Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumamosi: Rashford anaweza kurejea Man Utd
Marcus Rashford anaweza kurudi Manchester United msimu huu wa joto, Tottenham wanatafuta mchezaji wa kuchukua nafasi ya Igor Tudor na Arsenal wanaandaa mkataba na Leon Goretzka.
Mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, anaweza kurudi Manchester United baada ya muda wake wa mkopo Barcelona, ambao wanamtaka winga wa Chelsea na Ureno Pedro Neto, 26, kama mbadala. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Rashford anataka kubaki Barca, lakini mazungumzo yamegonga mwamba na mkurugenzi wa michezo Deco amependekeza msimu mwingine wa mkopo ili kuwapa timu hiyo ya Uhispania muda zaidi wa kulipa ada ya chaguo la kumnunua kutoka kwa Manchester United. (Talksport)
Tottenham wanaandaa chaguzi zinazowezekana za kuchukua nafasi ya Igor Tudor kama kocha mkuu ikiwa wataamua kufanya mabadiliko mengine ya usimamizi. (Athletic - subscription required)
Ingawa kocha wa Tottenham Tudor anatarajiwa kuendelea kuifundisha timu hiyo kwa muda mfupi, tayari amewatenga wachezaji kadhaa. (Talksport)
Napoli itaanzisha kifungu cha euro milioni 44 (£38m) cha kumnunua mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 23, na kufanya mkataba wake wa mkopo kutoka Manchester United kuwa wa kudumu. (Fabrizio Romano)
Manchester United ina orodha fupi ya makocha watano ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Michael Carrick msimu huu wa joto - kocha wa Crystal Palace Oliver Glasner, Unai Emery wa Aston Villa, Andoni Iraola wa Bournemouth kocha wa zamani wa Brighton Roberto de Zerbi na meneja wa Ujerumani Julian Nagelsmann. (Sun)
Arsenal wanajiandaa kutoa ofa rasmi ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ujerumani Leon Goretzka, 31, kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Hata hivyo, AC Milan pia wanavutiwa na Goretzka, ambaye Bayern Munich tayari wamethibitisha ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu. (Goal)
Arsenal inaweza kupata takriban pauni milioni 1.7 ikiwa Juventus itahamia kwa beki wa zamani wa Gunners na Poland Jakub Kiwior, 26, ambaye alijiunga na Porto kwa mkopo mnamo mwezi Septemba kukiwa na kipengele cha kununua kwa takriban pauni milioni 23. (Sun)
Liverpool itapata ushindani kutoka Barcelona ikiwa watafuatilia uhamisho wa beki wa kati wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 26. (Sport - in Spanish)
Manchester United wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa Bournemouth na Marekani Tyler Adams msimu huu wa joto, huku Chelsea na Liverpool pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Teamtalk)