Trump aambia Uingereza na nchi nyingine 'nendeni mkachukue mafuta yenu wenyewe' huko Hormuz

Rais wa Marekani aambia mataifa ambayo sasa hayana uwezo wa kupata mafuta ya ndege "Marekani haitaweza kuwasaidia tena, kama vile ambavyo hamukuwepo tulipowahitaji".

Muhtasari

Moja kwa moja

Ambia Hirsi na Martha Saranga

  1. Athari za vita Iran zaongeza bei ya petroli duniani kote

    xcv

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tangu vita vilipoanza, bei ya pipa moja la mafuta ghafi imepanda kutoka dola 73 hadi takribani dola 117 kwa sasa.

    Kwa kawaida, kupanda kwa bei ya jumla ya nishati huonekana kwanza kwenye vituo vya mafuta, na hali hii inaonekana kote duniani.

    Nchini Marekani, wastani wa bei ya petroli umeongezeka kwa zaidi ya dola moja tangu kuanza kwa mgogoro huo, na kufikia zaidi ya dola 4 kwa mara ya kwanza katika karibu miaka minne.

    Nchini Uingereza, wastani wa bei ya petroli umeongezeka kwa asilimia 14, na dizeli kwa asilimia 27.

    Baadhi ya nchi, kama Sri Lanka na Bangladesh, zimeanza kuweka mgao wa mafuta, na wiki iliyopita Slovenia ilikuwa nchi ya kwanza katika Umoja wa Ulaya kufanya hivyo.

    Nchini Australia, kodi ya mafuta imepunguzwa kwa nusu kwa muda wa miezi mitatu ili kusaidia madereva kukabiliana na bei kubwa za mafuta, huku majimbo mawili yakitoa usafiri wa umma bure kwa muda ili kuwahamasisha watu wasitumie magari yao.

    Unaweza pia kusoma:

  2. Ukatili wa kingono sehemu ya “maisha ya kila siku” katika baadhi ya maeneo Sudan: MSF

    xcv

    Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

    Vitendo vya ubakaji na ukatili wa kingono bado ni “sehemu ya maisha ya kila siku” katika maeneo ya Sudan hata pale ambapo mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yamepungua, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kimataifa la madaktari wasio na mpaka Médecins Sans Frontières (MSF).

    Ripoti hiyo inaeleza kuwa ubakaji umekuwa “sifa kuu” ya mzozo huo, ambapo mashambulizi mengi hutekelezwa na wanaume wenye silaha na mara nyingi huambatana na ukatili mkubwa pamoja na udhalilishaji.

    Hata hivyo, MSF inasema kuwa ubakaji umeendelea kama sehemu ya maisha kwa siri katika jamii za eneo la magharibi la Darfur, hata katika maeneo ambayo hayapo tena katika mstari wa mbele wa mapigano.

    Ripoti hiyo ndiyo uchambuzi wa kina zaidi hadi sasa kuhusu ukatili wa kingono katika vita vya Sudan ambavyo vimekaribia kuingia mwaka wa tatu.

    Onyo:Habari hii ina maelezo ya ukatili wa kingono ambayo yanaweza kuwa ya kusikitisha kwa baadhi ya watu.

    Ripoti hiyo inabainisha ushuhuda wa waathirika 3,396 waliotafuta matibabu katika vituo vinavyoshirikiana na MSF katika eneo la Darfur Kaskazini na Kusini kati ya Januari 2024 na Novemba 2025.

    Pande zinazopigana jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) zote zinatuhumiwa kufanya ukatili wa kingono.

    Hata hivyo, Darfur ni ngome ya RSF, na idadi kubwa ya wahalifu waliotambuliwa na manusura walikuwa wapiganaji wa kundi hilo.

    Visa vingi vilivyotajwa katika ripoti hiyo vilitekelezwa katika eneo lenye migogoro mikali la Darfur Kaskazini mwaka uliopita, kufuatia RSF kuchukua udhibiti wa kambi za wakimbizi za Zamzam na Abu Shouk, pamoja na mji wa el-Fasher mwezi Oktoba ambapo MSF inaeleza hali hiyo kuwa “moja ya matukio ya kutisha zaidi, yenye ukatili usioelezeka”.

    Unaweza kusoma pia:

  3. Serikali ya Taliban yataka kuongeza uagizaji wa mafuta kutoka Urusi

    xcv

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maafisa kutoka wa Urusi wamesema kuwa serikali ya Taliban nchini Afghanistan imeomba kuongeza kiwango cha mafuta inachoagiza kutoka Urusi hadi tani milioni mbili kwa mwaka.

    Shirika la habari la serikali ya Afghanistan, Bakhtar News Agency, limemnukuu mkuu wa kituo cha biashara cha Urusi, Rustam Khabibulin, akisema: “Afghanistan imependekeza kununua tani milioni mbili za bidhaa za petroli kutoka Urusi kila mwaka kwa muda mrefu.”

    Afisa huyo wa Urusi alisema kuwa nusu ya makubaliano hayo ya biashara itakuwa gesi asilia iliyoyeyushwa (LNG), huku sehemu iliyobaki ikiwa ni petroli na dizeli.

    Mkuu huyo pia alieleza matumaini yake kuwa makubaliano hayo yatasainiwa na baadhi ya kampuni kubwa za Urusi.

    Kwa mujibu wa ripoti, mauzo ya mafuta kutoka Urusi kwenda Afghanistan yameongezeka kwa asilimia 20 katika mwaka uliopita.

    Aidha, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni ya Energostar Trading, nchi ya Belarus imesafirisha tani 400,000 za mafuta kwenda Afghanistan mwaka huu pekee.

  4. Meneja wa timu ya Ghana Addo, apigwa kalamu

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Ghana ilishindwa kufuzu Afcon 2025 chini ya uongozi wa Addo

    Ghana imefuta kazi meneja wa timu ya taifa hilo Otto Addo, siku 72 tu kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia.

    Kuondoka kwa Addo kunajiri baada ya timu ya Black Stars ya Ghana kushindwa 2-1 na Ujerumani katika mechi ya kirafiki mjini Stuttgart siku ya Jumatatu, na pia kupokea kichapo cha 5-1 na timu ya Austria mjini Vienna Ijumaa iliyopita.

    Timu ya Black Stars ambao wapo katika kundi moja na timu ya Uingereza, wamepoteza mechi nne walizocheza hivi karibuni, licha ya kuwa na winga wa Manchester City Antoine Semenyo na mshambuliaji wa Tottenham Mohammed Kudus, licha ya kuwa nao walishindwa kuhitimu katika mashindano ya kombe la Africa Afcon chini ya kocha Addo.

    Baada ya mechi ya Ujerumani, shirikisho la soka la Ghana lilisema kuwa "wameachana na Addo" na "ataondoka mara moja"

    Shirikisho hilo liliongeza kuwa "tutatoa taarifa kuhusu mwelekeo mpya utakaochukuliwa na timu ya Black Stars"

    Addo, mwenye umri wa miaka 50, alizaliwa nchini Ujerumani na alichezea taifa hilo. Akiwa kocha wa Ghana wameshinda vikombe 15 chini ya uongozi wake, na alikuwa ameanza muhula wake wa pili kama meneja kuanzia Machi 2024.

    Michuano ya kombe la dunia yatafanyika nchini Canada,Mexico na Marekani kuanzia tarehe 11 mwezi Juni hadi tarehe 19 mwezi Julai.

    Ghana itaanza na kuchuana na Panama tarehe 18 mwezi Juni kabla ya kukabiliana na Uingereza tarehe 23 mwezi Juni na kisha Croatia tarehe 27 mwezi huo.

    Pia unaweza kusoma:

  5. 'Nendeni mukachukue mafuta yenu wenyewe kutoka Mlango-Bahari wa Hormuz - Trump

    .

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi "kama Uingereza" ambazo haziwezi kupata mafuta ya ndege kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa kuhusiana na Mlango Bahari wa Hormuz zinapaswa "kuwa na ujasiri ambao umeshachelewa, kwenda kwenye Mlango Bahari, na KUCHUKUA tu".

    Katika ujumbe kwenye mtandao wa Truth Social, aliandika kwamba nchi "zitalazimika kuanza kujifunza jinsi ya kujipigania, Marekani haitakuwapo kuwasaidia tena, kama vile ambavyo hamkuwepo tulipowahitaji," akizungumzia nchi "ambazo zilikataa kushiriki katika vita vya Iran".

    "Kimsingi, Iran imeangamizwa kabisa. Sehemu ngumu imekamilika," ujumbe huo uliongeza, ukiishia na: "Nendeni mukachukue mafuta yanu mwenyewe!"

    Ufaransa 'haisaidii sana', Trump asema katika ujumbe uliofuata

    Katika ujumbe uliofuata alioutuma kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema Ufaransa "haikuruhusu ndege zinazoelekea Israel, zenye vifaa vya kijeshi, kupaa juu ya eneo la Ufaransa".

    Aliendelea kusema Ufaransa "imekuwa haina msaada wowote kwa 'Iran anayechinja watu,' ambayo imesambaratishwa!"

    Ujumbe huo unahitimishwa na rais wa Marekani akisema: "Marekani ITAKUMBUKA!!!"

    Soma zaidi:

  6. Fahamu mambo manne kuhusu vita vya Marekani, Israel dhidi ya Iran

    XCV

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mwanamume akibeba masanduku kutoka nyumba iliyoharibiwa kwa shambulio mjini Tehran siku ya Jumatatu

    Vita vitaisha lini?

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa vita kati ya Marekani, Israel dhidi ya Iran “vimevuka zaidi ya nusu ya safari,” ingawa baadaye alifafanua kuwa alimaanisha kwa upande wa operesheni za kijeshi, si muda halisi wa vita.

    Netanyahu aliongeza kuwa vita hivyo vimesababisha vifo vya “maelfu” ya wanajeshi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC), na kwamba Israel pamoja na Marekani wako “karibu kumaliza kabisa sekta ya silaha” ya Iran, ikiwa ni pamoja na kuharibu viwanda muhimu na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

    Mashambulizi yanaendelea katika ukanda wote

    Wakati huo huo, mashambulizi yanaendelea katika maeneo mbalimbali.

    Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema limeanzisha wimbi jipya la mashambulizi katika mji mkuu wa Iran, Tehran, saa chache baada ya kubaini makombora yaliyotumwa kutoka Iran kuelekea Israel.

    Mashambulizi pia yameripotiwa katika eneo la Ghuba, ikiwemo Dubai, ambako mamlaka zimesema meli ya mafuta iliteketea kwa moto kufuatia shambulio la ndege isiyokuwa na rubani kutoka Iran.

    Mpango wa Iran wa kutoza ushuru katika Mlango-Bahari wa Hormuz

    Kwa upande mwingine, Iran inapanga kuweka ushuru kwa meli zinazopita katika mlango wa Bahari wa Hormuz.

    Ripoti zinaeleza kuwa meli za Marekani na Israel, pamoja na zile za nchi zilizoshiriki kuiwekea Iran vikwazo, zitazuiwa kupita katika mlango huo muhimu wa bahari.

    Rubio asema njia hiyo 'itafunguliwa tena kwa namna moja au nyingine'

    Naye Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani, Marco Rubio, amesema kuwa mlango huo wa Hormuz “utaendelea kufunguliwa kwa njia moja au nyingine,” akisisitiza umuhimu wake kwa biashara ya kimataifa.

    Unaweza kusoma pia:

  7. Idadi ya vifo yaendelea kuongezeka kufuatia vita kati ya Marekani, Israel dhidi ya Iran

    XCV

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mazishi katika makaburi ya Behesht Zahra kusini mwa Tehran tarehe 26 Machi.

    Tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani, Israel dhidi ya Iran tarehe 28 Februari, idadi ya vifo imeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati.

    Iran:Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Iran la Human Rights Activists in Iran (HRANA) linaripoti kuwa watu 3,492 wameuawa tangu vita vianze. Kati yao, raia ni 1,574, wakiwemo takriban watoto 236.

    Israel: Shirika la huduma ya dharura la Magen David Adom (MDA) linasema watu 19 wamefariki kutokana na mashambulizi ya makombora tangu vita kuanza. Aidha, wanajeshi tisa wa Israel wanaripotiwa kuuawa nchini Lebanon, kwa mujibu wa jeshi la Israel.

    Lebanon: Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu 1,247 wameuawa, wakiwemo watoto 124.

    Nchi za Ghuba: Kwa ujumla, watu wasiopungua 24 wamefariki katika nchi za Ghuba. Wengi wao ni maafisa wa usalama au wafanyakazi wa kigeni.

    • Umoja wa Falme za Kiarabu: vifo 11
    • Kuwait: vifo 7
    • Oman, Saudi Arabia na Bahrain: kila moja imeripoti vifo 2

    Hali inaendelea kuwa tete huku idadi ya waliopoteza maisha ikiongezeka kila siku kutokana na mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.

    Unaweza pia kusoma:

  8. Kamanda mstaafu wa jeshi asema matumizi ya nguvu hayataleta suluhisho Hormuz

    xcv

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kamanda mstaafu wa jeshi la wanamaji, Tom Sharpe, amesema anaamini kuwa Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni mojawapo ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta, hauwezi kufunguliwa kwa kutumia nguvu kama ambavyo Marekani imetishia kufanya.

    Akizungumza na kipindi cha Today cha BBC Radio 4, Sharpe amesema kuwa Kama Iran haitakubali kuacha kushambulia boti zinazopita hapo, basi kutumia nguvu kupambana nao hakutafanikiwa.

    “Iran ina udhibiti wa hali hii, hilo liko wazi, na naamini wataendelea kuwa nao hata katika siku zijazo,” amesema Sharpe, akiongeza kuwa si kwa manufaa yao kubadili msimamo huo kwa sasa.

    Amesema pia kuwa hatma ya hali hiyo inategemea uamuzi wa Iran katika wiki au miezi ijayo.

    Unaweza kusoma pia:

  9. Siku ya 32 bila mtandao Iran, mawasiliano yashuka hadi 1%

    xcv

    Chanzo cha picha, Netblocks

    Iran imeingia siku ya 32 tangu kukatika kwa mtandao, huku watumiaji wengi wakikosa mawasiliano nje ya mtandao kwa zaidi ya saa 744, kwa mujibu wa taasisi ya ufuatiliaji wa mtandao, NetBlocks.

    Inaelezwa kuwa kiwango cha mawasiliano ya intaneti na mataifa ya nje kimesalia kwenye asilimia 1 tu ya hali ya kawaida.

    Hata hivyo, baadhi ya maafisa wa serikali, watumiaji wanaoiunga mkono serikali pamoja na baadhi ya waandishi wa habari bado wana uwezo wa kutumia mtandao bila vikwazo, wakati wengine wakilazimika kulipa fedha nyingi ili kuweza kupata huduma hiyo.

    Watu wachache wamefanikiwa kuunganisha mtandao kwa kutumia huduma za intaneti ya satelaiti kama Starlink na njia nyingine, lakini gharama zake ni kubwa.

    Nchini Iran, kutumia au kumiliki huduma ya Starlink kunaweza kusababisha kifungo cha hadi miaka miwili gerezani, huku mamlaka zikiongeza juhudi za kukabiliana na matumizi yake.

    Unaweza kusoma pia:

  10. Shirika la ndege la Korea mbioni kudhibiti athari ya kupanda kwa bei ya mafuta

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Shirika la ndege la Korea Kusini, Korea linasema kuwa linachukua hatua za dharura kukabiliana na athari za kupanda kwa bei ya mafuta ya ndege na kuzorota kwa uchumi kutokan na vita vya Iran.

    Makamu mwenyekiti wa shirika hilo la ndege Woo Ki-hong aliwaambia wafanyakazi katika nyaraka zililozoonekana na BBC kwamba bei ya nishati imeongezeka zaidi ya mara mbili ya ile iliyowekwa kwenye mpango wa biashara wa shirika hilo, na kusababisha "kuongezeka kwa gharama ya mafuta ya kila mwezi".

    Shirika litachukua "hatua za kupunguza gharama" kuanzia mwezi Aprili ili kuimarisha utendakazi wa shirika hilo, msemaji wa Korea Air alisema Jumanne.

    Bei ya mafuta ya ndege ilipanda hadi takribani dola 200 (£151.45) kwa pipa tarehe 20 Machi, zaidi ya mara mbili ya ilivyokuwa mwezi Februari, kulingana na takwimu za hivi punde za Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga.

    Mafuta ghafi yanauzwa kwa zaidi ya 50% ya juu kuliko kabla ya vita kuanza, na kufanya bei ya mafuta ya ndege kuongezeka.

    Maelezo zaidi:

  11. Habari za hivi punde, Wanajeshi wanne wa Israel wauawa kusini mwa Lebanon

    Moshi umeonekana ukifuka baada ya shambulio la Israel kusini mwa Lebanon, huku uhasama ukiongezeka kati ya Israel na Hezbollah.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wanajeshi wanne wa Israel waliuawa na wawili kujeruhiwa siku ya Jumatatu, katika taarifa mpya iliyochapishwa katika mtandao wa Telegram.

    Kulingana na taarifa hiyo, Kapteni Noam Madmoni, 22, sajenti Ben Cohen, 21, sajenti Maxsim Entis, 22, waliuawa wakati wa mapigano kusini mwa Lebanon.

    Maafisa wawili pia wamepelekwa hospitalini - askari mmoja alitajwa kama "aliyejeruhiwa vibaya", na mwengine kwa kiasi".

    IDF inaongeza kuwa askari wa nne aliuawa katika tukio hilo hilo, lakini jina lake bado halijatumbuliwa ili kuchapishwa.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Israel yapitisha sheria inayotoa adhabu ya kifo kwa Wapalestina watakaofanya mauaji dhidi ya Waisraeli

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Bunge la Israel limepitisha sheria mpya inayotoa adhabu ya kifo kwa Wapalestina watakaopatikana na hatia ya mashambulizi ya mauaji dhidi ya Waisrael.

    Sheria hiyo ilipitishwa kwa kura 62 dhidi ya 48, huku mbunge mmoja akijizuia kupiga kura na wengine kutohudhuria kikao hicho. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alihudhuria binafsi kupiga kura kuunga mkono muswada huo bungeni.

    Muswada huo wa sheria uliwasilishwa na Waziri wa Usalama wa Taifa Itamar Ben Gvir, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wenye msimamo mkali nchini humo.

    Hatua hiyo imeibua mjadala mkubwa kimataifa, huku mataifa ya Umoja wa Ulaya na mashirika ya haki za binadamu yakielezea wasiwasi mkubwa.

    Muda mfupi baada ya kupitishwa, kundi la haki za binadamu la Israel lilisema limewasilisha malalamiko katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo.

    Mamlaka ya Palestina ilitaja muswada huo “uhalifu wa kivita dhidi ya watu wa Palestina”, ikisema kuwa unakiuka Mkataba wa Geneva, Hata hivyo marekani imesema kwamba Israel in haki ya kutungu sheria zake huku nchi zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uingereza zikielezea wasiwasi mkubwa kuhusu muswada huo.

  13. Trump yuko tayari kusitisha mapigano hata kama Mlango -Bahari wa Hormuz umefungwa- Ripoti

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jarida la Wall Street Journal linaripoti kuwa Rais wa Marekano Donald Trump amewaambia wasaidizi wake kuwa yuko tayari kusitisha operesheni ya kijeshi dhidi ya Iran hata kama Mlango wa bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa.

    Likiwanukuu maafisa wa utawala, jarida hilo linaripoti kuwa Trump na wasaidizi wake walihofia kwamba wazo la kutumia nguvu kufungua njia kuu ya baharini litarefusha mzozo huo zaidi ya muda wake wa wiki nne hadi sita.

    Badala yake, anaripotiwa kufikiria kukomesha mapigano ya sasa, akiwa ameharibu pakubwa jeshi la wanamaji la Iran na hifadhi ya makombora, na ataendelea kuishinikiza Iran kidiplomasia kufungua tena mkondo huo wa biashara.

    BBC imewasiliana na Ikulu ya White House kwa maoni.

    Soma pia:

  14. Celine Dion atangaza kurudi katika muziki

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Celine Dion

    Céline Dion ametangaza kurejea jukwaani, ikiwa ni miaka minne baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa usiotibika ambao uliathiri sauti yake na uwezo wake wa kutembea.

    Nyota huyo, anayejulikana kwa nyimbo kama vile My Heart Will Go On na Because You Loved Me, ataimba kwa siku 10 katika ukumbi wa Paris La Défense Arena mbele ya mashabiki 40,000 mnamo Septemba na Oktoba.

    Tangazo hilo lilikuja siku ya 58 kusherehekea kuzaliwa kwake. Katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram, Dion alitaja kurudi kwake kama "zawadi bora zaidi ya maisha yangu". "Niko tayari kufanya hivi," aliwaambia mashabiki. "Ninajisikia vizuri, nina nguvu, ninahisi msisimko, ni wazi, [na] bila shaka, wasiwasi kidogo."

    Akizungumzia hali yake ya kiafya, Dion alisema: "Ninaendelea vizuri, ninasimamia afya yangu, ninahisi vizuri. Ninaimba tena, hata kucheza dansi kidogo. "Lakini sina budi kukuambia jambo muhimu sana: Katika miaka hii michache iliyopita, kila siku ambayo imepita, nilihisi maombi na msaada wako, fadhila na upendo wako. Aliendelea: "Ninawashukuru ninyi nyote. Siwezi kusubiri kuwaona tena."

    Pia unaweza kusoma:

  15. Mpango wa Iran kutoza ushuru meli kupita Mlango - Bahari wa Hormuz waidhinishwa

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kamati ya bunge nchini Iran imeidhinisha mipango ya kutoza ushuru meli zinazopita Mlango-Bahari wa Hormuz, kwa mujibu wa shirika la habari la Fars linaloshirikiana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

    Imeripoti kuwa mjumbe wa tume ya usalama wa taifa amethibitisha kuidhinishwa kwa mpango huo, ambao pia utazifanya meli za Marekani na Israel zikizuiliwa kupita katika mkondo huo wa bahari.

    Inaongeza kuwa, chini ya mpango huo, nchi nyingine ambazo zimeshiriki katika vikwazo dhidi ya Iran pia zitazuiliwa.

    Shirika la habari la AFP liliripoti kuwa mfumo huo mpya wa ushuru ulitangazwa kwenye televisheni ya taifa ya Iran, ambayo ilisema Iran itautekeleza kwa ushirikiano na Oman.

    Takribani asilimia 20 ya mafuta ghafi duniani husafirishwa kupitia njia muhimu ya meli ambayo iko kati ya Iran na Oman.

    Hata hivyo, tangu vita kuanza, njia za kuvuka mipaka zimeshuka kwa karibu asilimia 95, kulingana na kampuni ya ujasusi ya baharini ya Kpler.

    Soma pia:

  16. ‘Wakati wa kuyaondoa majeshi ya Marekani umefika’ - waziri wa mambo ya nje wa Iran aiambia Saudi Arabia

    Abbas Araghchi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Abbas Araghchi

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ameiambia Saudi Arabia kuwa ni "wakati umefika wa kuyaondoa majeshi ya Marekani’’ nchini mwao.

    Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Araghchi anasema Iran "inaiheshimu" Saudi Arabia na inaiona kama "taifa ndugu".

    Operesheni za Iran zinalenga "wachokozi wa maadui ambao hawana hawawaeshimu Waarabu au Wairan", anasema.

    Araghchi alichapisha maoni yake pamoja na picha inayoonekana kuonyesha ndege iliyoharibiwa na iliyo na alama za Jeshi la Anga la Marekani. "Angalia tu kile tulichofanya dhidi ya kamandi yao ya anga," anaandika.

    Kamandi Kuu ya Marekani bado haijatoa kauli yoyotehadharani kuhusu tukio hilo. BBC imewasiliana na wahusika kupata maoni.

    Maelezo zaidi:

  17. Sitaki 'kuweka ratiba’ vita vya Iran vitaisha lini - Netanyahu

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa zaidi ya nusu ya malengo ya kijeshi dhidi ya Iran tayari yamefikiwa, lakini hakutaka “kuweka muda maalum” wa lini vita hivyo vitamalizika.

    Netanyahu anasema vita "bila shaka nusu ya vita imepita" na jamhuri ya Kiislamu ya Iran hatimaye "itaanguka," shirika la habari la AFP linaripoti.

    Kiongozi huyo wa Israel pia amesema kuwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanaendelea kudhoofisha uongozi wa Iran.

    Wakati huo huo Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa limetambua makombora yaliyorushwa kutoka Iran kuelekea Israel, na kwamba mifumo ya ulinzi wa anga kwa sasa inafanya kazi "kuzuia tishio".

    Tahadhari imetolewa kwa umma, kuwasahauri watu kuelekea maeneo salama ya " kujikinga dhidi ya makombora" na kusalia hapo hadi ilani nyingine itakapotolewa.

    Unaweza kusoma pia:

  18. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja.

Trending Now