Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumapili:Newcastle bado wana nia na Trafford
Newcastle United itaendelea na nia ya kumsajili James Trafford, 23, ikiwa mlinda lango huyo wa Uingereza ataamua kuondoka Manchester City.(Football Insider)
Sean Dyche amebatilisha ripoti kwamba yuko kwenye mazungumzo ya kuchukua nafasi ya Igor Tudor kama meneja wa Tottenham Hotspur. (Talksport)
Barcelona, ​​Tottenham, Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia Evan Ndicka, huku Roma ikiwa tayari kukubali ofa zinazozidi pauni milioni 39 kwa beki huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 26. (Caught Offside)
Liverpool na Chelsea ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu vyenye nia ya kumsajili beki wa Uswisi wa OH Leuven Roggerio Nyakossi, 22, ambaye anakaribia mwaka wa mwisho wa mkataba wake. (Sun)
Mchezaji hodari wa kimataifa wa Uhispania Marcos Llorente, 31, anataka kubaki na Atletico Madrid na yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Hispania, licha ya kupendezwa na Ligi Kuu. (Fichajes)
Real Madrid ni miongoni mwa timu zinazovutiwa kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Adam Wharton, 22. (AS)
Beki wa kati wa Ujerumani Nico Schlotterbeck, 26, ambaye inasemekana alikuwa akiwindwa na Liverpool na Real Madrid, anakaribia kukubali mkataba mpya na Borussia Dortmund hadi 2031. (Florian Plettenberg)