Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Spurs wanaongoza mbio za kumsajili Robertson
Tottenham inapigiwa upatu kumsajili beki wa Liverpool na Scotland Andy Robertson, 32, kama mchezaji huru msimu huu wa joto, na Spurs wataepuka kushuka daraja msimu huu. (Athletic - usajili unahitajika)
Chelsea huenda ikamuuza kiungo wa Argentina Enzo Fernandez msimu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akihusishwa na Real Madrid. (AS - kwa Kihispania)
Manchester City imefanya mazungumzo yasiyo rasmi na Sporting ili kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Morten Hjulmand, 26, ambaye pia ananyatiwa na Manchester United na Juventus. (A Bola - kwa Kireno)
Kiungo wa klabu ya Atalanta Ederson amekataa ombi la usajili kutoka kwa klabu kadhaa zikiwemo Arsenal, Manchester United na Newcastle huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, 26, akipania kuhamia Atletico Madrid. (AS - kwa Kihispania)
Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester United, Newcastle, Barcelona na Real Madrid zinahusishwa na mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi na AZ Alkmaar Kees Smit, 20. (Caughtoffside)
Klabu za Manchester United, Arsenal, Chelsea, na Paris St-Germain zinafikiria kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa na England Morgan Rogers, 23, 23. (Sky Sports).
Arsenal imefanya utafiti wa kina kuhusu hali ya winga wa Uingereza Anthony Gordon huko Newcastle na wanafuatilia upatikanaji wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Team talk)
Celtic iko tayari kumuuza winga wa Uswidi Benjamin Nygren, 24, msimu wa joto huku Tottenham ikitarajiwa kuanza mazungumzo kuusajili kwa takriban pauni milioni 26. Klabu za Brighton, Bournemouth na Valencia pia zimeonyesha nia kumnunua. (SportsBoom)
FC Cincinnati inatatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Brazil Neymar, 34, kutoka Santos hadi Ligi Kuu ya Soka huku majadiliano ya awali yakiwa tayari. (Athletic - usajili unahitajika)