Kombe la Carabao: Kiwango 'kibovu' cha Arsenal chazua hofu, je, wamejichimbia shimo?

Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal wamepoteza 2-0 dhidi ya Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao, Nico O'Reilly akifunga mabao yote mawili na kumalizia matumaini ya timu ya Mikel Arteta ya kutwaa mataji manne msimu huu. Mechi hii ilikuwa ya matumiani mengi lakini mwisho wake ulikuwa wa kukatisha tamaa.

Mchezaji wa Arsenal, William Saliba, alionesha kuwa na hasira akipanda ngazi za Wembley kupokea medali yake. Picha za wachezaji wa Arsenal wakijitahidi kuikabiliana na hali hiyo ya kukasirika zilionyesha huzuni ya dhahiri. Arsenal wamezoea kuona Man City wakifurahia ushindi, lakini mchezo huu walitarajiwa kuanzisha furaha ya kuwa na wao wanashinda.

Ni jambo linalowaumiza Arsenal zaidi kutokana na jinsi walivyokuwa bora msimu huu wa Ligi Kuu ya Uingereza na hata ligi ya mabingwa Ulaya. Walikuwa wanatazamiwa kuwa na uwezo wa kushinda dhidi ya wachezaji bora wa City, lakini hali ilitofautiana kabisa baada ya mapumziko.

City walitawala kipindi cha pili, na arsenal kuonekana kama timu iliyojiokoteza mtaani. Ilionyesha moja ya viwango vibovu kabisa katika msimu huu hasa kwenye kipindi cha pili. Ni jambo ambalo limekuwa changamoto kwa Arsenal katika mechi kubwa, ikihitaji kujirekebisha haraka chini Arteta.

Makosa binafsi na kukosekana kwa ubora kulivuruga mipango

Bao la kwanza na hata la pili yalitokea kutokana na makosa binafsi ya wachezaji wa Arsenal. Timu hiyo ilishindwa kudhibiti mpira mwanzoni mwa kipindi cha pili, hali iliyowapa mabao ya harakaharaka na kuondoa matumaini ya kuibuka na ushindi.

Kukosekana kwa Eberechi Eze kutokana na jeraha, pamoja na Martin Odegaard, kuliacha nafasi za katikati ya uwanja kuwa yatima. Arsenal ilisalia na mabeki tu hasa wa kati walioonekana imara, lakini si Saka, Haverts, Rice, Zubimendi wote walipotea. walipoteza mipira na pasi kama watoto. miili yao kipindi cha pili ilizungumza wazi kwamba imechoka, imekata tamaa hasa. Arsenal walihitaji bao kuanzia dakika ya 60, lakini walikuwa na 37% tu ya umiliki wa mpira katika kipindi cha pili, hakukuonekana na matumiani yoyote.

Uwepo wa Kepa Arrizabalaga mlango, badala ya kipa wa kwanza David Raya, ulijitokeza kama tatizo la kiufundi la kwanza. Makosa ya kipa huyu yalionekana wazi katika bao la kwanza, ikionyesha hali ya wasiwasi kwa timu nzima.

Hali hii ya kushindwa kudhibiti mpira na kutengeneza nafasi ya mabao inatoa picha ya tatizo la muda mrefu kwa Arsenal, haswa wanapokabiliana na wapinzani wenye ubora wa juu kama City.

Lakini City pia walikuja tofauti kabisa wakitumia 4-2-4, mfumo ambao ulilenga Man city kukaba kuanzia juu na kuwafanya Arsenal wasianze kutengeneza mashambulizi kutoka nyuma, na wakijaribu kufanya hivyo basi wawape presha ya kufanya makosa na kuwaadhibu.

Arsenal nguvu yao huanza na mabeki wao. Rice alishindwa kucheza kwa sababu hiyo, Zubibendi akapotea na kupotea kwa hawa kukawapoteza kina Kai Havertz, Saka na kumfunika kabisa Viktor Gyökeres.

Je, nini hatma ya Arsenal msimu huu?

Hata baada ya kichapo kutoka kwa City, Arsenal bado wana nafasi ya kupata mafanikio msimu huu. Wanaongoza Ligi Kuu kwa alama tisa na wamepata mechi 'rahisi' katika robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting CP. Hata hivyo, aina ya uchezaji wao dhidi ya mpinzani kama City, inawaongezea shinikizo kubwa la kiakili.

Kupoteza mpira, kushindwa kumiliki mpira na kuanzisha na kuendesha mashambulizi kunawaacha Arsenal kwenye hali tete. Na sasa kuumia kwa Eberechi Eze na Martin Ødegaard kumeongeza matatizo zaidi.

Arteta alisisitiza kuwa timu yake lazima itumie kichapo ilichokipata kama motisha: "Tutatumia huzuni hii ili kuwa namiezi miwili ya kushangaza zaidi kwa pamoja," alisema kocha huyo.

Uamuzi wa Arsenal sasa uko wazi, kujifunza kutokana na makosa ya Wembley. Kama watacheza soka bovu kama walilolionyesha dhidi ya City, haitashangaza kama watakosa ubingwa hata mmoja msimu huu.