Israel yashambulia kituo cha silaha kusini mwa Lebanon

Chanzo cha picha, EPA
Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) linasema limeshambulia kituo cha kuhifadhia silaha kusini mwa Lebanon.
Jeshi la IDF linasema liliwaona wanachama wa kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran wakibeba roketi hadi kwenye kituo hicho katika eneo la Al-Majadel siku ya Ijumaa.
Dakika chache baadaye Jeshi la Anga la Israeli lilishambulia ghala hilo na "kuwaangamiza" wanachama hao wa Hezbollah, inasema katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo cha picha, EPA
Moshi watanda baada ya shambulio la anga la Israel kusini mwa Lebanon
Picha mpya kutoka kusini mwa Lebanon, ambapo shambulio la anga la Israeli limesababisha uharibifu wa jengo katika eneo la Haret Saida huko Sidon.
Bado haijajulikana kama kumekuwa na majeruhi wowote.
Zaidi ya watu 770 wameuawa nchini Lebanon tangu kuanza kwa vita, kulingana na wizara ya afya ya nchi hiyo.
Soma zaidi:







