Tetesi za Soka Ulaya: Arsenal yamtaka Goretzka wa Bayern

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal itakabiliwa na ushindani kutoka Juventus katika kusaini mkataba na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Leon Goretzka huku kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kuondoka Bayern Munich mkataba wake utakapoisha msimu huu wa joto. (Gazzetta dello Sport)
AC Milan wanamtazama mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland, Troy Parrott wakati wa kiangazi huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akiwa na thamani ya takriban pauni milioni 25 kutoka AZ Alkmaar. (Independent)
Brighton wana hamu ya kukamilisha mkataba na Cologne kwa winga wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 19 Said el Mala baada ya mchezaji huyo kubadilisha mawakala. (Bild)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City inaweza kumruhusu winga wa Brazil Savinho, 21, kuondoka msimu huu wa joto huku Tottenham ikitarajiwa kuwa miongoni mwa timu ambazo mchezaji huyo anaweza kucheza ikiwa watabaki katika Ligi Kuu England. (Football Insider)
Juventus inamtaka kiungo wa kati wa Manchester City, Mreno, Bernardo Silva, 31, baada ya kupunguza hamu yao ya kumsajili Sandro Tonali, 25, wa Newcastle, kwa sababu Manchester United na Arsenal zote zinamtaka kiungo huyo wa kati wa Italia. (Gazzetta dello Sport)
Fulham wamefikia makubaliano ya maneno ya kumsajili mshambuliaji wa Marekani, Ricardo Pepi mwenye umri wa miaka 23 kutoka PSV Eindhoven huku masharti binafsi pia yakikubaliwa. (Fabrizio Romano)
Richard Hughes wa Liverpool yuko kwenye orodha ya wachezaji watatu watakaowania kuwa mkurugenzi mpya wa michezo katika klabu ya Saudi Pro-League, Al-Hilal. (Telegraph)
Xabi Alonso atataka kumsajili beki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni, 26, kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton, 22, na winga wa Paris St-Germain, Bradley Barcola, 23, ikiwa atachukua nafasi ya Arne Slot huko Anfield msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United imewasiliana na Ajax ili kuchunguza masharti ya mkataba wa mshambuliaji raia wa Ubelgiji, Mika Godts, 20. (Sacha Tavolieri)
Real Madrid na Barcelona wako mbele ya vilabu vya Ligi Kuu England katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa AZ Alkmaar, Kees Smit, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Uholanzi kwa sababu anataka kuhamia Uhispania ili kuishi katika hali ya hewa ya jua kali. (AS)
Manchester United na Liverpool zote zinaongeza nia yao ya kumsajili kiungo wa kati wa Wolves na Ureno, Joao Gomes, 25. (Teamtalk)
Kocha wa Barcelona, Hansi Flick ataongeza mkataba wake hadi 2028 baada ya Joan Laporta kuchaguliwa tena kuwa rais wa klabu hiyo. (Florian Plettenberg)














