa yuko Iran.
Katika malalamiko ya jinai yaliyowasilishwa katika mahakama ya Manhattan, waendesha mashtaka walidai kwamba afisa mmoja katika kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran alimwelekeza Shakeri mnamo Septemba kubuni mpango wa kumfuatilia na kumuua Trump.
Manowari ya Marekani yaizamisha meli ya kivita ya Iran katika Bahari ya Hindi - Hegseth
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amesema kwamba Marekani imezamisha "meli ya kivita ya Iran ambayo ilidhaniwa kuwa salama katika
"Ilizamishwa na kombora la chini ya maji," Hegseth amesema.
Hegseth hakutaja jina la meli ya Iran iliyoshambuliwa.
Lakini awali, jeshi la wanamaji la Sri Lanka liliripoti kwamba meli ya IRIS Dena ilizama katika Bahari ya Hindi, huku takriban watu 140 wakiwa hawajulikani walipo.
Chanzo cha picha, POOL
'Marekani inashinda,' asema Hegseth
Wakati huo huo, Waziri Pete Hegseth amesema: "Marekani inashinda pakubwa na bila huruma" vita hii.
"Tumefikisha siku nne pekee," anasema, lakini "kama Trump alivyosema" Marekani "itachukua muda wote tunaohitaji" kuhakikisha operesheni hiyo inafanikiwa.
Ulinzi wa anga wa Nato wadungua kombora la Iran kuelekea Uturuki
Chanzo cha picha, Ministry of Defence
Ulinzi wa anga wa Nato umeharibu kombora la Iran linaloelekea anga ya Uturuki, kulingana na wizara ya ulinzi ya Uturuki.
Katika taarifa, ambayo awali ilikuwa katika lugha ya Kituruki, wizara ya ulinzi inasema hakuna majeruhi.
Inasema kombora hilo "liligunduliwa likipita katika anga ya Iraq na Syria na kuelekea anga ya Uturuki".
"Tunaonya pande zote kujiepusha kuchukua hatua zozote zinazoweza kusababisha mzozo kuenea zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati," taarifa kutoka Uturuki, mwanachama wa Nato, inasema.
Mgogoro wa Mashariki ya Kati: Nigeria yasitisha safari ya Hija kwenda Israeli
Chanzo cha picha, Getty Images
Mamlaka ya Nigeria imesitisha safari zote za hija kwenda Israel mara moja, ikitaja wasiwasi wa kiusalama unaohusishwa na mzozo unaoongezeka Mashariki ya Kati.
Uamuzi huo ulitangazwa na Tume ya Kikristo ya Wahujaji wa Nigeria, chombo cha shirikisho kinachohusika na kuratibu mahujaji wa Kikristo.
Katika taarifa, tume hiyo ilisema hatua hiyo ni muhimu ili kuweka kipaumbele katika "usalama" wa mahujaji wa Nigeria.
Kusitishwa huko kunahusisha mipango yote ambayo tayari ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya safari za kiserikali na kibinafsi.
Maafisa walisema marufuku hiyo itasalia hadi hali katika eneo hilo itakapoimarika.
Maelfu ya Wakristo wa Nigeria husafiri hadi Israeli kila mwaka kwa ajili ya kuhiji katika maeneo takatifu kwenye Biblia huko Yerusalemu, Bethlehemu na Nazareti.
Safari hizo, ambazo mara nyingi hufadhiliwa au kuratibiwa na serikali za majimbo, ni sehemu muhimu ya kalenda ya kidini ya Nigeria.
Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika, lina idadi kubwa ya Wakristo, hasa kusini mwa nchi. Hija nchini Israeli inachukuliwa kuwa muhimu sana kiroho, huku washiriki wengi wakiweka akiba kwa miaka mingi ili kwenda safari hiyo.
Meli ya jeshi la wanamaji la Iran yazama pwani ya Sri Lanka
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Dena (nambari 75) aliyepigwa picha nchini Brazil mwaka 2023
Jeshi la wanamaji na anga la Sri Lanka limetumwa kuwaokoa mabaharia wa Iran, ambao walituma ishara ya dharura baada ya meli yao kuanza kuzama karibu na kisiwa hicho, mamlaka ya Sri Lanka yanasema.
Waziri wa mambo ya nje, Vijitha Herath, aliambia bunge kwamba ishara ya kutokea kwa hatari iliyojituma kutoka kwa meli "IRIS Dena" iliwafikia alfajiri. Inasemekana kulikuwa na watu 180 ndani ya meli hiyo.
Herath amesema mabaharia 30 waliojeruhiwa waliokuwa ndani ya meli hiyo wamesafirishwa hadi hospitalini katika bandari ya Galle nchini Sri Lanka.
Chanzo cha kuzama kwa meli hiyo hakijulikani. Mbunge wa upinzani aliuliza kama meli hiyo ilishambuliwa kwa bomu kama sehemu ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran - hakuna jibu rasmi lililotolewa.
Watu 140 hawajulikani walipo baada ya meli ya Iran kuzama pwani ya Sri Lanka
Wakati huo huo, jeshi la wanamaji la Sri Lanka limethibitisha kuwaokoa watu 32 baada ya kupokea simu ya dharura kutoka kwa meli ya wanamaji ya Iran 'IRIS Dena' mapema asubuhi ya leo.
Budhika Sampath, msemaji wa jeshi la wanamaji la Sri Lanka anasema: "Ingawa ilikuwa nje ya maji yetu, ilikuwa ndani ya eneo letu la utafutaji na uokoaji. Kwa hivyo tulilazimika kuchukua hatua kulingana na wajibu wa kimataifa."
Anaongeza kuwa: "Tuliwakuta watu wakielea juu ya maji, tukawaokoa, na baadaye tulipouliza tuligundua kuwa watu hao walikuwa wa meli ya Iran."
Pia anasema kwamba kulingana na nyaraka za meli hiyo watu 180 wanaaminika kuwa ndani yake, ingawa idadi kamili ya waliopotea haijulikani.
Msemaji huyo anasema wakati wa kuanza kwa shughuli za uokoaji hawakuona chombo hicho lakini waliona viraka vya mafuta juu ya maji na maboya ya kuokoa maisha yakielea.
Pia anaiambia BBC kwamba anakataa ripoti za shambulio la manowari lililosababisha kuzama, na kwamba chanzo cha ajali hiyo hakijulikani.
Habari za hivi punde, Israel yashambulia 'makao makuu ya usalama' mjini Tehran
Chanzo cha picha, UGC
Maelezo ya picha, Moshi ukifuka juu ya Tehran
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa Iimeshambulia makumi ya shabaha za kijeshi kote mjini Tehran, Msemaji wa Jeshi hilo Avichay Adraee ametangaza.
Mashambulizi hayo yalilenga makao makuu ya Basij - kikosi cha kijeshi chenye uhusiano na Walinzi wa Mapinduzi wa Iran - Ikiwa ni pamoja na zana za kurushia makombora na mifumo ya ulinzi, pamoja na "kurugenzi ya ugavi na usafirishaji inayoshirikiana na vikosi vya ardhini vya serikali".
Anaongeza kuwa IDF itaendelea "kuongeza mashambulizi yake" dhidi miundombinu ya serikali ya Iran.
Kambi ya Al Udaid yashambuliwa
Wakati huo huo Qatar imeshambuliwa kwa makombora mawili ya masafa marefu, Wizara yake ya Ulinzi inasema.
Moja kati ya makombora hayo ilizuiliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Qatar, huku moja ikigonga kambi ya Al Udaid -kambi kubwa ya jeshi la anga la Marekani katika eneo hilo.
Qatar inasema hakuna majeruhi waliyoripotiwa katika shambulio hilo.
Wanajeshi wa Marekani waliuuawa katika mzozo wa Iran watambuliwa
Chanzo cha picha, US Army Reserve Command
Jeshi la Marekani limewataja wanajeshi wake wa kwanza kuuawa katika mzozo kati ya Marekani na Iran.
Wanajeshi sita walikufa wakati "mfumo wa ndege isio na rubani" ulipokwepa ulinzi wa anga na kugonga kituo cha amri katika bandari ya Shuaiba, nchini Kuwait, Jumapili.
Kamandi Kuu ya Marekani hapo awali ilisema wanajeshi watatu walifariki katika shambulio hilo, lakini maafisa walithibitisha Jumatatu kwamba idadi ya waliofariki iliongezeka maradufu, baada ya mtu mmoja kufariki dunia kutokana na majeraha na miili miwili zaidi kupatikana kwenye vifusi.
Wanajeshi hao wa Akiba wa Jeshi la Marekani ni wa Kamandi ya 103 ya Ulinzi ya Des Moines, Iowa, ambao ni:
Kapteni Cody A. Khork, 35, wa Winter Haven, Florida
Sajenti Daraja la kwanza Noah L. Tietjens, 42, wa Bellevue, Nebraska
Sajenti wa Daraja la kwanza Nicole M. Amor, 39, wa White Bear Lake, Minnesota
Sajenti Declan J. Coady, 20, wa West Des Moines, Iowa
Siku ya Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kwamba ngome ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait ilipigwa wakati shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran.
Vifo hivyo sita pekee ndivyo vilivyothibitishwa na jeshi la Marekani tangu lilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa ushikiano na Israel.
Mataifa ya Ghuba yanatathmini jinsi ya majibu mashambulizi ya Iran
Chanzo cha picha, Reuters
Mataifa ya Ghuba yamejikuta katikati ya katika vita vipya vya Mashariki ya Kati, na yameghadhabishwa na hali hiyo.
Iran imelipiza kisasi mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel kwa kurusha mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani kuelekea majirani zake wa Kiarabu - kulenga kambi za kijeshi vya Marekani zilizopo kwenye himaya yao, lakini pia miundombinu ya kiraia na nishati.
Hatua hiyo ya Irana inabadili taswira ya Ghuba kuwa eneo salama, linalovutia wa wasafiri, utalii na fedha, na kuvuruga sekta ya mafuta na gesi katika msingi wake.
Hii ni vita ambayo serikali za Kiarabu hazikutaka na zilijaribu kuzuia. Swali ni kama watavutwa ndani yake na kile walichokiita mashambulizi ya "haini" ya Irani.
"Mipaka yote ya kisheria imevukwa," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al Ansari alisema katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne.
"Mashambulizi dhidi ya uhuru wetu yamefanyika mara kwa mara," aliwaambia waandishi wa habari.
"Miundombinu imeshambuliwa. Kuna mashambulizi yamefanywa maeneo ya makazi yetu. Na athari ya mashambulizi haya yako wazi. Inapokuja suala la kulipiza kisasi, uamuzi uko mikononi mwa uongozi wetu. Lakini tunapaswa kuweka wazi kwamba mashambulizi kama haya hayatafumbiwa macho."
Makombora mengi ya Iran yanazuiliwa katika eneo la Ghuba, lakini vifusi vinavyoanguka vimeanzisha moto na kuua watu
Ndege zisizo na rubani ambazo zinaweza kupenya kwa urahisi ulinzi wa anga mara nyingi husababisha uharibifu mdogo lakini huzua machafuko ambayo yavuruga biashara na usafiri.
Wanafunzi na wafanyakazi waliouawa katika shambulo dhidi ya shule ya Iran wazikwa
Chanzo cha picha, ISNA/WANA via Reuters
Wanafunzi na wafanyakazi waliuawa katika kile mamlaka ya Iran inasema kwamba ni shambulio la Marekani na Israel katika shule moja kusini mwa Iran wamezikwa.
Maafisa wa Iran walisema zaidi ya watu 160 waliuawa wakati shule ya wasichana iliposhambuliwa katika mji wa Minab siku ya Jumamosi, wakati Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi makubwa yakilenga kambi za kijeshi na uongozi wa Iran.
BBC haijafanikiwa kuthibitisha idadi ya vifo vilivyotolewa na mamlaka ya Iran.
Shule hiyo ilikuwa karibu na kambi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Jeshi la Marekani lilisema linachunguza ripoti za tukio hilo, huku jeshi la Israel likisema "halina habari" kuhusu operesheni zozote katika eneo hilo.
Mamia ya waombolezaji walimiminika barabarani kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi hayo ambayo yalirushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa ya Iran.
Majeneza yaliyokuwa yamefunikwa bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalibebwa katika umati wa watu, huku sauti ya kina mama walioshindwa kuhimili majonzi ya kina mama na baba waliopoteza mabinti zao zikisikika hewani.
Maafisa wa Iran wanasema shule hiyo ilishambuliwa kwa makombora matatu Jumamosi asubuhi. Ilikuwa takribani mita 600 (1970ft) kutoka kambi ya Walinzi wa Mapinduzi wa Iran,IRGC.
Habari za hivi punde, Saudi Arabia yadungua makombora mawili ya kulipua meli
Wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia imesema kuwa imezuia makombora mawili kusini mwa mji mkuu wake, Riyadh, mashirika ya habari ya Reuters na AFP yanaripoti.
Wakati huo huo Shirika rasmi la Habari la Saudia linaripoti kuwa ndege tisa zisizo na rubani zimeangushwa nchini humo.
Maafisa wa Saudia hawajasema makombora na ndege hizo zisizo na rubani zilirushwa kutoka wapi.
Uingereza na Uhispania zakataa ombi la Marekani kutumia kambi zake za kijeshi kuishambulia Iran
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Kambi ya kijeshi ya Uingereza iliopo katika visiwa vya Chagos
Uingereza imeripotiwa kukataa ombi la Rais wa Marekani Donald Trump la kutumia kambi za kijeshi za Uingereza, ikiwa ni pamoja na kambi ya Jeshi la Wanahewa la Diego Garcia katika Visiwa vya Chagos vinavyodhibitiwa na Uingereza katika Bahari ya Hindi, kwa ajili ya mashambulizi yanayoweza kutokea dhidi ya Iran.
Wakati huo huo serikali ya mrengo wa kushoto mjini Madrid Jumatatu ilisema kuwa imekanusha matumizi ya kambi zake za kijeshi kwa vikosi vya Marekani vilivyohusika katika shambulizi dhidi ya Iran, ikiwa ni pamoja na ndege kuu za kujaza mafuta ambazo ziliondoka Uhispania kuelekea nchi nyingine siku ya Jumapili.
Korea Kusini yasitisha biashara kwa muda baada ya bei ya hisa kuporomoka
Chanzo cha picha, Getty Images
Masoko ya hisa kote barani Asia yameathiriwa na mzozo unaoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran, lakini Korea Kusini ina ndio iliyoathiriwa vibaya zaidi.
Korea Kusini Ililazimika kusitisha biasha kwa dakika 20 Jumatano as baada ya hisa bei ya kushuka kwa zaidi ya 8% kutokana na kushuka thamani kwa sarafu yake ya Kospi.
Biashara imeanza tena lakini thamani ya Kospi iko chini zaidi ya 10%.
Kusitishwa kwa biashara ni sehemu ya utaratibu unaofahamika kama circuit breaker au kikatiza mzunguko wa mauzo, iliyoundwa ili kuzuia kuyumba kwa soko ikiwa bei za hisa zitashuka kwa kiasi kikubwa.
Hii ni mara ya kwanza hali hiyo imeshuhudiwa nchini tangu Agosti 2024.
Biashara itasitishwa tena ikiwa bei za hisa zitashuka kwa 15%.
Seoul ni muagizaji mkubwa wa mafuta ya Mashariki ya Kati na uchumi wake unaotegemea mauzo ya nje uko katika hatari kubwa yakuathiriwa na mzozo wa kikanda ambao unaweza kulemaza shughuki za usafirishaji.
Uingereza yakodi ndege kuwaondoa raia wake nchini Oman
Chanzo cha picha, Getty Images
Taarifa tulizopokea muda mfupi uliopita zinasema kuwa serikali ya Uingereza imekodisha ndege ya kibiashara kutoka Oman kuwasaidia raia wa Uingereza wanaotaka kuondoka Mashariki ya Kati.
Ndege inatarajiwa kuondoka mjini Muscat leotarehe 4 Machi saa tano usiku saa za ndani (19:00 GMT), na itawapa kipaumbele watu walio hatarini zaidi.
Raia wa Uingereza na wenzi wao na watoto wao walio chini ya umri wa miaka 18, wataruhusiwa kutumia ndege hiyo.
Ofisi ya Mambo ya Nje inasema raia wa Uingereza ambao wamejiandikisha kuwa wapo UAE na kwa sasa wako Oman wanapaswa kujaza fomu maalumu haraka iwezekanavyo, ikiwa wangependa kuabiri ndege hiyo.
Ofisi hiyo aidha imeomba watu kutofika uwanja wa ndege hadi watakapofahamishwa na Ofisi ya Mambo ya nje.
Inaongeza kuwa itaendelea kushirikiana na mashirika ya ndege kutafuta njia zaidi za kurejea watu nyumbani Uingereza.
Usafiri wa anga katika Mashariki ya Kati umetatizika sana tangu Jumamosi, wakati Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran na kumuua Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.
Iran tangu imelipiza kisasi kwa kufanya mashambulizi katika kanda nzima, yakilenga kambi za kijeshi vya Marekani zilizopo katika mataifa Kiarabu, lakini pia miundombinu ya kiraia na nishati.
Maelfu ya safari za ndege zimesitishwa, raia wengi wa Uingereza ambao wangependa kuondoka wamekwama katika eneo hilo.
Qatar yawakamata watu 10 wanaoshukiwa kuwa majasusi wa Iran
Shirika la habari la serikali ya Qatar linasema kuwa vikosi vya usalama vya Qatar " vilifanikiwa kukamata seli mbili" zinazofanya kazi katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mapema Jumatano.
Saba kati ya washukiwa hao "walipewa jukumu la kijasusi kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu miundombinu muhimu ya taifa na kijeshi," shirika la habari linasema.
Wengine watatu pia waliotumiwa kwa ujasusi "wana uzoefu wa kutumia ndege zisizo na rubani", inaongeza.
"Wakati wa uchunguzi, washukiwa walikiri uhusiano wao na Walinzi wa Mapinduzi ya Irani na kusema kwamba walikuwa wamepewa jukumu la kufanya ujasusi na uasi," shirika la habari la serikali linasema.
Israel yaanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran, IDF inasema
Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa limeanza wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran.
"IDF imeanza mashambulizi yanayolenga maeneo ya kufyatulia makombora ya utawala wa kigaidi wa Iran, mifumo ya ulinzi wa anga na miundombinu ya ziada," Jeshi la Ulinzi la Israeli liliandika kwenye mtandao wa wa kijamii wa Telegram.
Huku hayo yakijiri Jeshi la Marekani limewatambua wanajeshi wanne wa kwanza wa Kimarekani waliouawa katika mashambulizi ya Iran.
Wanajeshi hao wa Akiba wa Jeshi la Marekani, kutoka Kamandi ya 103 ya Ulinzi ya Des Moines, Iowa, ni pamajo na:
Kapteni Cody A. Khork, 35, wa Winter Haven, Florida
Sajenti Daraja la kwanza Noah L. Tietjens, 42, wa Bellevue, Nebraska
Sajenti wa Daraja la kwanza Nicole M. Amor, 39, wa White Bear Lake, Minnesota
Sajenti Declan J. Coady, 20, wa West Des Moines, Iowa
Wengine wawili waliuawa katika shambulizi la Iran dhidi ya kituo cha kijeshi huko Kuwait siku ya Jumapili, lakini bado hawajatambuliwa.
Siku ya Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kwamba ngome ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait ilipigwa wakati shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran.
Vifo hivyo sita pekee ndivyo vilivyothibitishwa na jeshi la Marekani tangu lilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa ushikiano na Israel.