Mataifa ambayo muda wa kufunga Ramadhan utakuwa mrefu zaidi 2026

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan 2026, unatarajiwa kuaanza Jumanne February 17 na kwa mataifa mengine itakuwa Februari 18.
Kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, ni mojawapo wa nguzo tano ya dini ya kiislamu, na inamlazimu kila muumini wa Kiislamu ambaye ametimiza vigezo kufunga.
Watu hufunga kwa siku 29 au 30 mwezi huo, kuanzia alfajiri hadi jua linapotua.
lakini, muda wa kufunga hutofautiana katika kila taifa, na ndio maana kuna utofauti wa jinsi Ramadhan huadhimishwa kote duniani.
Msimu wa majira ya joto haswa katika mataifa ya Ulaya, wao hushuhudia siku ndefu kabla ya jua kutua, huku mataifa mengine ya bara Afrika yakishuhudia joto kali, suala ambalo huathiri ratiba yao ya kufunga.
Kutokana na utofauti huu, BBC ilichambua ratiba tofauti za kufunga katika nchi tofauti ulimwenguni.
Sababu ya tofauti ya muda

Chanzo cha picha, Simwal Usman Jibril
Ili kuelewa tofauti za ratiba ya Ramadhan, BBC ilizungumza na Simwal Usman Jibril, mwanachama wa kamati ya wanaotazama mwezi nchini Nigeria, ambaye alielezea kuwa kuna vipengele tofauti ambavyo huzingatiwa.
Alisema kuwa kufunga ni lazima kwa kila mtu, ila muda wa kufunga hutofautiana haswa kulingana na majira ya mwaka.
"Katika maeneo mengine duniani, waumini wa Kiislamu wanaweza kufunga hadi kwa saa 20 kwa siku, ila kuna maeneo mengine ambayo huwezi kufunga zaidi ya saa 10," alielezea katika mahojiano na shirika la BBC idhaa ya Hausa.
Maeneo ambayo msimu wa kufunga ni mrefu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Simwal Usman Jibril, anaelezea kuwa mfungo wa muda mrefu hushuhudiwa kaskazini mwa Ulaya na maeneo ya Aktiki, ambapo jua huonekana wakati wa jioni msimu wa majira ya joto.
Miongoni mwa miji inayoshuhudia mfungo wa muda mrefu ni Tromso-Norway kuanzia saa mbili hadi saa nne usiku, Reykjavik – Iceland kuanzia saa mbili hadi saa tatu usiku, Murmansk, Urusi, Stockholm - Uswidi, kuanzia saa kumi na mbili hadi saa moja jioni.
Kulingana na mtaalamu huyu, miji hii itashuhudia mfungo wa muda mrefu 'kwa sababu yako mbali na ikweta, ambapo jua hudumu kwa muda mrefu majira ya joto yakikaribia.'
Anaelezea kuwa msimu wa Ramadhan huja karibu na majira ya joto, kwa hivyo jua huonekana kwa muda mrefu, kwa hivyo kufanya mfungo kuwa wa muda mrefu.
Kulingana naye "Ramadhan hufuata kalenda ya mwezi ya kiislamu ambayo huwa na siku 10 chache au 11 kila mwaka . Mwezi wa Ramadhan hubadilika kila mwaka, hii ni kumaanisha muda wa kufunga hubadilika kila mwaka. "
Anaongezea kuwa changamoto huja wakati ambapo kuna maeneo ambayo jua halitui na kusema kuwa wataalam wa dini ya kiislamu wanashauri watu wa maeneo hayo kufuata mifano ya kama ya Makka, ambapo kuna usiku na mchana kila siku.
Maneo ambayo mfungo utakuwa mfupi
Mtaalam huyo anaelezea kuwa mataifa yaliyo kusini mwa ikweta yatashuhudia mfungo wa muda mfupi.
Mji hii ni kama Ushuaia – Argentina masaa 11, Punta Arenas- Chile masaa 11, Christchurch-New Zealand masaa 11, Cape Town - Afrika Kusini takriban masaa 12.
Simwal anasema Ramadhan mwaka huu inatarajiwa kuanza mwezi Februari "hii inaendana na majira ya kiangazi kusini mwa ikweta, kipindi ambacho hushuhudia siku fupi. Aidha maeneo haya huwa karibu na ikweta kwa hivyo hayashuhudii jua kali."
Mazingira ya kufunga nchini Nigeria
Simwal anadai kuwa kuna mataifa yaliyokaribu na ikweta ambapo siku za kuanza mfungo huwa hazibadiliki kila mwaka.
Miji hii ni kama Abuja-Nigeria, Jakarta-Indonesia, Kuala Lumpur- Malaysia na Nairobi Kenya.
Simwal anasema muda wa kufunga katika miji hii ni takriban saa 12 hadi 13. Hii ni kutokana na miji hii kupokea kiwango sawia cha mwangaza na giza kila mwaka huku kukiwa na utofauti mdogo sana wa muda ambao jua linachomoza na kutua.
Muda wa kufunga huamuliwa vipi?
Simwal anaelezea kuwa vipengele muhimu vinavyozingatiwa kuamua muda wa kufunga ni ikweta, hali ya hewa, maeneo ya kaskazini na kusini mwa dunia na kalenda ya kila mwezi ya kiislamu.
"Ingawa muda wa kufunga hutofautiana, Ramadhan ni mwezi ambao waumini wa Kiislamu kote duniani huimarisha ibada kwa kufunga na kuomba."
Nani anapaswa kufunga?
Yeyote anayekidhi vigezo vifuatavyo ni lazima afunge:
- Aliyebalehe kufikia wastani wa umri wa balehe wa miaka kumi na nne na nusu katika kalenda ya Gregorian)
- Mwenye akili timamu - mtu yeyote anayesumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao ama huwafanya wasijue kufunga, au wasiweze kuelewa wazo la kufunga (kama vile wale wanaosumbuliwa na Down Syndrome) hawatalazimika kufunga.
- Ikiwa si mgonjwa na mwenye magonjwa sugu ambayo huzuia kufunga, kama vile kisukari kali, au hata udhaifu kutokana na uzee.
- Msafiri ambaye haendi safari ya zaidi ya maili arobaini na nane.
- Kufunga hakutamdhuru mtu au mtoto wake (ikiwa mwanamke ni mjamzito au ananyonyesha).
Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula na kuhaririwa na Ambia Hirsi












