Nchi tano zenye furaha zaidi duniani mwaka 2026

l

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Lindsey Galloway
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Ingawa nchi za Nordic zimetawala Ripoti ya Furaha Duniani kwa muda mrefu, lakini mwaka 2026 umeleta mshangao mmoja kwani ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 14 ya ripoti hiyo, nchi ya Amerika Kusini imeingia katika tano bora. Nchi ya Costa Rica imepanda hadi nafasi ya nne, ikiruka kutoka nafasi ya 23 mwaka 2023.

Viwango hivyo, vinavyotolewa kila mwaka na Gallup, Kituo cha Utafiti wa Ustawi cha Oxford, na Mtandao wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa, hutolewa kila baada ya miaka mitatu kwa kupima maisha ya wakazi katika nchi 140, kwa kutazama mambo kama vile Pato la Taifa, huduma za kijamii, matarajio ya maisha, uhuru, ukarimu na kiwango cha ufisadi.

Kwa mwaka wa pili mfululizo, hakuna nchi kubwa zinazozungumza Kiingereza zilizofika 10 bora, huku Australia ikiwa ya 15, Marekani ikiwa ya 23, Canada ikiwa ya 25 na Uingereza ikiwa ya 29.

Tulizungumza na wakazi wanaoishi katika kila nchi ili kujua ni nini kinachochangia furaha ya kila siku na ya muda mrefu - na jinsi wasafiri wanavyoweza kupata "maisha ya furaha" ya wenyeji wanapotembelea.

Finland

ol

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maktaba Kuu ya Helsinki Oodi ni mojawapo ya maeneo ya umma yenye sifa nzuri zaidi jijini humo

Kwa miaka tisa kati ya 10 iliyopita, Finland imekuwa nambari moja. Nchi hii ina alama ya juu katika masuala ya huduma za kijamii na kiwango kidogo cha ufisadi, na wakazi mara nyingi hutaja usalama wa kijamii - ikiwa ni pamoja na elimu na huduma za afya.

"Ninapenda ukweli kwamba Finland iko salama na ninaweza kumwamini mtu wa kawaida hapa," anasema Olli Salo, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Skimle yenye makao yake Helsinki.

"Watoto hutembea hadi shuleni kuanzia umri wa miaka saba, hujisikii kutishiwa, na kuna uaminifu kwamba ikiwa mtu atatoa ahadi mara nyingi ataitimiza."

Ingawa nchi ina kodi kubwa, lakini huduma zina ubora. "Mambo mengi muhimu maishani kama vile afya, elimu na usafiri ni huduma za umma, kwa nini tusitumie pesa na kupata huduma zenye ubora wa hali ya juu?" anasema.

Kwa Daniel Sazonov, meya wa sasa wa Helsinki, furaha pia hutokana na ukaribu na asili. "Kuweza kutoka nje, na baada ya dakika chache, kufika baharini, bustanini au msituni kwa ajili ya matembezi ya jioni ni jambo la kipekee," anasema.

Kwa takriban sauna milioni tatu kwa idadi ya watu milioni 5.5 pekee.

2. Iceland

p;

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtaa wa Skólavörðustígur katika mji mkuu wa Iceland
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikiipita Denmark hadi nafasi ya pili kwa mara ya kwanza tangu 2014, taifa hili la kisiwani lenye watu 400,000 pekee linashika nafasi ya kwanza kwa huduma nzuri za kijamii. Pia inashika nafasi ya 10 bora kwa Pato la Taifa kwa kila mtu, umri mkubwa wa kuishi na afya njema na ukarimu, huifanya kuwa mojawapo ya nchi bora katika orodha hiyo.

"Kihistoria, kutengwa kwetu kulimaanisha kuishi kwa juhudi za kikundi. Kwa karne nyingi, hakukuwa na msaada kutoka nje. Ni sisi tu, na ilibidi tusimame pamoja," anasema Ingibjörg Friðriksdóttir, mkazi wa Reykjavík na meneja wa masoko ya kidijitali katika Hoteli ya Rangá. "Urithi huo umeunda utamaduni ambapo kusaidiana ni asili yetu."

"Tunajifunza kuthamini nyakati za furaha: kupata kahawa, mabwawa ya maji ya joto na kutumia muda na marafiki," anasema Bryndís Björnsdóttir, mkurugenzi mkuu wa Laugará́s Lagoon huko Reykjaví́k. "Wakati wa kiangazi unapofika, ghafla tunapata mwanga wa mchana karibu usiku kucha, na kila mtu anakuwa na nguvu na furaha zaidi."

"Hewa safi, mandhari nzuri na hisia ya uhuru ni sehemu kubwa ya kinachofanya nchi hii kuwa nzuri," anasema Björnsdóttir. "Chakula kinafaa kutajwa pia," anaongeza, "hasa samaki wabichi."

3. Denmark

ol

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mito ya Copenhagen ni muhimu kwa maisha ya kila siku, huku wakazi wakiogelea mara kwa mara, wakiendesha mitumbwi na kupiga makasia

Denmark haijawahi kushuka chini ya nafasi ya nne katika historia ya ripoti hiyo na mara nyingi imekuwa ikichukua nafasi ya kwanza. Ikishika nafasi ya tatu mwaka huu, nchi hiyo pia inashika nafasi ya tatu duniani kwa huduma za kijamii na kiwango kidogo cha ufisadi, na ya saba kwa Pato la Taifa kwa kila mtu.

"Furaha sio kuhusu tabasamu kubwa na kucheka," anasema Laura Hall, mwandishi wa habari na mwandishi wa vitabu. "Kwa kweli ni kuhusu kuaminiana katika jamii, na kwamba kila mtu anafanya kazi pamoja kwa manufaa ya wote."

Hall anawalea mabinti wawili hapa na anasema hisia ya usalama ni ya kudumu. Pia anapenda bandari safi ya Copenhagen.

Huko Copenhagen, wageni huja wakiwa na hisia ya utulivu na amani - na wivu kidogo wanapowaona watu wakiendesha baiskeli wakiendelea na shughuli zao za siku kwa utulivu.

Hall anasema. "Hakuna utamaduni wa maisha magumu hapa."

Costa Rica

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mji wa pwani wa Las Catalinas usiotumia gari

Ikipanda hadi nafasi ya nne katika orodha ya mwaka huu, Costa Rica ndiyo nchi ya kwanza ya Amerika Kusini kuingia katika tano bora, huku alama zake za uhuru na huduma za kijamii zikiongezeka maradufu tangu 2021.

Costa Rica haijapanda kutokana na Pato la Taifa au huduma za serikali kama mataifa ya Nordic, lakini wakazi wanaripoti kuwepo kwa uhuru mkubwa wa kufanya maamuzi yao ya maisha.

Alipoulizwa ni nini kinachofanya Costa Rica kuwa mahali pa furaha, mkazi Adrian Hunt anasema. "jamii, jamii, jamii," anasema mtaalamu wa teknolojia anayeishi Las Catalinas, mji usio na magari kwenye pwani ya Guanacaste.

Asili pia ni chanzo cha furaha ya kila siku. Hunt anaelezea kuamka asubuhi, kutembea ufukweni na kuwatazama nyani wanaohama kutoka mti mmoja hadi mwingine huku samaki wakifukuzana kwenye ghuba.

"Naamini Costa Rica ina ubora bora wa maisha kuliko nchi yoyote Amerika ya Kati," Hunt anasema. "Kuna kitu kuhusu wenyeji na wageni, kinachofanya nchi hii kuwa ya kipekee sana."

5. Sweden

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Stockholm ndiko ambako maji, mbuga na maisha ya ujirani hayako mbali

Katika nafasi ya tano mwaka huu, Sweden imepanda kati ya nafasi ya nne na ya 10 katika muongo mmoja uliopita. Inashika nafasi ya saba duniani kwa maisha yenye afya na ya tano kwa uhaba wa rushwa. Uwepo wake katika ngazi za juu unaonyesha kile ambacho wakazi wanakielezea kama usawa kati ya maisha ya mijini na mazingira.

"Sababu moja kuu kwa nini Sweden inashika nafasi ya juu sana katika furaha ni kwamba sisi ni nchi ndogo," anasema Micael Dahlen, profesa wa ustawi, na furaha katika Chuo cha Uchumi huko Stockholm. "Umbali ni mdogo - kati ya watu, kati ya miji na asili. Tumejifunza kuaminiana na kutegemeana, kupeana na kuthamini kile tulicho nacho, kuishi na asili na kukaribisha mawazo na watu wapya."

"Ninapenda watu na wema wao, mwendo wa polepole wa maisha, asili nzuri na mandhari, na hisia kwamba nilifanya chaguo zuri kwa ajili ya mustakabali wangu na kwa ajili ya mustakabali wa watoto wangu," anasema Karolina Pikus, aliyehamia hapa kutoka Poland.

Huko Gothenburg, anapenda kwamba anaweza kuogelea baharini, kutembelea ziwa na kutembea msituni, yote hayo kwa siku moja kutokana na usafiri wa umma uliounganishwa vizuri.

Nchi 10 Bora zenye Furaha Zaidi kwa Mwaka 2026