Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Wasiwasi waikumbuka Bayern Munich huku ligi ya Saudia ikijaribu kumshawishi Hary Kane

Muda wa kusoma: Dakika 2

Rais wa heshima wa Bayern Munich Uli Hoeness anahofia Ligi ya Saudia inajaribu kumshawishi mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiendelea na mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kuhusu mkataba mpya zaidi wa msimu wa joto wa 2027. (Kicker - in German)

Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 31, ameiambia Manchester City kwamba ataondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Offside Trap)

Aston Villa, Bayern Munich, Chelsea na Liverpool wanamfuatilia beki wa Crystal Palace Mfaransa Maxence Lacroix, 25. (TeamTalks}

Liverpool na Newcastle United wanavutiwa na mshambuliaji wa klabu ya Ureno ya Sporting na Colombia Luis Suarez, 28. (Correio da Manha - In Portugal)

Kiungo wa kati wa Uskoti Scott McTominay haongei na vilabu vya Saudi Pro League kwani lengo la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 linasalia Italia na Napoli. (Fabrizio Romano)

Barcelona itampa mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 37, ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo inamalizika msimu wa joto, mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao unajumuisha kupunguzwa kwa mishahara na bonasi zaidi zinazohusiana na utendaji. (Sport - In Spanish)

Juventus wanaangalia uwezekano wa kuwaongeza Lewandowski na fowadi wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 27, ambaye yuko kwa mkopo Tottenham kutoka Paris St-Germain, kwenye safu yao. (Gazzetta dello Sport - In Italy)

Mlinzi wa Chelsea na Ufaransa Malo Gusto, 22, anasema Liam Rosenior ni "meneja mkuu" licha ya kukosolewa kufuatia kiwango duni cha hivi majuzi. (ESPN)

Inter Miami wameanza mazungumzo na kambi ya kiungo wa kati wa Brazil Casemiro kuhusu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye ataondoka Manchester United majira ya joto, lakini timu hiyo ya Ligi Kuu ya soka inakabiliwa na ushindani kutoka kwa timu nyingine za Ulaya na Saudi Arabia. (Fabrizio Romano)