Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Real Madrid na Man United zampigania Bruno Guimaraes.

.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Bruno Guimareas
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wako kwenye mazungumzo ya kiwango cha juu kumsajili nahodha wa Newcastle United Bruno Guimaraes kwa takriban pauni milioni 69, lakini nia mpya kutoka kwa Real Madrid inatishia kutatiza uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 28. (Reuters)

Hatahivyo, Magpies wana nia ya kuendelea na Guimaraes na wanapanga mazungumzo kuhusu mkataba unaoweza kuweka rekodi mpya katika klabu hiyo. (TeamTalks)

Manchester United itakataa juhudi za Barcelona za kuongeza mkopo wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford, 28, kwa msimu mwingine, ikiambia klabu hiyo ya Uhispania kulipa £26m iliyokubaliwa hapo awali au kumrudisha fowadi huyo Old Trafford. (Mirror)

Real Madrid wako kwenye mazungumzo na beki wao wa miaka 33 wa Ujerumani Antonio Rudiger kuhusu mkataba mpya. (Marca)

Borussia Dortmund wana nia ya kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Uingereza Jadon Sancho. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliye kwa mkopo Aston Villa, mkataba wake na klabu mama wa Manchester United utakamilika mwezi Juni. (Athletic - Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mracus Rashford
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Youri Tielemans

Beki wa Tottenham Hotspur Cristian Romero amepuuzilia mbali uvumi unaomhusisha na uhamisho wa majira ya joto, huku Muargentina huyo, 27, akisema kujitolea kwake ni kuisaidia klabu hiyo kuepuka kushuka daraja. (Independent)

Wakati huohuo, mshambuliaji Randal Kolo Muani, ambaye yuko Tottenham kwa mkopo kutoka Paris St Germain, anahusishwa na uhamisho wa Juventus ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alicheza msimu uliopita. (Gazzetta dello Sport – In Italy)

Mshambulizi wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 33, bado hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake licha ya kutakiwa na Saudi Arabia, huku Al-Hilal wakiwa na imani kuwa wanaweza kumshawishi mkurugenzi wa michezo wa Reds Richard Hughes kujiunga nao. (Mail – Subscription Required)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 28, yuko tayari kukataa ofa zozote za kuondoka Aston Villa kwa kuwa amekuwa kwenye rada za vilabu kadhaa nchini Saudi Arabia. (Football Insider)

Manchester City wanazidi kuzoea uamuzi wa meneja Pep Guardiola anayeondoka mwishoni mwa msimu huu, huku wachezaji wakitathminiwa. (Football Insider)

Kipa wa Tottenham Guglielmo Vicario analengwa na Inter Milan na mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 29 anaaminika kuwa tayari kuhamia klabu hiyo ya Serie A. (Calciomercato -In Itali)

Kipa wa Brighton Carl Rushworth, aliye kwa mkopo katika klabu ya Coventry City, anavutia vilabu sita vya Ligi Kuu ya Uingereza huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 24 akitarajiwa kuamuru ada ya takriban £20m. (Sportsport)