Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Marcus Rashford kusalia Barcelona kwa mkopo

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona itajaribu kumbakisha mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 28, kwa mkopo kwa msimu mwingine ili kuepuka kulipa ada ya uhamisho ya £26m. (Daily Mail)
United inaweza kumnunua kiungo wa kati wa Nigeria Wilfred Ndidi, 29, kutoka Besiktas, huku mlinda lango wa Uturuki Altay Bayindir, 27, akielekea upande mwingine. (SporX - In Turkish)
Borussia Dortmund wanaamini kuwa wanaweza kumshawishi Jadon Sancho, 25, wa United kusaini kwa mara ya tatu katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Times - Subscription Required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wana nia ya wazi ya kumnunua kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali lakini Newcastle United itadai ada ya zaidi ya £100m ikiwa wataamua kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (I)
Juventus wameambiwa wanaweza kumsajili Joshua Zirkzee kutoka Manchester United kwa kitita cha euro 25m (£21.6m) lakini pia wako tayari kufikiria kumtoa kwa mkopo na chaguo la kumnunua fowadi huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24. (Tuttosport - In Italy)
Kiungo wa kati wa Senegal Lamine Camara analengwa na Newcastle na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anaweza kuondoka Monaco msimu huu wa joto. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
The Magpies pia wana nia ya kumleta mlinda lango wa Ufaransa Robin Risser mwenye umri wa miaka 21 kutoka Lens. (Sky Sports Switzerland - In French)
West Ham wanapanga mazungumzo na Chelsea kubadilisha usajili wa mkopo wa beki wa Ufaransa Axel Disasi, 28, kuwa uhamisho wa kudumu. (Football Insider)
Chelsea na Tottenham wanamwinda mshambuliaji wa Hoffenheim mwenye umri wa miaka 23 wa Kosovo Fisnik Asllani. (Bild - In Germany}











