Ima wakuue au ujiue mwenyewe: Kilichotokea katika eneo la kuajiri na kuangamiza vijana

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya jamaa za watu waliopotea walitambua mali za wapendwa wao miongoni mwa zilizopatikana huko Rancho Izaguirre.
    • Author, Dario Brooks
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Picha na video za rundo kubwa la viatu, nguo, na vitu binafsi zilisambaa ulimwenguni zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Walikuwa ni watu waliopitia katika eneo la Rancho Izaguirre.

Vitu hivyo vilipatikana kupitia juhudi za kundi la Guerreros Buscadores de Jalisco (GBJ), shirika la wazazi wa waliotoweka katika jimbo hilo la magharibi mwa Mexico.

Matangazo ya moja kwa moja waliyoyafanya kwenye Facebook Machi 5, 2025 pia yalifichua kwamba eneo hilo huenda lilitumika kuwaua watu wengi katika eneo linalotawaliwa na gende la Jalisco New Generation Cartel (CJNG).

Raúl Servín, mmoja wa wazazi wa GBJ, aliiambia BBC Mundo wakati huo kwamba walipata maganda ya risasi na majarida, pamoja na makaburi ya siri na alama za matumizi ya moto.

Ugunduzi huo uliishtua Mexico na kuvuka mipaka ya kimataifa kwa sababu ilionekana kuwa eneo la kuajiri watu la CJNG lilikuwa pia ndio eneo la mauaji ya halaiki.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (FGR) ilichukua jukumu la uchunguzi, lakini tangu wakati huo imekataa kwamba kulikuwa na "tanuri za kuchomea maiti" au aina yoyote ya mabaki ya binadamu kupotea.

"Uchunguzi umebaini kwamba eneo hilo lilitumika kama uwanja wa mafunzo," Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilisema Machi 5.

,ik

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idadi ya viatu vilivyotelekezwa, wachunguzu wanasema hii inafanana na kambi za mateso.

Tangu wakati huo kumekuwa na maendeleo kadhaa katika uchunguzi:

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

• Watu 47 wanaohusiana na uendeshaji wa shughuli hizo wamekamatwa.

• Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inasema imeshughulikia 64% ya ushahidi uliopatikana na uchunguzi bado unaendelea.

• Washtakiwa kumi walihukumiwa kifungo cha miaka 141 jela kwa kutoweka na mauaji ya watu watatu katika eneo hilo.

• José Ascensión Murguía Santiago, meya wa Teuchitlán, alikamatwa na anatuhumiwa kuwa mshirika wa uhalifu huo.

• Waajiri wawili wanaoshukiwa kuwa wa CJNG waliokuwa wakiwapeleka vijana Rancho Izaguirre walikamatwa na wanashtakiwa kwa makosa kadhaa.

Ushuhuda wa wanaume na wanawake wanaodai kuwa walikuwepo Rancho Izaguirre inaeleza kuwa mauaji na kutoweka kwa vijana wengi waliopelekwa huko kwa ajiliya kazi rasmi.

Mwandishi wa habari za uchunguzi Sandra Romandía alipata ushuhuda wa baadhi ya manusura hao na, baada ya miezi kadhaa ya kazi, akachapisha kitabu "Witnesses of horror: the truth that was hidden at Rancho Izaguirre."

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya ugunduzi huo, Romandía alizungumza na BBC Mundo kuhusu kinachojulikana juu ya kilichotokea hapo na mashaka yanayoendelea juu ya uchunguzi.

BBC Mundo iliomba kuzungumza na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuhusu kesi hiyo, lakini haikupata jibu kabla ya kuchapishwa makala haya.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha hii inaonyesha kwa ndani jumba linalochunguzwa na serikali ya Mexico.

Kile ambacho manusura wanakitaja ni kwamba ni kama kambi ya wafanyakazi wa bei rahisi kwa genge la wahalifu. Ni kana kwamba eneo hili kituo ambacho wanawake wanapika na kuna madaktari kwa ajili ya Wapiganaji —kwa sababu pia kuna dalili kwamba waliwateka nyara madaktari—wanaowatibu.

Kwa hivyo Rancho Izaguirre kilikuwa ni kambia ya usambazaji wa wafanyakazi kwa ajili ya Jalisco New Generation Cartel.

Mashuhuda wanaelezea kila kitu kuanzia aina za mafunzo, kama unaweza kuyaita hivyo, wanayopokea hapo, lakini pia ukatili huu wote, uhalifu huu wote unaofanywa na watu wanaohusika.

Wengi waliweza kutoroka kwa njia tofauti: katika makabiliano, wakati wakubwa wao hawakuwa makini. Waliweza kukimbia, lakini kwa namna fulani waliweza kusimulia hadithi—hadithi hii ya jinsi walivyoajiriwa na uwongo, jinsi walivyotishiwa kupigania maisha yao, na kuishi.

Na katika jaribio hilo la mapambano, iliwabidi kuwaua watu wengine, kuwakata vipande vipande watu wengine, kuchoma miili mingine, kula nyama ya binadamu, kuishi kwa minyororo.

Walilazimika kufuata maagizo kwa usahihi: wakati waliolazimika kwenda bafuni; wakati waliolazimika kuvaa suruali; wakati waliolazimika kuvua nguo; ikiwa wangelazimika kufanya push-up 50, walilazimika kufanya hivyo kwa sababu vinginevyo walijua wangepigwa au hata kuuawa; na jinsi wanavyoelezea jinsi walivyogeuka ghafla kuwa kitovu cha burudani kwa viongozi wa kundi la wahalifu.

Wakiwafanya wapigana au kuwafanya watesane au wateswe ili kila mtu aweze kuiona kana kwamba ni tamasha, jambo ambalo linazungumzia kiwango cha ukatili wa makundi haya na pia mbinu za kudhalilisha utu zinazotumika dhidi ya waathiriwa.

Wanawafanya wakae huko kama mazezeta, wakijaribu tu kuishi chini ya amri za makundi haya ya wahalifu.

Wakuuwe au ujiuwe

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ardhi hiyo ilianzishwa kwa ajili ya mazoezi ya kimwili, lakini watafutaji wa watu waliopotea walipata ushahidi wa makaburi ya siri.

Wakati mmoja katika kitabu hicho, mtu anasema, "Kuna njia mbili tu za kutoka hapa: ama watakuua, au wewe ujiue."

Hizi zilikuwa hali mbaya na zisizo na utu. Mmoja wa mashahidi anasimulia jinsi alivyoajiriwa kwa nguvu kupitia udanganyifu, kutekwa nyara, kuteswa, na kupitia awamu zote, ambazo zilikuwa za kutisha.

Kama wangekuwa 100 katika kundi lao, 30 tu ndio walinusurika.

Anasimulia jinsi alivyoona baadaye kundi jipya likiwasili, na alikuwa na silaha na akasema, "Ningeweza kufanya jambo fulani kuwatetea, lakini sikufanya chochote kwa sababu nilijua kwamba ningeweza pia kupigwa ikiwa ningewafanyia chochote."

Kwa hivyo alijifanya kama mwanachama mwingine tu wa genge la wahalifu ili aweze kuishi, lakini kwa kweli alikuwa akifikiria, "Nifanye nini ili kuwaokoa watu hawa?"

Tulijaribu kuzungumza na watu wa eneo hilo, na niliweza kuona hofu iliyohisiwa na wakazi wa Teuchitlán, na haswa La Estanzuela.

Lakini kila mtu alikuwa na muktadha wake; yaani, watu wengi walishuku kwamba huenda kulikuwa na shughuli haramu katika eneo lao. Waliiona kwa sababu baadhi ya viwanja vya majirani zao vilikuwa vikipigwa mnada, na hakuna aliyeelezea ni kwa nini.

Na polisi wa manispaa, ofisi ya meya, n.k., walikuwa wakiwalinda wahalifu, kama hii inavyoonyeshwa tayari katika baadhi ya taarifa, katika kesi inayoendelea dhidi ya meya.

Kuwadanganya vijana

p

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jalisco imekusanya zaidi ya ripoti 16,000 za watu waliopotea, kulingana na takwimu rasmi

Kwa kuwa vijana wengi waliajiriwa karibu au katika manispaa zilizo karibu na Guadalajara au jimbo la Jalisco, baadhi huko Nayarit, wengine huko Zacatecas, baadhi huko Michoacán, ambazo ni majimbo yanayopakana na jimbo la Jalisco, walichofanya ni kuwaahidi kazi ya aina yoyote kwanza.

Wangeweza kuwa wahandisi wa kompyuta, walinzi wa usalama, madereva, wafanyakazi wa ujenzi, na walipewa malipo mazuri. Yote yalifanyika kupitia WhatsApp, Facebook, na mitandao mingine ya kijamii.

Vijana hao walipitia baadhi ya majaribio kupitia simu au ujumbe mfupi, na mtu alipoambiwa kwamba amechaguliwa, aliambiwa: "Tutakutumia tiketi yako ya basi kwenda kituo cha mabasi cha Tlaquepaque" (Guadalajara). Wangefika huko na kuchukuliwa na Uber au teksi ili kupelekwa kwenye "ofisi za kampuni."

Bila shaka, wengi wao hawakuona kuwa jambo la kutiliwa shaka sana kwa sababu baadhi walifika mchana. Baadhi walifika wakiandamana na wafanyakazi wenzao ambao inadaiwa walikuwa wanaenda kazini.

Na nini kilitokea? Baada ya Uber hiyo kuwasili, ambayo kwa kweli ilikuwa ni gari binafsi, walitekwa nyara, walitishiwa silaha, simu zao zilichukuliwa na walipelekwa Rancho Izaguirre au maeneo mengine ili kupewa mafunzo ya lazima.

Mtu yeyote aliyepinga alikufa wakati huo.

Uchunguzi zaidi unahitajika

ol

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jeshi la Taifa lilivamia eneo hilo Septemba 2024, lakini wakati huo hawakuripoti kuona shughuli zilizoelezwa na wanaharakati.

Mwandishi anasema, mamlaka ndizo zinazohitaji kuchunguza kwa undani zaidi. Ninachoweza kusema ni kile ambacho ushuhuda unasema.

Kwa mfano, kuna tuhuma za kukausha maiti ili ziungue haraka zaidi katika vipande vidogo. Na wengine waliosema walitupa baadhi ya mabaki kwenye tangi la maji taka.

Wale wetu ambao tumeandika kuhusu biashara ya dawa za kulevya nchini Mexico kwa miaka hii yote tunafahamu mbinu tofauti ambazo makundi ya wahalifu yamebuni ili kuepuka kuacha alama yoyote.

Kwa hivyo nadhani hilo ni jukumu la mamlaka kufanya uchunguzi wa kina.

Kulingana na ushuhuda, naweza kusema kwamba watu hapo walionewa. Miili yao ilikatwa vipande vipande, ikaachwa ikauke kwenye jua, ikachomwa moto, na kuzikwa. Pia walielezea aina fulani ya oveni, zilizotengenezwa kwa mbao na mawe. Na nilipokuwa kwenye shamba la mifugo, niliona sehemu za vitu vilivyochomwa moto, vipande vilivyochomwa moto. Kulikuwa na ishara kwamba vitu vilikuwa vimechomwa moto.

Lakini mimi si mtaalamu wa kusema kama hiyo inalingana na kuchomwa kwa mifupa ya binadamu. Mmoja wa maafisa kutoka Jalisco aliniambia kwamba mabaki hayo lazima yalitokana na moto mkubwa.

Kwa hivyo ni sehemu ya mahitaji kutoka kwa vyombo vya habari na kutoka kwa raia kujua zaidi na kwa uchunguzi wa kina zaidi.

m

Chanzo cha picha, GettyImages

Maelezo ya picha, Kutoweka kwa miili ya wanafunzi 43 kutoka Ayotzinapa mwaka 2014 kulihusishwa na kuchomwa kwa maiti, lakini wanasayansi wanakataa dhana hiyo.

Ukweli ni kwamba ikiwa ranchi ya Izaguirre ilikuwepo na ilidhibitiwa na kundi la wahalifu linalotawala angalau majimbo 20 katika nchi hii, basi ni wazi wanaweza kutumia mbinu zile zile kupata wafanyakazi katika majimbo 20 ya nchi hii.

Ninachotaka pia kusema ni kwamba maeneo mengi zaidi ya mbali ya Jalisco yanahitaji kuchunguzwa: Baadhi tayari zimepatikana, kwa mfano, Rancho de la Vega, ambapo gazeti la El Universal lilikuwa na ushuhuda kutoka kwa watu walionusurika na walioishi kama huko Rancho Izaguirre.

Ni wazi kwamba haikuwa mahali pekee ambapo wanadamu waliajiriwa kwa nguvu, kufunzwa, na kuangamizwa.

Mwaka mmoja baada ya matukio na madai hayo, maswali mengi yanabaki. Haya yaliyotokea—haikuwa siku moja tu, wiki mbili, wiki tatu, mauaji matano—hapana, ilikuwa ni kitu cha kimfumo na cha kutisha kilichodumu kwa muongo mmoja.

Sizungumzii meya pekee, maafisa wachache wa polisi, na watu wengine wanne wanaoshikiliwa. Operesheni kubwa, ya kikatili, na kubwa kama hiyo haiwezi kudumishwa na wao pekee. Lazima kuwe na ushirikiano zaidi wa polisi na taasisi, na viongozi ndani ya kundi ambao wanahitaji kushtakiwa.