Wairani wanaambiwa nini kuhusu vita?

Ripoti za kwanza zilitokea kwenye vituo vya televisheni vya kigeni, mbali sana na kufikiwa na Wairani wengi. Tarehe 28 Februari, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa kuna ishara kwamba ''kiongozi mbabe hayuko hai tena'', akirejelea kifo cha Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei katika shambulio la pamoja la Marekani na Israel.
Hata hivyo, Wairani waliokuwa wakitazama televisheni ya serikali hawakusikia chochote kuhusu hilo.
Maafisa wa serikali hawakuthibitisha wala kukana ripoti za kifo cha Khamenei.
Kwenye moja ya vituo vya taifa vya Iran, ART3, mchambuzi wa habari aliwahimiza watazamaji "kumwamini" yeye na "taarifa za hivi karibuni" za serikali, akipuuza ripoti zinazozunguka kuhusu kifo cha Khamenei kama "tetesi zisizo na msingi," na kuongeza kuwa ukweli "utafahamika hivi karibuni."
Vyombo vya habari vya serikali vya Iran havikutoa habari za kifo cha Khamenei hadi asubuhi iliyofuata, saa kadhaa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza hadharani habari hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
Tangu kuibuka kwa vita, ambavyo ripoti zinasema viliua zaidi ya watu 1,200 nchini Iran na kuenea hadi Lebanon na nchi za Ghuba ya Kiarabu, vyombo vya habari vya serikali vya Iran vikionesha sehemu za ukweli lakini pia inaongeza maelezo au tafsiri ya mamlaka, wakitoa maelezo maalum ya matukio kwa hadhira yao ya ndani.
End of Unaweza kusoma
Ingawa mamilioni ya Wairani hufuatilia vituo vya satelaiti vya lugha ya Kipersia vinavyotangaza kutoka nje ya nchi, kupata taarifa huru bado ni changamoto.
Wakati wa machafuko na migogoro, kuzimwa kwa mtandao, udhibiti wa habari, na vizuizi vya vituo vinawaweka Wairani mbali na dunia ya nje.
BBC ilifuatilia jinsi vyombo vya habari vya serikali vya Iran vilivyofunika vita katika wiki yake ya kwanza na kugundua kuwa ripoti nyingi ziliangazia mateso ya raia, wito wa kulipiza kisasi dhidi ya kile kilichotajwa kama "maadui," na kuhimiza umma kuonesha uaminifu kwa Jamhuri ya Kiislamu, huku vituo vya kijeshi na serikali vilivyolengwa na Israel na Marekani vikipatiwa uangalizi mdogo.
Uchunguzi huo pia unaonesha mifano ya upotoshaji wa taarifa.
Mfumo wa vyombo vya habari vya Iran

Chanzo cha picha, IRTV
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kulingana na shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka, Reporters Without Borders, linalofuatilia uhuru wa vyombo vya habari duniani kote, Iran ipo miongoni mwa nchi ambazo zina vizuizi vikali zaidi vya uhuru wa vyombo vya habari.
Tangu mapinduzi ya mwaka 1979 yaliyosababisha kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, vyombo vya habari ndani ya nchi hiyo vimefanya kazi chini ya vizuizi vikali.
Vituo vingi vya habari vya Magharibi na vya lugha ya Kipersia, ikiwa ni pamoja na BBC Persian Service, pia vinazuiwa kuripoti kutoka ndani ya Iran.
Ingawa televisheni na redio ndizo jukwaa kuu la vyombo rasmi vya habari, shughuli zake pia zinaenea mtandaoni kupitia tovuti za habari na mitandao ya kijamii kama Instagram, Telegram, na X. Watumiaji ndani ya Iran mara nyingi wanahitaji kutumia Virtual Private Network (VPN) kufikia majukwaa haya.
Vituo vya habari vinavyosimamiwa na serikali vimekuwa chanzo kikuu cha taarifa kwa wananchi ndani ya nchi, hasa wakati mtandao unapozimwa.
Mahsa Alimardani, kutoka shirika la haki za binadamu Witness, amesema:
"Kuna hadithi inayosambazwa kwamba nchi inapata ushindi kamili na kwamba jeshi ni lenye nguvu sana."
Vyombo kadhaa vya habari vya serikali vya Iran viliripoti kwamba vikosi vya Iran ziliwaua au kujeruhi mamia ya wanajeshi wa Marekani, katika ripoti ambazo zilionesha zaidi kiwango cha vifo vya Marekani.
Tarehe 3 Machi, Tasnim News Agency, liliripoti kwamba wanajeshi 650 wa Marekani waliuawa katika siku mbili za mwanzo za vita, akirejelea msemaji wa Jeshi la Iran
Dhana hii baadaye ilichukuliwa na vyombo vya habari katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na India, Uturuki, na Nigeria.
Kinyume chake, Pentagon lilitangaza wakati huo vifo vya wanajeshi sita wa Marekani. Tarehe 13 Machi,Jeshi lithibitisha vifo vya wanajeshi wa Marekani saba zaidi.
Kupotosha ukweli

Teknolojia za kisasa pia zinachangia kurahisisha vyombo vya habari vya serikali kusambaza propaganda ya kisiasa.
Kwenye chapisho la Facebook ambalo baadaye lilifutwa, kituo cha habari cha serikali kilichotangaza kwa lugha ya Kiingereza, Press TV, kilichapisha video iliyoonesha jengo likiteketea moto huku moshi mzito ukipanda kutoka humo. Maandishi yaliyoambatana na video yalieleza:
"Moshi unapanda kutoka jengo refu nchini Bahrain kufuatia shambulio la Iran."
Hata hivyo, uchunguzi wa karibu wa video hiyo ulionesha maelezo yasiyo ya kawaida, kama vile magari mawili yakiungana kuwa moja, jambo linaloashiria kwamba video hiyo ilitengenezwa kwa kutumia akili bandia (AI).
Brett Schafer, mkurugenzi mkuu katika taasisi ya Strategic Dialogue, iliyoko Uingereza, amesema:
"Matumizi ya maudhui yaliyozalishwa na AI katika propaganda za vita si jambo jipya. Lakini ukweli kwamba vyombo vikubwa vya habari vya serikali vinatumia picha bandia kwa njia hii ni jambo la kushangaza, hata kama havijulikani kwa kufuata usahihi."
Anaongeza kwamba matumizi mara kwa mara ya picha za deepfake katika vyombo rasmi vya Iran yanaonesha kuwa imekuwa sehemu ya mtindo wa ufafanuzi wa habari za vita, si tukio la pekee.
Kama ilivyo kwa taarifa nyingi za upotoshaji zinazosambazwa mitandaoni kuhusu vita, bado haijulikani nani aliyetengeneza au aliye nyuma ya vifaa hivi.
Hata hivyo, tangu kuanza kwa vita, BBC imebaini mifano mingine ya picha zilizozalishwa na AI zilizotolewa na mashirika ya serikali ili kuunga mkono hadithi zao.
Kinyume chake, White House na Rais wa Marekani Donald Trump pia wamekuwa wakichapisha mara kwa mara picha au video zilizotengenezwa na AI zinazolenga propaganda na kuvitukuza vita.
Rais wa Israel Benjamin Netanyahu hivi karibuni alichapisha picha iliyozalishwa na AI kwenye Instagram ikimuonesha akiwa pamoja na Trump na Waziri Mkuu wa Uingereza wakati wa Vita Kuu vya Pili, Winston Churchill, katika sura ya kusherehekea. Kisha shirika moja la habari lilitoa chapisho hilo kwenye akaunti yake kupitia kipengele cha ushirikiano cha jukwaa hilo.
Ukweli uliojificha

Chanzo cha picha, Iranian Press Center/AFP via Getty Images
Rekodi ya Iran ya kusambaza taarifa zinazokanganya ukweli na madai yasiyo sahihi imechangia kuzidisha shaka miongoni mwa wakosoaji wengi wa serikali, ndani na nje ya nchi.
Wakati vyombo vya habari vya serikali vya Iran viliripoti tarehe 3 Machi kuwa zaidi ya watoto 160 na wafanyakazi waliuawa katika shambulio la anga lililolenga shule, tukio ambalo wataalamu huru wanaamini lilikuwa shambulio la Marekani lililolenga kambi ya kijeshi iliyo karibu, pia walichapisha picha ya anga ya mazishi ya watu wengi.
Wapinzani wa serikali walisema kwamba picha ya mazishi ilitengenezwa kwa kutumia akili mnemba (AI), lakini ukaguzi ulionesha kuwa ilikuwa halisi.
Ilikuwa ipo katika makaburi karibu km 3.7 kutoka shule, kwani miti, mpangilio wa barabara, na jengo jirani vililingana na kile kilichonekana kwenye picha za satelaiti.
Picha za satelaiti zilizopigwa siku baada ya mazishi zinaonesha makaburi mapya, wakati picha zilizopigwa siku kabla ya mazishi zinaonesha ardhi ikiwa tupu.
Mahsa Alimardani wa shirika Witness amesema:"Tunahitaji kushughulika na ukweli wa pande mbili kwa wakati mmoja."
Anaongeza: "Mamlaka za Iran mara nyingi hushughulika na kuficha ushahidi wanapokabiliwa na mashtaka ya ukiukaji, lakini wakati wa vita wanawekeza sana katika kuripoti vifo vya raia."
Anadai kuwa kurekodi huku, ingawa kunaweza kutumika kuunga mkono propaganda rasmi na hadithi ya serikali kuhusu vita, haukubaliani kuwa ni wa uongo.
Alimardani anaeleza kuwa kushughulika na ripoti kutoka vyombo rasmi vya habari vya Iran kunahitaji shaka yenye uhakika.













