Jeshi limejibu mashambulizi dhidi ya Iran: UAE
Wizara ya Ulinzi ya Umoja wa Falme za Kiarabu imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga inakabiliana na vitisho vya makombora na ndege zisizo na rubani vinavyotoka Iran.
Katika taarifa yake, wizara hiyo imeongeza kuwa sauti zilizosikika katika maeneo mbalimbali ya nchi zimetokana na mifumo ya ulinzi wa anga ikizuia makombora ya balistiki, pamoja na ndege za kivita zikizuia na kuangusha ndege zisizokuwa na rubani.
Hali hii inakuja muda mfupi baada ya UAE kusema kuwa imefanikiwa kuzuia makombora 6 ya Iran na mashambulizi 131 ya ndege zisizokuwa na rubani hadi sasa. Hata hivyo, kombora moja na ndege sita zimeripotiwa kutua ndani ya eneo la UAE.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Shirika la afya duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa shirika hilo limethibitisha mashambulizi 13 dhidi ya vituo vya afya nchini Iran na shambulizi moja nchini Lebanon tangu kuanza kwa vita.
Hata hivyo, hakutaja ni nani anayehusika na mashambulizi hayo wala kutoa maelezo ya ziada.
Siku ya Jumatatu, Fatemeh Mohammad Beigi, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya afya ya bunge la Iran, alisema kuwa hospitali tisa zimeshambuliwa nchini Iran, na akazishutumu Israel na Marekani kwa kuzilenga hospitali hizo.
Pia unaweza kusoma: