Tundu Lissu arejea tena Mahakamani Tanzania

Kesi ya uhaini dhidi ya Kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania inaendelea kusikilizwa jijini Dar es Salamaa.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu, Beldeen Waliaula na Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya leo. Kwaheri.

  2. Afrika Kusini kutumia wanajeshi kukabiliana na magenge ya wahalifu

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amesema atatuma wanajeshi kuwasaidia polisi kupambana na magenge yaliyojihami na uchimbaji haramu wa madini nchini humo.

    Magenge yaliyojihami yamekuwa tishio kubwa katika usalama wa Afrika kusini, taifa ambalo limerekodi idadi ya juu ya visa vya mauaji. "Magenge yaliyojihami kwa sasa wanatishia demokrasia yetu, jamii yetu na ukuaji wa Uchumi," Ramaphosa alisema katika hotuba yake kwa taifa siku ya Alhamisi.

    "Nitatuma jeshi la Afrika Kusini (SANDF) kuwasaidia polisi," aliongezea Ramaphosa.

    Mwezi uliopita, Waziri wa Usalama wa Ndani Firoz Cachalia, alisema polisi bado hawajafanikia kukabiliana na magenge yaliyojihami.

    Ramaphosa pia amewataka machifu, polisi na jeshi kubuni utaratibu utakaotoa mwongozo wa ni wapi vikosi vya usalama vinafaa kutumwa katika siku zijazo.

    Aliongezea kuwa wanajeshi hao wataanza na Wilaya ya Western Cape na Gauteng, ambayo yanapakana na miji ya Cape Town na Johannesburg.

    "Watoto katika eneo la Western Cape hujipata katikati ya makabiliano makali ya magenge hayo.

    Watu wanafukuzwa majumbani kwao na wachimbaji haramu wa madini eneo la Gauteng" Alisema Ramaphosa

    Rais huyo wa Afrika Kusini pia alitangaza kuwaajiri maafisa 5,500 zaidi wa polisi, ili kupambana na uhalifu uliokithiri pamoja na kuimarisha idara ya ujasusi.

  3. Habari za hivi punde, Lissu Mahakamani: Kesi yaahirishwa hadi Jumatatu

    .

    Kesi ya Kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu imeahirishwa hadi Jumatatu asubuhi saa tatu.

    Kesi hiyo imekuwa ikiendelea katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam kwa siku kadhaa wiki hii.

    Mashahidi wa upande wa Serikali leo wametoa ushahidi wao huku Mshatakiwa akipata furas ya kuwahoji.

    Shukrani kwa kutufuatilia kwenye Tovuti na mitandao yetu ya kijamii tangu tulipianza kukuljuza yote yanayojiri.

    Ungana nasi Jumatatu asubuhi kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu kesi ya Lissu kutoka Mahakamani.

  4. Habari za hivi punde, Wakili wa serikali sasa anauliza maswali ya dodoso kwa shahidi.

    Wakili wa serikali: Ieleze mahakama kwanini maeleze uliyotoa mahakamani na kwenye ushahidi wako ni tofauti ilhali ulimweleza mshitakiwa hakuna utofauti?

    Shahidi: Hayana utofauti bali hapa mahamani nimetoa ufafanuzi na maelezo ya ziada kulingana na maswali ya Jamuhuri

    Wakili wa serikali: Swali la mwisho mshitakiwa alipokua akikuuliza swali la mwisho alikuuliza anashitakiwa na kosa gani ulisema haujui hebu iambie mahakama

    Shahidi: Mheshimiwa ninaelewa anakabikiwa na kesi ya uhaini kutokana na kauli aliyoitoa ya kutaka kuzuai uchaguzi

    Jaji: Shahidi tunakushukuru Mahakama inakushukuru umemaliza kutoa ushahidi wako.

  5. 'Nataka ujibu kiaskari': Lissu aendelea kumhoji shahidi wa serikali

    Lissu

    Lissu: Swali langu la pili umesema ulijiunga na jeshi mwaka 2012 na ukafuzu mwaka 2013 waleze majaji kama yapo shahidi Sikuyaandika hayo

    Lissu: Sema kwa sauti kaka

    Shahidi: Nimesema kwa sauti sikuyaandika hayo

    Lissu: Kwa ushahdi wako umesema ulipata mafunzo kwenye shule ya upolisi iliyoko Moshi

    Shahidi: Hakuna

    Lissu: Nataka ujibu kiasakari ...Sasa shahidi twende kwenye yaliyotokea tarehe 8 april 2025 umesema baada ya kumkamata huyu kijana umesema RCO alikuelekeza ufungue faili la uchunguzi. Nataka kujua RCO alisema muandike maelezo na awekwe mahabusu mpaka mtakapopata maelekezo mengine?

    Shahidi: Waheshimiwa maelezo hayo yapo ila nimeifafanulia mahakama ila hilo la akae mahabusu mpaka maelekezo mengine sikuliandika

    Lissu: Umeeleza kwamba huyu mtuhumiwa aliwekwa rumande na baadae akaachiwa kwa masharti ya kuripoti kila jumatatu?

    Shahidi: kwenye maelezo yangu hakuna

    Lissu: Asante kwenye maelezo yako hakuna, sasa shahidi nikulete kwenye kilichotokea RCO alipokuelekeza umtafute huyo kijana tarehe 22 na umuandikishe maelezo upya ya shahidi

    Shahidi: Waheshimiwa hilo lipo ila kuna mengine hayapo

    Lissu: Kipi kilichohamasisha vijana wenzake kufanya vurugu yapo hayapo?

    Lissu: Haya maneno alisema alikuwa anaunga mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Tundu Lissu

    Shahidi: Mheshimiwa Jaji haya mengine sikuyaeleza hapa

    Lissu: Na umesema kwamba huyu kijana alikuambia kwamba wamedhamiria kufanya uasi dhidi ya serikali ya CCM

    Shahidi: Mheshimiwa kwenye hii aya hakuna

    Lissu: Pia umesema kwamba huyu kijana alikuambia kuwa watakinukisha hayo maelezo yapo?

    Shahdi: Hayapo yako huku mwanzo

    Lissu: unasema kwamba huyu P8 alikuambia kwamba watakinukisha mpaka serikali itakapofanya mabadiliko ya uchaguzi na katiba mpya yapo hayapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: Sasa shahidi naomba uwaeleze majaji kama umeeleza sababu ya maelezo yako polisi na ushahidi wako kutofautiana kiasi hiki

    Shahidi: Mheshimiwa sijaeleza sababu, sababu hakuna utofauti

    Lissu: Ahsante bwana Koplo Lissu: umeeleza kwamba ulimkamata huyu PA ndipo RCO akakuambia fungua faili

    Shahidi: tulimkamata baada ya kupata taarifa ndipo tukafungua faili

    Lissu: Naam ndio ninachouliza mnakamata ndipo mnaenda kuchunguza na kumpa kesi

    Lissu: Mtu anayepanga kufanya Vurugu anafanya kosa la Jinai kweli si kweli

    Shahidi: kweli

  6. Tundu Lissu Mahakamani: Shahidi ahojiwa na mshtakiwa

    .

    Mshatakiwa ameanza kuwauliza maswali shahidi wa upande wa serikali Koplo Michael.

    Jaji amemuuliza mshitakiwa kama ana maswali ya Dodoso.

    Lissu akamjibu mengi na kuendelea kusema; Nyie wenye watoto mkipeleka watoto polisi wanaenda kupata dhambi za uongo.

    Lissu: Shahidi detective Michael naomba nikuhoji kama uliandika maelezo yako ya ushahidi.

    Lissu: Naomba Uwaeleze Majaji iwapo utayatambua

    Shahidi: Ndio nitayatambua

    Lissu: Mheshimiwa Jaji naomba shahdi apewe maelezo yake.

    Shahidi: Nimeyaoana maelezo haya ya tarehe 24/4/2025 na nimeyatambua yana sahihi yangu

    Lissu: Waheshimiwa naomba nimuulize maswali machache kufahamu ukweli wa shahidi huyu ...Lissu ana msomea shahdi maelezo yake yote Kisha anamuomba shahidi kama melezo yake yapolewe kama kielelezo

    Shahidi anasema kwa kuwa maelezo ni yake na upande wa Jamuhuri utarudhia basi yuko tayari yapokelewe na upande wa mashitaka

    Wakili wa serikali: Ni sawa hakuna pingamizi

    Jaji; Maelezo hayo yamepokelewa na yatatambulika kama kielelezo D5

    Lissu: Asante waheshimiwa, naomba shahdi apewe kilelezo D5 Umeileza mahakama kwamba wewe ni askari polisi ofisi ya RCO Kilimanjaro tangu 2015 naomba waeleze majaji kuwa hayo maneno kama yapo

    Shahidi: yapo ila mwaka ndio hakuna.

  7. Lissu Mahakamani: Mashahidi wa serikali watoa ushahidi

    Kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu inaendelea katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam baada ya kuahirisha hapo awali.

    Shahidi wa upande wa serikali Koplo Michael, Mkuu wa Upelelezi MkoaNI Kilimanjaro amekula kiapo na kuielezea Mahakama kilichotokea mwezi wa nne 2025.

    Wakili wa Serikali - Tarehe mwezi wa nne 2025 unakumbuka nini

    Shahidi: nilikuwa doria na askari wenzangu ambapo tulikuwa tunazunguka maeneo mbali mbali ya Moshi mjini yani wilaya ya Moshi Mjini.

    Wakili wa serikali: Mlikuwa na lengo gani

    Shahidi: Lengo ilikuwa kudhibiti uhalifu na kuwalinda raia na mali zao - [ ] Nakumbuka siku hiyo nilipofika maeneo ya Njoro iliyopo Moshi tulipata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kijana mmoja anahamasisha wenzake kuhusiana na kufanya vurugu katika uchaguzi mkuu ujao uliokua unakaribia kufanyika mwaka 2025

    Wakili wa serikali: Bada ya kupata hizo taarifa mlichukua hatua gani

    Shahidi: Baada ya kuoata hizo taarifa tuliende eneo la alipokuepo huyo kijana kama tulivyopewa taarifa na kumkamata huyo kijana

    Wakali: Nini kilifuata

    Shahidi: Tulimpeleka mpaka ofisi ya RCO Mkoa wa Kilimanjaro

    Wakili: Nini kilifuata

    Shahidi: Tulimfahamisha Mkuu wa Upelelezi ACP Abichi Malanga na kunielekeza nifungue jalada la uchunguzi

    Wakili: Na wewe ukafanya vipi

    Shahidi: Nilifungua Jalada kesi nambari ar/cid/ee/18/2025

    Wakili: Nini kilifuata baada ya kufungua jalada

    Shahidi: Afande RCO alisema kijana huyo ahojiwe na alihojiwa na detective Koplo Rashid

    Wakili: Nini kikafuata

    Shahidi: Pia alitoa maelekezo awekwe mahabusu na kuongeza kuwa atatoa maelekezo ya nini kitakachofuata baadae.

    Wakili: Nini kilifuata

    Shahidi: Kijana huyu alitolewa kwa masharTi baada ya kukaa mahabusu kuwa angekuwa anakuja kuripoti polisi

    Wakili wa serikali: Nini kilifuata

    Shahidi: Ilipofuka tarehe 22/04/2025 afande RCO alinipa maelekezo ni mtafute yule kijana ambaye anakuja kuripoti na nimuandikie maelezo upya.

    Wakili: Maelezo ya aina gani

    Shahidi: Maelezo ya shahdi aeleze ni kitu gani kilichopelekea yeye kuhamasisha vijana wenzake kufanya vurugu katika uchaguzi mkuu uliokuwa unatarajiwa 2025.

    Wakili: Wewe ulifanya nini

    Shahidi: Nilienda kwenye kumbukumbu na kuchukua mawasiliano yake na bahati nzuri siku hiyo alikuwa amepangiwa kuripoti

    Wakili: Nini kiliendelea

    Shahidi: Nilitoa maelekezo kwa askari wanaohusika na kuwahudumia hao wanaokuja kuripoti kuwa akifika awasiliane na mimi .Alipofika niliandika maelezo yake kwenye karatasi ya maelezo ya shahidi

    Wakili:alikueleza nini kwa ufupi

    Shahidi: Alinieleza yeye ni mwanachama wa chama cha Chadema na amelikuwa mwanachama tangu akiwa sekondari

    Mashahidi upande wa serikali wamemaliza kutoa ushahdi wao na kinachofuata ni maswali ya upande wa mshatakiwa.

  8. AU yapinga kuundwa kwa serikali mbadala Sudan

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Baraza la usalama na amani la Umoja wa Afrika, limepinga vikali kuundwa kwa '‘serikali mbadala’' nchini Sudan.

    Baraza hilo linaonya kuwa hatua hiyo itakandamiza uhuru, umoja na kuheshimu kwa mipaka ya taifa hilo.

    Taarifa iliyotolewa na kundi la Sudan Founding Alliance, muungano unaohusishwa na kundi la wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF), ambao walitangaza kuunda serikali mbadala nchini Sudan.

    Umoja wa Afrika umetaka mataifa wanachama na jamii ya kimataifa, kutoitambua wala kutoiunga mkono serikali hiyo ya RSF.

    Muungano huo ambao unajiita Leadership Council of the Sudan Founding Alliance (TASIS), unaongozwa na kiongozi wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti.

    RSF awali ilikuwa imetangaza mipango yake ya kuunda serikali itakayoiongoza eneo la magharibi mwa Sudan, ikiwemo kuwateua viongozi na mawaziri.

    Mwezi Agosti 2025, baraza la usalama la umoja wa mataifa ilipinga tangazo la RSF la kuunda serikali mbadala na kusema hatua hiyo itadhoofisha zaidi mgogoro wa kibinadamu unaoshuhudiwa nchini humo.

    Vita wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vilianza mwezi Aprili mwaka wa 2023, baada ya mvutano wa madaraka kati ya kikosi cha RSF na jeshi la Sudan (SAF).

    Maelezo zaidi:

  9. Tarique Rahman kutangazwa Waziri Mkuu mpya wa Bangladesh

    .

    Chanzo cha picha, NurPhoto via Getty Images

    Chama cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) kinaongoza katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo, huku kiongozi wa chama hicho Tarique Rahman, akitarajiwa kutangazwa kama Waziri Mkuu wa taifa hilo.

    Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika baada ya maandamano makubwa kushuhudiwa nchini humo mwaka wa 2024, na kumuondoa madarakani aliyekuwa Waziri mkuu Sheikh Hasina.

    Mpinzani mkuu wa chama cha BNP ni Jamaat-e-Islami ambacho kimetilia shauku matokeo ya uchaguzi huo.

    Chama cha BNP kinaongoza kwa kuchukua viti zaidi ya theluthi mbili vya bunge. Kiongozi wa sasa Muhammad Yunus, ambaye anatarajiwa kujiuzulu baada ya serikali mpya kuchukua madaraka amewataka raia wa taifa hilo kudumisha amani.

    Soma pia:

  10. Katika taarifa zingine Rubio asema: Tunaishi katika 'enzi mpya' ya siasa za kijiografia

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, anasema ni ulimewengu uko katika ''enzi mpya’'

    Amesema hayo katika ziara yake ya Ulaya huku akitarajiwa kutoa hotuba katika kongamano la usalama mjini Munich.

    Hii ni ziara ya kwanza ya wajumbe wa Marekani kuhudhuria kongamano la kimataifa barani Ulaya, baada ya Rais Trump kutishia kuliichukua eneo la Greenland.

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesisitiza kuwa lazima Ulaya ijikomboe kutoka kwa Marekani, huku Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya Nato, Mark Rutte, akisema uhusiano wa mataifa ya transatlantic bado uko imara.

    Vita vya Ukraine, wasiwasi ulioko China, na mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani inatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo wa Munich "Dunia inabadilika kwa kasi sana," Rubio aliwaambia wanahabari.

    Alipoulizwa iwapo ujumbe wake kwa ulaya utakuwa wa utangamano alijibu kuwa; "Tunaishi katika enzi mpya ya siasa za kijiografia, na itatulazimu tutathmini jinsi hali ilivyo na wajibu wetu utakuwa upi".

    Katika kongamano la mwaka uliopita, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance, aliishambulia Ulaya, ikiwemo Uingereza kuhusu sera zao za uhuru wa kujieleza na uhamiaji.

  11. Lissu Mahakamani: Kesi yaahirishwa hadi saa nane

  12. Lissu amaliza kumhoji shahidi

    Lissu: Naweza ondoa hili swali, maandamu wanasema wana mlinda shahidi lakini kielezo D4 kina taarifa zote za shahidi mpaka jina, umri makazi na dini licha ya mahakama kueleza shahidi alindwe.

    Jaji: Kama umeridhia kuendelea bila kutolea uamuzi ni sawa tuendelee.

    Lissu: Shahidi, umesema wewe ni mwanachama wa Chadema kwenye kilele D4 polisi ulisema wewe ni mwanachama wa chadema

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Waeleze majaji tangu ulipoandika maelezo hayo umewahi kwenda polisi kuandika maelezo mengine au kupelekea taarifa nyingine yoyote polisi kuhusiana na kesi hii?

    Shahidi; Hapana

    Lissu: Waleze maajaji kama umetoa tarifa polisi kama kuna mtu yeyote anakutishia maisha baada ya tarehe 25/04/2025 kama kuna kiongozi au mfuasi wa Chadema aliyekutishia maisha

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Waleze majaji kama kuna mtu yeyote Chadema aliyekutishia sababu ya kutoa maelezo haya polisi.

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Waeleze majaji kama kuna mtu ametishia kuwadhuru ndugu zako baada ya kutoa maelezo haya polisi

    Shahidi: Hapana

    Lissu: Sina maswali mengine Mheshimiwa.

    Upande wa mashitaka unaomba ahirisho la saa moja waandae mashahidi ikiwa ikiwa ni pamoja na maswala mengine ya kibinadamu.

  13. Lissu anaendelea kumuliza shahidi kwa maswali

    Lissu: Naomba ni kuulize maswali mengine baada ya kukupitisha maelezo yako ya polisi. Waeleze majaji kama kiongozi wa chama kama mimi kuita mkutano na kusema tutazuia uchaguzi kama hakuna mabadiliko ni kosa la jinai

    Shahidi; Sifahamu

    Lissu: Waleze Majaji kama kuna sheria inayokataza kusema tutazuia uchaguzi

    Shahidi: Sifahamu

    Lissu: Waeleze majaji kwamba kutaka kuzuaidi uchaguzi si kosa la jinai

    Shahdi: Sifahamu

    Lissu: Waeleze majaji kama ni halali au si halili kwa chama kama Chadema kufanya mkutano wa hadhara popote nchini

    Shahidi: Hilo sifahamu. Waeleze majaji kama una fahamu

    Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kukataza kutoa vibali vya maandamano au mikutano hawana vibali.

    Shahdi Sifahamu

    Lissu: Waleze majaji kama unafahamu mikutano iliyozuiliwa ilikuwa imetolewa taarifa siku mbili kabla ya mkutano

    Shahidi: Sifahamu

    Lissu: Wewe si umesema ulihamasika na Chadema wewe?

    Shahidi: Hilo mimi sifahamu

    Lissu: Kuvaa fulana iliyoandikwa maandishi no reforms no election kwenye matembezi ni kosa sio kosa?

    Shahidi embu tuzungumze kidogo juu ya kukamatwa kwako umesema tarehe 20/04/2025 mkiwa eneo mlilopanga kuanzia matembezi mlikamatwa kweli sio kweli:

    Shahdi: Kweli

    Lissu: Waliwakamata sababu mlikuwa mnapanga kufanya maandamano bila ya kibali Lissu na waliwapeleka polisi na kutoa melezo shahidi kweli

    Lissu: Hayo melezo yako wapi

    Shahidi: Mimi sifahamu

    Lissu: Hizo tuhuma za kupanga maandamano bila kibali hiyo kesi iliishia wapi ulipelekwa mahakamani?

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Kesi namba ngapi

    Shahidi Kesi ilikua inasinamiwa na kaka yangu kwa hiyo sifahamu

    Lissu: Kwa hiyo ulishitakiwa

    Shahidi: Mimi sifahamu sababu kesi alikuwa anasimamiwa kaka yangu

    Lissu; Ndugu yako ni wakili

    Shahidi: Mimi sifahamu

    Lissu: Waeleze majaji ilikuwaje kesi yako ya kupanga njama ikapotea na sasa ni shahidi kwenye kesi ya uhaini ya unayemuita mwenyekiti wako

    Shahidi: Mimi sifahamu Lissu sasa shahidi

    Shahidi: Ndio

    Mheshimiwa Lissu: Wewe ni mwanachama wa Chadema

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Waeleze majaji umejiunga na chama lini -

    [ ] Wakili wa serikali huyu ni shahIdi anayelindwa kupata hizo taarifa kutarahisisha kumtambua shahidi

    Kimya kidogo

  14. Tundu Lissu anaendelea kuuliza maswali kwa shahidi P6

    Lissu: Ulikuwa na bando la internet hayo maneno yapo hayapo

    Shahidi: Hayapo

    Lissu: shahidi kwenye ushahidi wako uneeleza kwa kutumia simu yako uliingia kwenye mtandao wa jambo TV

    Shahidi: hapana nimeeleza niliingia kwenye akaunti ya jambo TV Lissu: ahsante kwemye maelezo yapo hayapo Shahidi: Hayapo

    Lissu: kwenye ushahidi wako umeeleza kwamba kwenye hiyo video uliona nikisema kuwa anayetaka kwenda nasi tutaenda naye na asiyetaka tutamuacha

    Shahidi: Ndio

    Lissu: waeleze majaji kama kwenye maelezo yako ya polisi yapo hayo

    Shahidi: hayapo Lissu: umesema nilitoa kauli ifuatayo kama kuna anayetaka kugombea udiwani asahau ubunge asahau na mimi uraisi nimeusahau

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Je kwenye maelezo yako ya polisi Shahidi: yapo nilisema polisi ila hapa hayapo

    Lissu: Je, kuna mahali popote umeandika kwenye maelezo ya polisi ulikuwa na simu?

    Shahidi: hilo swali ushauliza nikakujibu Lissu: Hapana sijakuuliza Shahidi: ndio kuna mahali nimesema nilikuata na mwenyekiti akaniunga kwenye kundi la watsap hiyo inaonesha nilikuwa na simu

    Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema nilikuwa nimevaa kombati za kaki waeleze majaji kama kwenye maelezo yako yapo shahidi: sijaona

    Lissu: Naomba ni kuulize kidogo kuhusu huyu Esau chiza umemtambulisha kama katibu na kwingine kama mwenye kiti tushike lipi shahidi: 2024 alikuwa katibu 2025 alikuwa mwenyekiti

    Lissu: Kwenye maelezo yako 2025 unasema ulimfata katibu je hapo tushike lipi Shahidi: Polisi labda walikosea kuandika Lissu: umesema maneno yangu yalikuhamasisha waeleze majaji kama maneno ya kukinukisha na kufanya vurugu kama yako kwemye maelezo yako polisi

    Shahidi: Yapo Lissu: Twende tarehe sita kuwa tarehe sita Lissu atazuru songea na ulipata taarifa toka kwa Esau Chiza waeleze majaji kama yapo kwenye kieleezo polisi

    Shahidi: Yapo Nilipata taarifa kuwa mwenyekiti wa chadema taifa…..anasita hapaonekani vizuri

    Lissu: leta nikusomee Imeandikwa nilipigiwa simu na Esau Chiza na akanieleza kuwa kuna ziara ya mwenyekiti wilaya ya Songea

    Lissu: Je kuna maneno Tundu Lissu?

    Shahidi anarudi kusoma na kusema …. kuwa ataongozana na viongozi.

    Lissu: shahidi twende siku ya tarehe 10 umesema hivi kwemye ushahidi wako mkiwa na wenzako mkiwa mmekusanyika na wenzako kwenye viwanja vya shule ya msingi makarawe gari ya polisi ikaja na kuwatawanya Je yapo kwenye maelezo yako?

    Shahidi: hayo maelezo tulitawanywa hayapo Lissu: Umesema baada ya kutawanywa mlipofika ofisi za chama mfaranyaki polisi walifika na kuwapiga mabomu je hayo maneno mlipigwa mabomu yapo

    Shahidi: Tulitawanywa …… Lissu: mlipigwa maboumu kaka Shahidi kimya.. shahidi: mimi ni binadamu siezi kumbuka kila kitu

    Lissu: yapo hayao Shahidi: hayapo

  15. Tundu Lissu amkosoa shahidi

    Lissu anamaliza kusoma, Hayo ndio maelezo uliyoandika polisi ?

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Kuna maeneo kadhaa nataka kukukanusha eneo la kwanza dini yako la pili umri wako la tatu ni kwenye shughuli za chama uliambiwa utakua unaongoza shughuli za chama kwa bendera?

    Eneo la nne ulisema ulipokua kazini ulikuwa na simu ya infinix kwenye maelezo ya polisi haipo

    Eneo la tano ni ushahidi wako kuwa ulikuwa na bando kwenye maelezo ya polisi haipo

    Eneo la sita ni kuwa ulingia mtandao wa Youtube kwenye maelezo ya polisi haipo

    Eneo la saba ni ushahdi wako kuwa mimi mtuhumiwa nilisema anayetaka kwenda nasi tutaenda naye na asiyetaka tutamuacha

    Eneo la nane nilisema kuwa hata mimi ninayetaka kutaka kugombea urais nisahau kwenye maelezo ya polisi haipo

    Eneo la tisa kwamba nilisema maneno 'no reforms no election' sijayaona kwenye maelezo yako

    Eneo la kumi kwenye ushahidi wako ni maneno kuwa nilisema watasema tunafanya uasi nioneshe yako wapi kwemye maelezi yako

  16. Tundu Lissu: 'Mheshimiwa nataka kuonesha kuwa shahidi ni muongo na hapaswi kuaminika'

    Jaji - Maswali ya Dodoso

    Lissu: Shahidi unanisikia?

    Shahidi: Nakusikia mheshimiwa

    Lissu: Naomba ujibu maswali sawa sawa na nitakavyokuuliza sawa

    Shahidi: Nimeelewa

    Lissu: Naomba uwaambie majaji kama uliandika maelezo polisi? Ndio au hapana

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Ukioneshwa hayo maelezo yako utayatambua

    Shahid: Kimya…kisha ndio ninaweza kuyatambua

    Lissu: Uliyasaini?

    Shahidi: Sikumbuki

    Lissu: Mheshimiwa jaji naomba shahidi aoneshwe maelezo yake

    Kimya kwa muda mahakamani wakati shahidi alikipelekewa maelezo yake

    Lissu: Umepata maelezo yako shahidi?

    Shahidi: Ndio nimepata

    Lissu: Waeleze kama ndio maelezo uliyoandika polisi Songea

    Shahidi: Ndio

    Lissu: Waeleze kama yana sahihi yako

    Shahidi: Ndio ipo Lissu: Waeleze majaji kama ni ya tarehe 25/04/2025

    Shahidi: Sioni

    Lissu: Angalia juu ya karatasi maneno yanayosomeka maelezo yametolewa tarehe 25 mwezi wa nne 2025

    Shahidi: Sioni

    Lissu: Mheshimiwa nataka kuonesha kuwa shahidi ni muongo na hapaswi kuaminika Waheshimiwa majaji ninaomba nimsomee maelezo yake sawa shahidi

    Shahidi: Sawa!

    Tundu Lissu anasoma maelezo yote ya shahidi

  17. Shahidi: 'Nilikuwa nimevalia T-shirt yangu ya 'No Reform No Election'

    Wakili: Pia nini kilifuata?

    Shahidi: Ulifanyika utaratibu kupata tisheti hizo toka Dar es salaam hadi kutufikia Wakili: baada ya hapo nini kiliendelea?

    Shahidi: Baada ya utaratibu huo tuambizana tutakutana tarehe 20 kwa matembi hayo ya hiari Wakili: Baada ya kufika tarehe 20 nini kilifuata?

    Shahidi: Tulikusanyika

    Wakili: Kabla ya matembezi majira ya asubuhi siku hiyo unakumbuka nini Shahidi: nakumbuka tulivaa tisheti tulizoagiza kutoka Dar

    Wakili: baada ya kupata T shirt

    Shahidi: Tulikubaliana matembezi itakuwa jioni kwa ajili ya matembezi

    Wakili: Na hiyo taarifa uliipata wapi?

    Shahidi: Kwenye group

    Wakili: Sasa mlikubaliana mkutane wapi?

    Shahidi: Sehemu moja songea panaitwa kwa Dis kitimoto

    Wakili: Sasa baada ya kukutana jioni hiyo nini kilitokea?

    Shahidi: Ghafla ilikuja gari ya polisi

    Wakili: Twende taratibu wewe wakati unaenda kwa dis ulikuwa kwenye muonekano upi? Shahidi: Nilikuwa nimevaa tshirt yangu ya No reforms no election

    Wakili: Baada ya kukutana kwa Dis Nini kilitokea?

    Shahidi: Walikuja Polisi na kujitambulisha wanatoka kituo cha polisi songea na kutuambia tunatakiwa kituoni

    Wakili: Nini kikafuata?

    Shahidi: Walitukamata hadi kituo cha polisi Songea

    Wakili: Mlipofika kituoni nini kiliendelea?

    Shahidi: Nakumbuka tuliambiwa tunatuhumiwa kupanga maandamano bila ya kibali

    Wakili: Baada ya kupewa tuhuma hizo nini kiliendelea?

    Shahidi: Walituambia tutatoka kwa dhamana na tungetakuwa kurejea kituoni kwa RCO RUVUMA tarehe 25/04/2025

    Wakili: 25:04/2025 nini kilitokea? Shahidi: 25/04/2025 Baada ya kuripoti kwa RCO alitaka tuelezee ilikuaje hadi kufika sehemu hiyo. Wakili: Mheshimiwa Jaji kwa shahidi huyu ni hayo

    Shahidi P6 amemaliza kutoa ushahidi, hatua inayofuata ni mshtakiwa Tundu Lissu kuumuuliza shahidi P6 maswali ya dodoso

  18. Kesi ya Lissu: 'Nilipata taarifa kwamba Mwenyekiti amekamatwa Wilaya ya Mbinga

    Wakili: Sasa tuambie unakumbuka nini tarehe 6 april 2025 Shahidi nakumbuka nilipata taarifa mwenyekiti atakuwa na ziara mkoani ruvuma Wakali taratibu mwenyekiti ni nani

    Shahidi: Mwenyekiti ni Tundu Lissu

    Wakili: Hiyo taarifa ulipata wapi

    Shahidi: Niliipata kwa ndugu Chiza

    Wakili :Hiyo taarifa ilikutaka ufanye nini

    Shahidi Ilinitaka tufanye maandalizi ya kumpokea mwenyekiti

    Wakili: Nini kikafuata

    Shahidi :Tulianza maandalizi na ikaeleza tarehe 10:4/2025 atakuepo Songea

    Wakili :Walipanga aatakuepo wapi Songea

    Shahidi: Walipanga atakuepo uwanja wa shule ya msingi Matawalo Songea

    Wakili: Sasa Tarehe 9 mwezi wa nne 2025 wewe unakumbuka nini

    Shihidi: Ninakumbuka nilipata taarifa kuwa mwenyekiti amekamatwa huko wilaya ya mbinga kwenye ziara Baada ya kupata taarifa nini kilitokea

    Shahidi: Niliwasiliana na chiza na kumuaambia nimesikia mwenyekiti amekamatwa mbinga akanithibitishia akaniambia lakini ratiba ya mkutano wa tarehe 10/04/2025 iko pale pale jiandae ili tuwepo eneo la mkutano

    Wakili :Tarehe kumi sasa mwezi wa nne 2025 nini kilitokea

    Shahidi: Nakumbuka tulikusanyika uwanja wa shule ya msingi matabawe kuwasubiri viongozi waliongozwna na mwenyekiti weweze kuhutua mkutano

    Wakili: Viongozi hao ni wa wapi Godbless Lema dokta slaaaa Na mwingine nani Nakumbuka pia alikuepo pia makamu mwenyekiti Heche

    Wakili :nini kiliendelea

    Shahidi :Nakumbuka ilikuja gari ya polisi na kututawanyisha na kwamba hakuna mkutano unaofanyika hapo na hakuna mtu anaruhusiwa kuwa eneo hilo

    Wakili: Sasa baada ya kupewa katazo la polisi nini kilitokea

    Shahidi: Tulielekea ofisi za chama kujua nini kifanyike kwa siku hiyo

    Wakili: Hizo ofisi ziko wap

    Shahidi: Ziko Songea

    Wakili Songea wapi

    Shahidi :Songea Mfaranyaki

    Wakili :Baada ya kufika ofisini mfaranyaki nini kiliendelea

    Shahidi: Nakumbuka niliwaona waandishi wa habari wakijiandaa kuongea na viongozi katika ofisi hizo Ni viongozi gani unakumbuka uliwakuta ofisini hapo

    Shahidi: Namkumbuka kiongozi ndugu Abel Mayala ambaye wakati huo alikuwa mwenyekiti chadema kanda ya kusini

    Wakili: vVongozi wengine unaowakumbuka Shahidi hapana ni huyo tu

    Wakili: Baada ya hapo nini kiliendelea

    Shahidi: Polisi wakukuja na kupiga mabomu na kututawanyisha

    Wakili :Siku hiyo majira ya saa saba siku hiyo hiyo nini kiliendelea

    Shahidi :Tuelekea uwanja wa shule ya msingi matabawe alikuja makamu mwenyekiti na kusema amepokea barua ya polisi kuwa kusifanye mkutano katika eneo hilo siku hiyo

    Wakili :Akasemaje tena

    Shahidi :Pia akasema tutawanyike eneo hilo viongozi watapanga siku ingine

    Wakili: Umetuambia makamu mwenyekiti huyo makamo ni nani

    Shahidi: huyo makamo ni mheshimiwa Heche

    Wakili: Shahidi unakumbuka nini tareh 18/04/2025

    Shahidi: Nakumbuka nilipokea taarifa kuwa tarehe 20/04/2025 ambapo ilikuwa siku ya pasaka kuwa kutakuwa na matembezi ya hiari ambapo kwenye matembezi hayo yataambatana na kuvaa tsheti zilizo andikwa no reforms no election ili kusisitiza msimamo wa chama

  19. Kesi ya Tundu Lissu: Shahidi P6 aendelea na ushahidi

    Shahidi wa siri wa Jamuhuri P6 anaendelea kutoa ushahidi

    Wakili: Eleza mahakama ulipokuwa kwenye mtandao wa youtube ulikuwa unafanya nini Shahidi: Kwenye Youtube niliingia kwenye akaunti ya jambo TV

    Wakili: Baada ya kuingia Jambo TV?

    Shahidi: Nilifanikiwa kuona video ya hotuba ya mwenyekiti wa chama cha Chadema akiwa anahutubia watu kwamba bila ya mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo 'tunaenda kukinukisha tunakwenda kuvuruga uchaguzi', pia nilisikia na kuona akisema 'tunakwenda kukinukisha na yeyote ambaye atakuwa pamoja nasi tutaenda naye ambaye hatotaka tutamuacha' pia alisema 'kama kuna mtu yeyote anatarajia kugombea udiwani asahau' pia alisema 'yeyote anayetarajia kugombea ubunge pia asahau' akaendelea kusema 'hata mimi mwenyekiti kuhusu kugombea urais hilo sahau' pia akasema 'bila ya mabadiliko hakuna uchaguzi'

    Wakili: Kingine kipi alisema? pia akasema 'watasema tunafanya uasi, ni kweli ni uasi bila ya mabadiliko hakuna uchaguzi'

    Wakili: Alikuwa anazungumza kwenye mazingira gani?

    Shahidi: Ilikuwa ukumbini sehemu aliposimama nyuma kulikuwa na bendera ya taifa na bendera ya Chadema pembeni

    Wakili: Lissu alikuwa kwenye muonekano gani siku hiyo

    Shahidi: Alikuwa amevaa kombati ya kaki

    Wakili: Huyo Tundu Lissu wewe unamfahamu vipi?

    Shahidi: Namfahamu kama mwanasiasa mkongwe na maarufu

    Wakili: Baada ya kuona na kusikia hiyo video nini kilifuata?

    Shahidi: Maneno yake yaliniingia na kunishawishi kuwa miongoni mwa wale watakaounga mkono ajenda ya kuzuia uchaguzi pasipo na mabadili

    Wakili: Kuzuia vipi uchaguzi

    Shahidi: kuzia uchaguzi kwa maana ya kukinukisha

    Wakili: Na hiyo ajenda ambayo unasema ulishawishika ni ipi?

    Shahidi: Ajenda ya kukunukisha ni kwamba kufanya vurugu au kuharibu uchaguzi

    Wakili: Shahidi umezungumza kuhusu uchaguzi huo uchaguzi ni upi?

    Shahidi: Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambao unahusisha madiwani wabunge na Rais

    Wakili: Baada ya kushawishika na hotuba ya mwenyekiti wewe ulichukuwa hatua gani

    Shahidi: Niliamua kumfuata mwenyekiti wa vijana ambaye ni maarufu kama mwamba wa kigoma nikamweleza nia yangu na namna nilivyoshawishika na maneno ya mwenyekiti na kutamani kuwa miongoni mwa watu tutakao kinukisha kutafuta mabadiliko kabla ya uchaguzi Wakili: Baada ya kumuambia nia yako hiyo nini kiliendelea?

    Shahidi: Alinisifia na kunipongeza kwa huo ushujaa

    Wakili: Nini kiliendelea

    Shahidi: Alinipongeza akaniambia vijana kama ninyi ndio mnatakiwa kulikombia taifa

    Wakili: Nini kilifuata

    Shahidi: Aliniambia kitakachofuata kuhusu harakati hizo za kukinukisha atanishirikisha na pia aliniahidi ataniunganisha na makundi mbalimbali yanayojadili mipango ya kudai mabadiliko kabla ya uchaguzi

    Wakili: Group lipi ambalo uliwekwa

    Shahidi: Nakumbuka ni kundi la siasa yetu update

    Wakili: Baada ya hapo nini sasa kilifuata

    Shahidi: Nilendelea na shughuli zangu na yeye akaendelea na shughuli zake

  20. Kesi ya Tundu Lissu: Yaliojiri hapo Jana kwa ufupi

    .

    Iwapo unajiunga nasi kwa mara ya kwanza, hapo jana siku ya Alhamisi kesi iliahirishwa baada ya mshitakiwa kusema hajala

    Wafuasi wake waliokuwa mahakamani waliangua kilio baada ya kusikia kauli hiyo.

    Awali shahidi wa kwanza alisema kwamba 'alliona video ya Lissu akisema atakinukisha na uchaguzi mkuu hautafanyika' - Shahidi

    Vilevile aliongezea kwamba 'aliihofia video hiyo ingesababisha uvunjifu wa amani, kukwamisha biashara na kusababishia njaa'.

    Hatahivyo akimjibu Tundu Lissu alisema Nukisha inatokana na neno nuka na kwamba inaweza kuwa harufu nzuri au harufu mbaya

    Tundu Lissu ambaye anajiwakilisha katika kesi hiyo alimuuliza shahidi huyo kuhusu video aliyokuwa akiitazama Facebook ilikuwa kwenye akaunti ya nani wakati alipokua anaiperuzi….

    Shahidi alimjibu akisema hakufahamu kupitia account gani

    Mashahidi 5 kati ya 30 wanatoa ushahidi katika kesi ya Tundu Lissu leo ambapo anashtakiwa kwa makosa ya uhaini.

    Uhaini ni kesi ambayo ukipatikana na hatia hukumu yake inaweza kuhusisha kunyongwa hadi kufa

    Lissu alikamatwa April mwaka jana mkoani Iringa kwenye shughuli za chama akituhumiwa kwa kesi ya mbili za uhaini na kesi nyingine ya uchochezi.

Trending Now