Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumamosi: Newcastle United yamfuatilia Liam Delap
Mshambuliaji wa Chelsea Liam Delap anawindwa na Newcastle msimu huu wa joto huku ada ya takriban pauni milioni 40 ikitangazwa kwa Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 23. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Manchester United Kobbie Mainoo, 20, anatarajiwa kuongeza mkataba wake hadi mwaka 2031 na kuongeza mara nne mshahara wake Old Trafford hadi pauni 120,000 kwa wiki, pamoja. (Talksport)
Matumaini ya Liverpool ya kuishawishi Inter Milan kumuuza mlinzi wa kimataifa wa Italia Alessandro Bastoni, 26, yanafifia. (Teamtalk)
Tottenham wamemtazama mlinda lango wa Ujerumani Noah Atubolu, 23, huku nambari moja wa sasa Guglielmo Vicario akiangalia kurejea Italia akiwa na wachezaji wanaopigiwa upatu na Inter Milan. (Mail)
Kiernan Dewsbury-Hall wa Everton hauzwi kwa bei yoyote licha ya nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 27 kutoka Manchester United. (Teamtalk)
Kocha mkuu wa Newcastle United Eddie Howe anaelezea kwamba tetesi kuhusu kiungo wa Brazil Bruno Guimaraes kuwa anaweza kuhamia Manchester United ni dharau.(Sky Sports)
Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa wanaomuwania beki wa kushoto wa Fulham Antonee Robinson, 28, ambaye anaiwakilisha Marekani katika ngazi ya kimataifa. (Caught Offside)
Kocha wa Bournemouth Andoni Iraola ni mmoja wa wagombea wakuu wa kuwa kocha mpya wa Athletic Bilbao kufuatia uamuzi wa Ernesto Valverde wa kujiuzulu. (Marca)
Iraola pia amejadiliwa na Tottenham na Crystal Palace wakati wote wakitafuta meneja wakati wa kiangazi. (Mail)