Katibu mkuu wa CAF ajiuzulu baada ya mzozo kuhusu fainali ya Afcon
Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) amejiuzulu wakati wa kipindi cha mzozo barani Afrika.
Veron Mosengo-Omba alisema katika taarifa kwamba alikuwa akistaafu, lakini kuondoka kwake kunakuja wakati wa mzozo kuhusu maamuzi ya kuipokonya Senegal taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) la 2025 na kuahirisha mashindano ya wanawake dakika za mwisho.
Matukio haya yameiacha Caf, chombo kinachoongoza soka la Afrika, kikipambana na mgogoro wa kupoteza imani ya wapenzi wa soka.
Mosengo-Omba aligusia utata uliokuwa ukimkabili wakati wa uongozi wake katika taarifa yake siku ya Jumapili. "Sasa kwa kuwa nimeweza kuondoa tuhuma kwamba baadhi ya watu wamejitahidi sana kunishawishi, naweza kustaafu nikiwa na amani ya akili na bila vikwazo, na kuiacha CAF ikiwa na mafanikio zaidi kuliko hapo awali," Mosengo-Omba, naibu wa rais wa Caf Patrice Motsepe, aliandika.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 66 amekosolewa kwa kubaki kama Katibu Mkuu baada ya umri wa kustaafu wa lazima wa shirikisho hilo wa miaka 63.
Pia ameshutumiwa na baadhi ya wafanyakazi kwa kuunda mazingira mabovu mahali pa kazi, ingawa uchunguzi baada ya malalamiko ya wafanyakazi ulimsafisha kuwa hakuwa na makosa yoyote.
Mosengo-Omba, ambaye anatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini pia ana uraia wa Uswisi, aliteuliwa kuwa katibu mkuu mnamo Machi 2021.
Unaweza kusoma;