Tetesi za soka Ulaya: Tonali kuzitosa Man Utd, Man City kwenda Italia

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City na Manchester United wanavutiwa na kiungo wa Newcastle, Sandro Tonali, 25, lakini mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan anapendelea kurejea nyumbani Italia (Talksport).
Ben White, mlinzi wa Arsenal mwenye umri wa 28 anaweza kuondoka msimu huu huku Everton wakionesha hamu ya kumsajili (FourFourTwo).
Aston Villa ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ligi kuu England zinazoangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain kutoka Senegal, Ibrahim Mbaye, mwenye umri wa 18, msimu huu (Sky Sports).
Manchester United wamemuweka nyota wa Fulham na Marekani, Antonee Robinson, mwenye umri wa 28, kwenye orodha yao ya mabeki wa kushoto wanaohitajika msimu huu (Football Insider).
West Ham na Nottingham Forest kukabiliwa na ushindani kutoka AC Milan kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Bologna kutoka Argentina, Santiago Castro, mwenye umri wa 21, msimu huu (Tuttomercatoweb).

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wako tayari kutumia hadi £86.5m (100m euros) kwa ajili ya kiungo wa Barcelona, Fermin Lopez, 22, lakini mchezaji huyo wa Hispania hajapenda kuondoka Camp Nou (El Chiringuito via Football Espana).
Mshambuliaji wa Paris St-Germain aliye kwa mkopo Tottenham, Randal Kolo Muani, mwenye umri wa 27, anataka kuhamia Juventus msimu huu (Gazzetta dello Sport).
Crystal Palace wanachunguza uwezekano wa kumpa mikoba ya umeneja, kocha wa Bournemouth, Andoni Iraola, ambaye anamaliza mkataba wake msimu huu, huku Manchester United pia wakionyesha nia wakati hatma yake Bournemouth ikiwa haijulikani (Telegraph & Mirror).
Wamiliki wa Chelsea watamuunga mkono kocha wa sasa Liam Rosenior hata kama klabu itashindwa kufuzu ligi ya mabingwa Ulaya (Mail+).
Cesc Fabregas, kocha wa Como, anaonekana kama mbadala wa Rosenior iwapo Chelsea wataamua kufanya mabadiliko ya kocha (Teamtalk).
Juventus wanaendelea kumfuatilia beki wa kati wa Real Madrid na Ujerumani, Antonio Rudiger, 33, ambaye atakuwa huru kujiunga na klabu nyingine msimu huu (Tuttosport).













