Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Bayern na Man Utd zampigania Anderson wa Nottigham Forest

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Kiungo wa Nottigham Forest Elliot Anderson
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wanatarajiwa kukabiliana na ushindani katika kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, 23, kwani Bayern Munich nao wako tayari kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Mail +)

Winga wa Aston Villa, Mwingereza Morgan Rogers, 23, anaweza kulazimika kutafuta timu ili kucheza Ligi ya Mabingwa ikiwa kikosi cha Unai Emery kitashindwa kufuzu kwa mashindano ya msimu ujao. (Talksport)

Winga wa Arsenal, Mbrazili, Gabriel Martinelli, 24, anakabiliwa na mustakabali usiojulikana katika klabu hiyo pamoja na beki wa kushoto wa Uingereza Myles Lewis-Skelly, 19, na winga raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18, Ethan Nwaneri. (Times)

Newcastle wanaogopa kuingizwa kwenye sakata jingine la mtindo wa Alexander Isak na kiungo wa kati wa Italia, Sandro Tonali, 25, huku kukiwa na uvumi wa kuhamia Manchester United, Manchester City, Chelsea au Real Madrid kwa pauni milioni 100. (The I)

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Sandro Tonali

Beki wa Manchester City, Nathan Ake analengwa na AC Milan na Inter Milan huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 31, akishindwa kupata nafasi ya kuanza msimu huu. (Caughtoffside)

Arsenal haina nia ya kumruhusu mlinzi wake raia wa Italia mwenye umri wa miaka 23 Riccardo Calafiori kuondoka msimu huu wa joto licha ya vilabu vya Serie A ikiwemo Inter Milan, AC Milan, Juventus na Napoli kutaka kumsajili. (Teamtalk)

Liverpool wanatazamia kumsajili kiungo wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 23, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Juventus wanasikiliza ofa za kumnunua Jonathan David, 26, huku West Ham, Tottenham na Nottingham Forest zote zikionyesha nia ya kumnunua mshambuliaji huyo raia wa Canada. (Tuttosport)

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Khvicha Kvaratskhelia

Paris St-Germain hawana mpango wowote wa kumuuza winga wao raia wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia mwenye umri wa miaka 25 kwa Arsenal. (Fabrizio Romano)

Nahodha wa Roma, Lorenzo Pellegrini anahitajika na Juventus huku kiungo huyo mshambuliaji raia wa Italia mwenye umri wa miaka 29 akiwa hana mkataba na Giallorossi mwishoni mwa msimu. (Gazzetta dello Sport)