Je, pazia inayofunika eneo takatifu la Kaaba ilitumwa kwa Jeffrey Epstein?

Chanzo cha picha, EPA
Kutolewa kwa nyaraka zinazoonyesha kwamba vipande kadhaa vya pazia la Kaaba, eneo takatifu zaidi kwa waumini wa dini ya Kiislamu, vilitumwa kwa Jeffrey Epstein, mfadhili mashuhuri na mhalifu wa ngono, kumeibua wimbi ghadhabu miongoni mwa Waislamu duniani kote.
Katika sehemu ya hati zinazohusiana na Jeffrey Epstein zilizotolewa na Idara ya Sheria ya Marekani mnamo Januari 30, kuna barua pepe kutoka 2017 zinazorejelea kutumwa kwa vipande vitatu vya pazia ya Kaaba kutoka Saudi Arabia hadi nyumbani kwa Jeffrey Epstein huko Carribea.
Mtumiaji wa mtandao wa kijamii X aliandika: "Fikiria kutuma kipande cha mahali patakatifu zaidi duniani kwa mtu mchafu zaidi!"
Katika picha nyingine ya mwaka wa 2014, Jeffrey Epstein na mwanamume mwingine wanaonekana wakichunguza kipande cha kitambaa kilichopo chini ambacho kinafanana na sehemu ya kifahari zaidi ya pazia la Kaaba, kinachofunika mlango wake.

Chanzo cha picha, Source: US Department of Justice
Mtumiaji mwingine kwenye X aliandika kwamba picha hiyo "iliuvunja moyo wake vipande elfu moja," wakati alipoona pazia la Kaaba "lililoenea kama zulia sakafuni."
Hata hivyo, picha hiyo haionekani kuhusishwa moja kwa moja na nyaraka zinazoonyesha kwamba vipande vya pazia la Kaaba vilitumwa kwa Jeffrey Epstein mwaka wa 2017.
Pia haijulikani ikiwa kitambaa kinachoonekana kwenye picha ni sehemu ya pazia la Kaaba.
"Msikiti"
Pazia la Kaaba (kiswah), lililotengenezwa kwa hariri nyeusi, limepambwa kwa aya za Quran kwa dhahabu na uzi. Inafunika kuta nne za nje za muundo wa mawe wa Kaaba katikati mwa Msikiti Mkuu huko Makka.
Pazia hili hubadilishwa na kitambaa kipya kila mwaka wakati wa sherehe inayoambatana na mwanzo wa Mwaka Mpya wa Lunar, baada ya mamilioni ya mahujaji kuigusa.

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Nyaraka za Idara ya Haki zinaonyesha mawasiliano kati ya wafanyikazi wa Epstein na akaunti ya barua pepe inayoitwa "Aziza Al-Ahmadi" ambayo inadaiwa ilijadili kutuma vipande vitatu vya pazia la Kaaba kwa Epstein mnamo 2017: kipande cha kijani kibichi kutoka ndani ya Kaaba, kitambaa cheusi kutoka kwa kifuniko cha nje kilichotumika hapo awali, na kipande kilichopambwa lakini ambacho hakijatumika.
Katika barua pepe ya Februari 1, 2017, msaidizi wa mtu aliyejulikana kama "Ahmadi" aliwaambia wafanyakazi wa Epstein kwamba "wangetuma vipande kadhaa vya pazia la Kaaba kwenye msikiti." Haijulikani ikiwa walimaanisha na "msikiti" eneo au mali ya Jeffrey Epstein.
Hakuna kutajwa kwa msikiti kwenye kisiwa cha Epstein katika hati zilizopitiwa hadi sasa. Hata hivyo, nyaraka zilizochapishwa kwenye tovuti ya Idara ya Haki zinarejelea jengo dogo linaloitwa "hekalu." Haijulikani wazi kutoka kwa mawasiliano mahali palipolengwa.
"Msikiti" uliotajwa katika nyaraka hizi usifananishwe na Msikiti Mkuu wa Makka, ambao ni nyumba ya Kaaba.
Hati zinaonyesha shehena hiyo ilifika nyumbani kwa Jeffrey Epstein's Palm Beach mnamo Machi 4, 2017, na kisha kutumwa kwa St. Thomas katika Visiwa vya Virgin vya Marekani.
Eneo hilo liko karibu na kisiwa cha kibinafsi cha Little St. James, ambapo waathiriwa kadhaa wamedai kuwa walidhulumiwa baada ya kuuzwa huko.
Kwenye fomu ya forodha ya Marekani ya Machi 14, 2017, usafirishaji huo ulitangazwa kuwa "michoro na pastel" na thamani yake ilikuwa $10,980.
Barua pepe ya tarehe 21 Machi pia inathibitisha uwasilishaji wa vipande vya pazia vya Kaaba kwenye "nyumba ya Bw. Epstein."
Baada ya shehena hiyo kutumwa, barua pepe ambayo inaonekana ilitumwa kutoka kwa akaunti ya Bi Ahmadi ilimwambia Jeffrey Epstein kwamba kipande cha kitambaa cheusi kilikuwa kimeguswa na "angalau Waislamu milioni 10 wa imani tofauti, Sunni, Shia na wengineo."
Barua pepe hiyo inasema: "Wanaizunguka Al-Kaaba mara saba, kisha kila mtu anajaribu kuigusa kadiri awezavyo; wanaweka sala zao, matakwa, machozi na matumaini kwenye kitambaa hiki."
Bado haijulikani ikiwa Jeffrey Epstein alipokea vipande hivi kama zawadi au kama vitambaa hivi vilikuwa vipande vya pazia la Kaaba.
Hata hivyo, kulingana na rekodi za Idara ya Haki ya Marekani, hii haikuwa shehena ya kwanza kutumwa kutoka Saudi Arabia hadi kwa Epstein.
Katika msururu wa barua pepe wa Januari 27, 2017, mtu anayesemekana kuwa msaidizi wa Bi Ahmadi alidaiwa kuomba "picha za ndani za msikiti" ili kuruhusu maandalizi ya "kitu ndani ya msikiti." Katika mlolongo huo huo, mmoja wa wasaidizi wa Epstein alithibitisha kuwasili kwa "hema na vitu vingine vya nyumbani" nyumbani kwake.
Katika hati za Idara ya Haki ya Marekani, kuna ushahidi unaoonyesha picha ya hema la kitamaduni la Waarabu na vitu vingine kama vile zulia, sufuria ya kahawa, kikombe na kikapu.
Hata hivyo, haiwezi kusemwa kwa uhakika kwamba hivi ndivyo vitu vilivyotumwa kwa Epstein katika usafirishaji huo.
Shehena zote mbili zilitumwa baada ya kutiwa hatiani kwa Epstein kama mshukiwa wa ngono mwaka wa 2008, wakati alikiri makosa mawili.
Aziza Ahmadi hakujibu ombi la BBC la kutaka maoni yake. Kutaja majina katika hati sio ushahidi wa kufanya makosa.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa kwenye faili za Epstein hadi sasa, licha ya neno "msikiti" kutajwa kwenye barua hizo, hakuna ushahidi wala anuani maalum ya kuwepo kwa jengo hilo kisiwani humo.
Jeffrey Epstein aliunda muundo unaofanana na hekalu kwenye Kisiwa cha Little St. James kati ya 2009 na 2013, jumba lake la dhahabu ambalo liliharibiwa na kimbunga cha 2017.
Hatahivyo, haijulikani ikiwa "msikiti" katika shehena zote mbili ulimaanisha jengo moja au eneo lingine kwenye mali yake.
"Msikiti" uliotajwa katika hati hizi haupaswi kufananishwa na Msikiti Mkuu wa Makka, ambapo Kaaba ipo.
Inaheshimika, lakini si takatifu.

Chanzo cha picha, EPA
Mamlaka za Saudi zina udhibiti kamili juu ya pazia la Kaaba, kuanzia jinsi linavyotengenezwa, kuwekwa , na kutolewa hadi jinsi mapazia ya zamani yanavyotumika. Hata hivyo, hakuna sheria maalum juu ya jinsi mapazia ya zamani yanapeanwa.
BBC imewasiliana na mamlaka ya Saudia kwa taarifa zaidi, lakini haijapata jibu kufikia wakati wa habari hii kuchapishwa.
Ahmed Halabi, mwandishi aliyebobea katika masuala ya Hijja na Umrah, aliiambia BBC Arabic: "Sehemu zilizopambwa kwa dhahabu na fedha, zinazojulikana kama Ḥizam (mkanda) na samadiyah, hutolewa tu na maafisa wa ufalme wa Saudi."
Anaongeza: "Vipande hivi vinatolewa kwa wakuu wa nchi za Kiislamu na maafisa wao wa serikali."
"Kitambaa cheusi kinachobaki kwa kawaida hukatwa vipande vidogo na huenda wakapewa maafisa wa ngazi za chini," asema Bw. Halabi.
Dk Simon O'Meara, mwanahistoria wa sanaa ya Kiislamu katika Shule ya Mafunzo ya Mashariki na Afrika, Chuo Kikuu cha London, anasema pazia la Kaaba si "takatifu kwa asili" lakini linaheshimiwa sana katika ulimwengu wa Kiislamu.
Anasema, "nguo hiyo inaipa utakatifu jengo la Kaaba, kama vazi la mfalme."
Anaongeza: "Baada ya kuondolewa kwa pazia la Al-Kaaba, haifai kuharibiwa wala kukanyagwa."
Wakati huo huo, Bwana Halabi pia anaelezea shaka juu ya ukweli wa kipande kilichotajwa katika barua iliyochapishwa na Idara ya Sheria ya Marekani, akisema kuwa kupeana pazia la Kaaba kwa wasio Waislamu hairuhusiwi.

Chanzo cha picha, Source: US Department of Justice
Mawasiliano ya Saudi
Kulingana na hati kutoka Idara ya Haki ya Marekani, kuanzia mapema 2016 hadi mapema 2019, Bi Ahmadi alibadilishana barua pepe nyingi na Jeffrey Epstein kuhusu mada mbalimbali.
Katika baadhi ya barua pepe hizi, alimtaja Epstein kama "bosi" na "bwana," na hati zinaonyesha kwamba walikutana katika miji kama New York na Paris.
Kulingana na nyaraka zilizochapishwa, Jeffrey Epstein inaonekana alijaribu kushawishi serikali ya Saudi Arabia kupitia Aziza Ahmadi.
Mnamo Julai 2016, barua pepe iliyotumwa chini ya jina "Ahmadi" inaonyesha kwamba alikuwa akijaribu kupanga mkutano kati ya Jeffrey Epstein na mtu aliyetambuliwa kama "H.E. Raafat." Neno "HE" huenda ni kifupisho cha Mheshimiwa, ambacho hutumiwa nchini Saudi Arabia kwa maafisa wa juu wa serikali.
Rekodi za barua pepe zinaonyesha kuwa mtu huyu "alifurahia" uwepo wa Epstein karibu naye.
Nyaraka za Idara ya Haki ya Marekani zinaonyesha kwamba Jeffrey Epstein alipendekeza "kukaguliwa kifedha" katika barua pepe kwa mtu anayeitwa "Ahmadi" mnamo Agosti 2016, akibishana dhidi ya utoaji kwa umma wa Aramco (ambayo ni kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Saudi Arabia).
Ahmadi baaadaye anaonekana kujibu kwamba "angechunguza" suala hilo, na pia akatuma nakala ya barua pepe kwa mtu aliyemwita "Raafat Al-Sabbagh."
Barua pepe kutoka kwa akaunti ya mmoja wa washirika wa Epstein mnamo Novemba 2016 ilisema: "Aziza ni msaidizi wa Bw. Raafat." Katika barua pepe kadhaa kwa wapokeaji tofauti, Jeffrey Epstein alionekana akielezea "Raafat Al-Sabbagh" kama "mshauri" wa "naibu mkuu wa Saudi Arabia."
Katika tangazo la 2017 kutoka kwa Shirika rasmi la Wanahabari la Saudi, alijulikana kama "mshauri wa familia ya kifalme."
Kulingana na barua pepe katika hati za Idara ya Haki ya Marekani, mtu anayeitwa "Sabbagh" anaonekana kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Epstein. Ujumbe wa maandishi wa 2016 kutoka kwa akaunti inayoitwa "Raafat Sabbagh" kwa Epstein ulisomeka: "Ninajivunia kuwa rafiki yako."
Katika barua pepe kutoka kwa "Rafat Al-Sabbagh," Epstein alitumiwa kiungo cha taarifa kuhusu malkia wa urembo wa Urusi mwenye umri wa miaka 17 ambaye inadaiwa alikimbilia Dubai kuuza ubikira wake. Epstein alijibu: "Mwishowe ulinitumia kitu cha maana."















