Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: PSG inamsaka Haaland Man City

Chanzo cha picha, Getty Images
Paris St-Germain imekuwa ikimfuatilia mshambuliaji wa Norway klabu ya Manchester City, Erling Haaland kwa muda mrefu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huenda akaelekea Uhispania, ikiamua kuhama. (Team Talk)
Klabu ya Aston Villa inataka kumsajili kiungo wa kati wa Wales Harry Wilson kwa uhamisho wa bure kutoka Fulham msimu huu wa joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia akidaiwa kunyantiwa na Everton. (Telegraph - usajili unahitajika)
Beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 27 na Argentina Cristian Romero na kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 26, ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka Spurs msimu huu wa joto ikiwa ikiwa klabu hiyo itashuka daraja. (Athletic- Usajili unahitajika)
Barcelona na Atletico Madrid zinapigana vikumbo kwa kiungo wa kimataifa wa Ureno Bernardo Silva, ambaye mkataba wake Manchester City unakalika msimu huu wa joto, huku klabu za Juventus na Monaco pia zikimuwania mchezaji huyo wa aliye na umri wa miaka 31. (Teamtalk)
Carlo Ancelotti ananuia kusaini mkataba wa miaka minne kama kocha wa Brazil. (Movistar kupitia AS - kwa Kihispania)
Mfungaji bora wa muda wote wa Ufaransa Olivier Giroud, ambaye sasa ana umri wa miaka 39, yuko kwenye njia panda kuhusiana na mustakabali wake katika klabu ya Lille ya Ufaransa. (L'Equipe - kwa Kifaransa - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Newcastle Muingereza Anthony Gordon, 24, anasema hataruhusu uvumi wa uhamisho umuathiri baada ya kuhusishwa na Liverpool na Arsenal. (Sun)
Kipa wa Manchester City Muingereza James Trafford, 23, angelipendelea kuhamia klabu ya Aston Villa badala ya Newcastle United msimu huu wa joto. (Football Insider)
LA Galaxy inafuatilia kwa karibu hali ya Philippe Coutinho huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye sasa ni mchezaji huru baada ya Vasco da Gama kukubali kusitisha mkataba wa kiungo huyo wa zamani wa Brazil. (AS - kwa Kihispania)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












