Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Bayern yakataa ofa ya Liverpool ya £170m kwa Olise
Bayern Munich wamepuuza madai kwamba mshambuliaji wa Ufaransa Michael Olise, mwenye umri wa miaka 24, ataondoka na kujiunga na Liverpool, hata kama klabu hiyo itatoa dau la rekodi la zaidi ya pauni milioni 170. (Talksport)
Manchester United wanatarajia kuwasilisha rasmi ofa kwenda Newcastle United kwa ajili ya kiungo wa Italia Sandro Tonali, 25, mwishoni mwa msimu. (Mail)
Pia Manchester United wamemuongeza beki wa kushoto wa Arsenal Myles Lewis-Skelly, 19, kwenye orodha yao ya wachezaji wanaowahitaji majira ya kiangazi, huku mchezaji huyo akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara. (Daily Express)
Paris Saint-Germain na AC Milan wanafuatilia kwa karibu hali ya mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 28, ambaye yuko kwa mkopo, na wako tayari kuchukua hatua iwapo Barcelona watashindwa kumsajili moja kwa moja majira haya ya kiangazi. (Caughtoffside)
Aston Villa nao wanapanga kumsajili Marcus Rashford iwapo watashindwa kumsajili mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 26, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Manchester United lakini mkataba wake unaisha msimu huu wa joto. (SportsBoom)
Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, 26. (Football.London)
Liverpool wanatafuta kumsajili mshambuliaji wa Senegal Iliman Ndiaye, 26, kutoka kwa wapinzani wao wa jiji Everton. (Teamtalk)
Iliman Ndiaye pamoja na kiungo wa Everton James Garner, 25, pia wako kwenye rada ya Manchester United katika dili la pamoja linaloweza kufikia pauni milioni 100. (Fichajes)
Newcastle United wanamchukulia beki wa Arsenal Ben White, 28, kama mbadala wa Kieran Trippier, 35 iwapo ataaondoka. (Sports Boom)
Paris Saint-Germain haitarajii kwamba Arsenal itawasilisha ofa kwa ajili ya winga wake Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 25, huku Arsenal pia wakimsaka pia mshambuliaji wa Newcastle United Anthony Gordon, 25. (Sky Sports)
Atletico Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ferran Torres, 26, ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji. (Fichajes)
Beki wa kushoto wa Barcelona Alejandro Balde, 22, anavutiwa na Manchester United, Manchester City na Aston Villa. (Mundo Deportivo)
Sunderland wanaweza kupata changamoto kumbakiza mchezaji wao aliyepo kwa mkopo akitokea RB Leipzig Lutsharel Geertruida, 25, huku klabu kadhaa zikiwemo Liverpool, Aston Villa, Everton, Tottenham Hotspur na Crystal Palace zikionesha nia ya kumsajili. (Teamtalk)