Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya: Vinicius Junior kutua EPL?
Manchester United, Manchester City, Chelsea na Arsenal wamefahamishwa kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa mshambuliaji wa Real Madrid, Mbrazil Vinicius Junior (25). (Teamtalk)
Manchester United wanaweza kumuuza kiungo Manuel Ugarte (24) majira ya kiangazi, huku Newcastle United, Aston Villa na Juventus zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka. (Caught Offside)
Liverpool wanafikiria kumtoa Mohamed Salah na kumchukua mshambuliaji wa Al Hilal, Marcus Leonardo (22) katika dili la kubadilishana wachezaji. (Give Me Sport)
Kiungo wa Aston Villa, Amadou Onana (24), anaweza kuondoka kwa dau kubwa, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa wanaomtaka. (Football Insider)
Beki wa Tottenham Hotspur, Luka Vuskovic (19), anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Hamburger SV, amesema anaweza kurejea White Hart Lane licha ya kusakwa na vilabu vikubwa Ulaya. (The Standard)
Chelsea wanaweza kumsajili kipa wa Sunderland, Robin Roefs (23), kuchukua nafasi ya Robert Sanchez. (Teamtalk)
Bayer Leverkusen wanataka kumbakiza mshambuliaji Yan Diomande (19) kwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, licha ya kusakwa na vilabu kadhaa. (Fabrizio Romano)