Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Qatar yataka Iran ikomeshe mashambulizi dhidi ya viwanda vya nishati

Iran ililipiza kisasi kwa kushambulia kiwanda cha nishati huko Qatar, na kusababisha "uharibifu mkubwa" pamoja na bei ya mafuta kupanda.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu & Asha Juma

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo ya leo. Kwaheri

  2. Chad yaonya Sudan kwamba italipiza kisasi baada ya shambulizi la ndege zisizo na rubani

    Rais wa Chad ameamuru jeshi kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya siku zijazo kutoka Sudan kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani lililoua watu wasiopungua 17 na kuwajeruhi watu wengine kadhaa waliohudhuria mazishi.

    Akiwa amevaa sare za kijeshi, Rais Idris Mahamat Déby aliitisha mkutano wa dharura wa usalama Jumatano jioni, ambapo aliamuru jeshi kuwa macho. Pia aliamuru "kufungwa kabisa" kwa mpaka na Sudan.

    Alielezea shambulizi lililolenga mji wa Tiné ulioko mpakani kama "la kuchukiza na la waziwazi" dhidi ya uadilifu wa eneo la Chad.

    Alisema kwamba imetokea licha ya onyo kwa pande hizo mbili zinazopigana nchini Sudan na kufungwa kwa mpaka hapo awali.

    Soma zaidi:

  3. Hegseth anasema dunia inapaswa kumshukuru Trump

    Waziri wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth leo ametoa taarifa mpya kuhusu vita vita Marekani na Israel dhidi ya Iran.

    amesema mashambulizi ya makombora ya Iran na ndege zisizo na rubani za upande mmoja dhidi ya vikosi vya Marekani "yamepungua kwa 90% tangu kuanza kwa mzozo".

    Amesema "kitu cha mwisho mtu yeyote duniani anataka hivi sasa" ni kiongozi mkuu ndani ya jeshi la Iran, kuiita "kazi za muda".

    Aliendelea kusema, Marekani imeharibu au kuzamisha takriban meli 120 za majini za Iran, huku zilizoachwa "zikiwa hazina umuhimu tena" na manowari yao "yamelipuliwa".

    "Utawala kama huo, unaokataa kuachana na matarajio yake ya nyuklia, si tatizo la kikanda tu, ni tishio la moja kwa moja kwa Marekani, uhuru na ustaarabu," Hegseth amesema kuhusu Iran.

    Pia alisema "dunia, Mashariki ya Kati, washirika wetu wasio na shukrani barani Ulaya, na hata sehemu za vyombo vyetu vya habari vinapaswa kusema jambo moja tu kwa Rais Trump - 'asante'".

    Uwezo wetu unaendelea kuimarika, Iran inaendelea kudhoofika

    Akilinganisha utawala wa Iran na Hamas huko Gaza, Hegseth alisema Iran imemwaga pesa kwenye handaki, roketi, makombora na ndege zisizo na rubani.

    Lakini, amesema, Marekani inawawinda kikatili na kwa nguvu nyingi, kama hakuna jeshi lingine lolote duniani linaloweza kufanya hivyo".

    Marekani imeshambulia zaidi ya maeneo lengwa 7,000 nchini Iran hadi sasa, na akaongeza kuwa Alhamisi kutakuwa na shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea, "kama jana".

    Uwezo wetu unaendelea kuimarika, Iran inaendelea kudhoofika," alisema, akiongeza kuwa ulinzi wa anga wa Iran "umesambaratishwa".

    Soma zaidi:

  4. Iran yaapa 'kuharibu kabisa' miundombinu ya nishati ya Ghuba ikiwa itaendelea kushambuliwa

    Iran imeapa kushambulia miundombinu ya nishati ya washirika wa Marekani na Israeli katika eneo la Ghuba hadi "itakapoharibiwa kabisa" ikiwa vituo vyake vya nishati vitalengwa zaidi.

    Iran imeanzisha wimbi la mashambulizi dhidi ya maeneo ya gesi na mafuta katika eneo lote la Ghuba baada ya vituo vyake vilivyounganishwa na maeneo ya gesi ya South Pars kushambuliwa na Israeli.

    "Tunawaonya adui kwamba mlifanya kosa kubwa kwa kushambulia miundombinu ya nishati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," amesema msemaji wa amri kuu ya kijeshi ya Iran, kulingana na shirika la habari la Fars linaloshirikiana na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

    "Ikiwa hili litarudiwa, mashambulizi ya baadaye kwenye miundombinu ya nishati yako na ya washirika wako hayatasimama hadi iharibiwe kabisa, ilisema, akiongeza kuwa Iran itajibu "vikali" kuliko mashambulizi ambayo yamefanyika kufikia sasa."

    Soma zaidi:

  5. Marekani 'italipua' viwanda vya gesi vya Iran ikiwa itaishambulia tena Qatar - Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kulipua kiwanda kikubwa cha gesi nchini Iran ikiwa itashambulia tena mshirika wa Marekani wa Kiarabu wa Ghuba, Qatar.

    Tishio la Trump linawadia siku moja baada ya Israeli kushambulia kiwanda cha South Pars cha Iran - sehemu kubwa zaidi ya uzalishaji gesi asilia duniani.

    Iran ililipiza kisasi kwa kushambulia kiwanda cha nishati huko Qatar, na kusababisha "uharibifu mkubwa" pamoja na bei ya mafuta kupanda.

    Ingawa Israel haijathibitisha rasmi shambulizi lake kwenye kituo cha gesi, rais wa Marekani alisema Marekani "haijui chochote" kuhusu mshirika wake, ambaye "alikuwa ameishambulia vikali" Iran "kwa hasira kwa kile kilichotokea Mashariki ya Kati".

    Mgogoro katika eneo hilo unaendelea baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Iran mnamo tarehe 28 Februari.

    Soma zaidi:

  6. DR Congo na Rwanda zakubaliana kupunguza mvutano

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda zimekubaliana kuchukua hatua madhubuti kupunguza mvutano na kuendeleza makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja.

    Taarifa ya pamoja kutoka DR Congo, Rwanda na Marekani inasema "wamekubaliana mfululizo wa hatua za kuchukuliwa ili kupunguza mvutano na kusonga mbele".

    Hatua hizo ni pamoja na “ahadi ya pande zote kuheshimu mamlaka na mipaka ya kila mmoja, ratiba ya kuondoa majeshi au kupunguza hatua za ulinzi za Rwanda katika maeneo maalum ndani ya DRC, juhudi za haraka na zenye muda maalum za DRC kusambaratisha kundi la FDLR, na ulinzi wa raia wote.”

    Mapigano katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa DRC, ambapo kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda linadhibiti miji muhimu, yameendelea licha ya nchi hizo mbili kusaini makubaliano ya amani mwaka jana chini ya Rais wa Marekani, Donald Trump.

    Maelfu ya wanajeshi wa Rwanda wamepelekwa mashariki mwa DRC, “ambapo wanashiriki moja kwa moja katika mapigano na kusaidia udhibiti wa M23 wa maeneo,” alisema Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, tarehe 2 Machi.

    Ahadi hii mpya inakuja siku chache baada ya Marekani kuongeza shinikizo kwa Rwanda kuhusu mzozo huo, kwa kuiwekea vikwazo jeshi lake na kuweka vizuizi vya visa kwa baadhi ya maafisa wakuu.

    Rwanda na Congo zilisaini makubaliano ya amani mjini Washington mwezi Desemba kama sehemu ya juhudi za Rais Donald Trump za kuleta amani na kuvutia uwekezaji wa mabilioni ya dola kutoka Magharibi.

    Hata hivyo, siku chache baada ya tukio hilo, waasi wa M23 waliingia katika mji wa mashariki mwa Congo eneo la Uvira, karibu na mpaka wa Burundi, katika hatua kubwa zaidi ya kuongezeka kwa mapigano katika miezi kadhaa.

    Baadaye walijiondoa kufuatia shinikizo la Marekani. Hata hivyo, Washington ilisema mwezi huu kuwa uwepo wa waasi hao karibu na mpaka wa Burundi “una hatari ya kugeuza mzozo huo kuwa vita pana ya kikanda.”

    Marekani imeilaumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la M23, hali inayochangia kuendelea kwa vurugu mashariki mwa Congo.

    Kwa upande wake, Rwanda ilisema vikwazo vya Marekani “vinalenga upande mmoja tu kwa njia isiyo ya haki,” na kuishutumu DRC kwa kukiuka makubaliano ya amani kupitia “mashambulizi ya kiholela ya droni na operesheni za ardhini.”

    Rwanda imekanusha kuunga mkono M23 na kwa muda mrefu imekuwa ikiishinikiza serikali ya Kinshasa kuchukua hatua dhidi ya FDLR, kundi la wapiganaji wa Kihutu wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

    Kundi la M23 lilifanya mashambulizi ya ghafla mashariki mwa Congo Januari 2025 na bado linadhibiti maeneo makubwa.

    Kundi la FDLR lilianzishwa na Wahutu waliokimbia Rwanda baada ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyosababisha vifo vya karibu watu milioni moja wa kabila la Watutsi na Wahutu wa wastani. M23 inasema inapigania kulinda jamii za Watutsi mashariki mwa Congo.

    Soma zaidi:

  7. Sultani wa Oman alaani mashambulizi dhidi ya maeneo ya nishati ya Ghuba

    Usultani wa Oman imelaani mashambulizi ya Iran dhidi ya maeneo ya nishati huko Qatar, UAE na Saudi Arabia, kulingana na shirika la habari la serikali la nchi hiyo.

    "Oman inathibitisha umuhimu wa kuzingatia sheria na kanuni za kimataifa, kujiepusha na kushambulia katika vituo vya kiraia na usambazaji wa nishati duniani," ameandika katika chapisho kwenye mtandao wa X.

    Hili linatokea baada ya Iran kushambulia kituo cha nishati cha Ras Laffan cha Qatar siku ya Jumatano.

    Kituo cha gesi cha Habshan cha UAE na uwanja wa Bab pia vimelazimika kufungwa, huku Saudi Arabia ikiripoti kuzuia mashambulizi mashariki mwa nchi na katika mji mkuu, Riyadh.

    Soma zaidi:

  8. Kiwanda cha pili cha kusafisha mafuta Kuwait chashambuliwa

    Kiwanda cha pili cha kusafisha mafuta nchini Kuwait kimelengwa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani, kulingana na Shirika la Habari la Kuwait linaloendeshwa na serikali.

    Inasema ndege isiyo na rubani ilishambulia sehemu ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Mina Abdullah, kusini mwa Jiji la Kuwait, na kusababisha moto kuzuka katika eneo hilo.

    Inafuatia shambulizi lililoripotiwa kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta cha Mina Al-Ahmadi, maili chache tu barabarani, ambalo lilisababisha "moto mdogo" ambao umezimwa.

    Awali, moto ulizuka katika kiwanda cha kusafisha mafuta huko Kuwait baada ya kushambuliwa na ndege zisizo na rubani, kulingana na Shirika la Habari la Kuwait (KUNA) na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

    Shirika la Petroli la Kuwait linasema hakukuwa na majeruhi katika kiwanda cha kusafishia mafuta cha Mina Al-Ahmadi na "moto mdogo" umezuiwa, KUNA inaripoti.

    Soma zaidi:

  9. Afcon: Senegal yataka Caf kuchunguzwa

    Serikali ya Senegal imetoa wito wa, ‘kuchunguzwa kwa washukiwa wa ufisadi ndani ya bodi zinazoongozwa na CAF,’ kufuatia uamuzi wa mshtuko wa kuivua nchi hiyo taji la kombe la mataifa ya Afrika kwa kupendelea Morocco.

    Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Soka barani Afrika ilibatilisha ushindi wa 1-0 wa Senegal katika muda wa ziada katika mchezo ambao uliokumbwa na mgogoro katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah huko Rabat.

    Uamuzi huo unakuja miezi miwili baada ya fainali na tayari umezua hisia kali katika ulimwengu wa soka.

    Raia wa Morocco walisherehekea uamuzi huo, huku wengi nchini Senegal wakijibu kwa mshtuko na kutoamini.

    Serikali ya Senegal imeutaja uamuzi huo kuwa ‘kinyume cha sheria na usio wa haki kabisa.’

    Mkuu wa zamani wa kamati ya nidhamu ya CAF hata alielezea uamuzi huo kuwa sarakasi ambayo soka la Afrika halihitaji.

  10. Qatar yasema Iran imevuka 'mpaka' kwa 'uchokozi wa kishenzi'

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ilitoa taarifa ikilaani Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa "masharti makali" kwa mashambulizi ya Iran kwenye vituo vya nishati nchini humo, na kuyataja mashambulizi hayo kuwa "ukiukaji wa wazi wa kanuni za sheria za kimataifa" na "tishio kubwa" kwa usalama wa mafuta duniani.

    Taarifa ya wizara hiyo iliendelea kwa kusema kwamba "uchokozi wa kinyama" wa Iran dhidi ya nchi jirani "umevuka mipaka yote" na kusisitiza haja ya kupunguza mivutano katika eneo ili "kurejesha usalama na utulivu wa kieneo na kimataifa."

    Hapo awali, iliripotiwa kuwa Iran ilifanya uharibifu mkubwa kwenye kituo cha mafuta cha Ras Laffan cha Qatar katika shambulio la kombora la Iran.

  11. Mkuu wa Ujasusi Marekani asema utawala wa Iran 'upo thabiti' lakini 'umedhoofishwa

    Afisa wa ngazi ya juu wa ujasusi nchini Marekani amesema siku ya Jumatano kwamba utawala wa Iran 'haujatatizika lakini umedhoofishwa kwa kiasi kikubwa' .

    Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa Tulsi Gabbard na maafisa wengine wakuu wa utawala wa Trump walitoa ushahidi kwenye kikao cha bunge kwa zaidi ya saa mbili kuhusu vitisho vya kimataifa kwa Marekani.

    Ilikuwa ni mkutano wa kwanza kwa umma kuhusu ujasusi tangu vita hivyo vilipoanza mwishoni mwa Februari na ilikuja siku moja baada ya kiongozi mkuu wa kukabiliana na ugaidi kujiuzulu akisema Iran haikuwa tishio kwa Marekani.

    Gabbard, ambaye anaratibu shughuli za kijasusi nchini humo, pia alisema kuwa Marekani ilitarajia kutokea matatizo katika Mlango wa bahari wa Hormuz, kituo muhimu cha meli.

    "IC [jumuiya ya kijasusi] inatathmini utawala nchini Iran unaonekana kuwa sawa, lakini kwa kiasi kikubwa umedhoofishwa kutokana na mashambulizi dhidi ya uwezo wake wa uongozi na kijeshi," alisema.

    Akindman pamoja na wakuu wa CIA, FBI, Shirika la Usalama wa Taifa na Shirika la Ujasusi la Ulinzi, Gabbard alikataa kujibu alipoulizwa mara kwa mara na Seneta Jon Ossoff, Mwanademokrasia, kuhusu kama aliiona Iran kama tishio lililokaribia.

    "Mtu pekee anayeweza kubaini ni nini tishio ni nini na sio hatari ni rais," alisema.

  12. Afisa wa zamani wa Trump ashutumu mauji ya Ali Khamenei

    Joe Kent, afisa mkuu wa Trump wa kukabiliana na ugaidi ambaye alijiuzulu wiki hii kutokana na upinzani wake kwa vita nchini Iran, amezungumza na mchambuzi wa siasa za kihafidhina Tucker Carlson kwa undani zaidi kwa nini alipinga uamuzi wa Donald Trump wa kuingia vitani, ikiwa ni pamoja na ukosoaji wake wa kumshambulia Ali Khamenei.

    Operesheni ya Marekani na Israel iliyomuua kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, ilikuwa "jambo la mwisho ambalo tulipaswa kufanya," Kent alisema.

    "Angesimamia mpango wao wa nyuklia, angewazuia kupata silaha ya nyuklia," aliongeza.

    "Ukimuua kwa kumshambulia vibaya , watu wataiunga mkono serikali pamoja na Ayatollah anayekuja, na nadhani hiyo ni kweli kwa data zote tulizo nazo juu ya mtoto wake,"

    Kent alisema, akimaanisha kiongozi mpya wa Iran aliyechaguliwa, Mojtaba Khamenei.

    Saa moja baada ya mahojiano ya Bw. Kent na Tucker Carlson kupeperushwa, iliripotiwa kuwa FBI ilikuwa ikichunguza msimamo wa Bw. Kent.

    Vyanzo kadhaa vimeiambia CBS, mshirika wa BBC wa Marekani, kwamba Joe Kent, mkurugenzi wa zamani wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi cha Marekani, anachunguzwa na FBI.

    Kulingana na CBS, uchunguzi huo unahusiana na kutolewa kwa habari za siri, na vyanzo vilisema ulianza kabla ya kujiuzulu mapema wiki hii kutokana na vita nchini Iran.

    CBS ilisema FBI haikujibu ombi la maoni wakati wa kuchapishwa.

  13. Mahakama ya Marekani yaamuru kufunguliwa tena kwa V.O.A

    Mahakama ya Marekani imeamua kwamba amri ya utawala wa Donald Trump ya kuifunga kituo cha habari cha Voice of America V.O.A ilikuwa "kinyume cha sheria" na kwamba mamia ya waandishi wake lazima warudi kazini.

    Jaji wa Mahakama ya Wilaya Royce Lambert amekipa chombo hicho cha kimataifa wiki moja kuendelea kutangaza.

    V.O.A iliundwa wakati wa Vita vya dunia vya pili ili kukabiliana na propaganda za Wajerumani wa Nazi.

    Donald Trump aliamuru kufungwa kwa chombo hicho cha habari wiki chache tu baada ya kurejea ofisini Januari 2025.

    Maafisa katika utawala wake wameishutumu V.O.A kwa kuwa na mielekeo ya mrengo wa kushoto.

    Wakati huo huo, Donald Trump pia aliamuru shughuli za vyombo vya habari kama vile Radio Free Europe na Radio Free Asia "kuzimwa

  14. Habari za hivi punde, Iran yaishambulia tena gesi ya Qatar licha ya onyo kali kutoka kwa Trump

    Shambulizi jingine la Iran limebabisha uharibifu mkubwa katika kituo cha nishati cha Ras Laffan .

    Kabla ya onyo la Trump, televisheni ya taifa ya Iran iliripoti kwamba makombora yalipiga tena kiwanda cha gesi cha Qatar huko Ras Laffan.

    Kampuni ya gesi ya serikali ya Qatar ilithibitisha kuwa vituo vya gesi katika kampuni yake kuu vilipigwa na roketi mapema Alhamisi asubuhi, na kusababisha moto na uharibifu mkubwa zaidi, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

  15. Pentagon inatafuta zaidi ya $200bn kufadhili vita vya Iran - ripoti

    Pentagon imeiomba Ikulu ya White House kuidhinisha zaidi ya $200bn (£151bn) ili kufadhili vita nchini Iran, afisa mkuu wa utawala ameiambia Washington Post.

    Gazeti hilo linasema kwamba kiasi hiki kingepita gharama ya kampeni ya utawala wa Trump hadi sasa, na badala yake kuongeza kwa haraka uzalishaji wa silaha muhimu zinazotumika.

    Maombi tofauti ya ufadhili "yamewasilishwa" na Pentagon katika muda wa wiki mbili zilizopita, inapendekeza kwamba wazo hilo lina uwzekano wa kuanzisha vita vya kisiasa katika bunge la Congress".

    Idara ya ulinzi ya Marekani na Ikulu ya White House zote zilikataa kutoa maoni yao wakati wa chapisho la taarifa hii .

  16. Trump atishia 'kuvilipua kwa kiasi kikubwa' viwanda vya gesi vya Iran

    Rais wa Marekani Donald Trump ametoka tu kutoa chapisho refu la Ukweli wa Kijamii kuhusu shambulio la Israeli kwenye uwanja wa gesi wa Pars Kusini huko Iran Jumatano usiku.

    Katika kulipiza kisasi mgomo huo, Iran ilishambulia Ras Laffan ya Qatar - eneo la viwanda ambalo lina kituo kikubwa zaidi cha kusindika gesi ya kimiminika duniani (LNG).

    Katika chapisho lake lenye maneno makali, Trump anasema Marekani "haikujua lolote" kuhusu mgomo wa Israel, na anatishia kuongezeka iwapo Iran itaishambulia tena Qatar.

    "Kwa hasira kwa kile kilichotokea Mashariki ya Kati", Israeli "ilikemea vikali", Trump anaandika.

    Anaendelea kusema: "Marekani haikujua lolote kuhusu shambulio hili mahususi, na nchi ya Qatar haikuhusika kwa njia yoyote, sura au umbo, wala haikuwa na wazo lolote kwamba ingetokea."

    Lakini Iran haikujua hili, Trump anaandika, na kwamba mashambulizi yake ya kulipiza kisasi kwa Ras Laffan wa Qatar yalifanywa "bila uhalali na isivyo haki".

    Trump anaandika - katika miji mikuu - kwamba Israeli haitashambulia tena uwanja wa gesi wa Pars Kusini wa Iran, "isipokuwa Iran itaamua bila busara kushambulia" taifa lingine lisilo na hatia, ambalo katika kesi hii lilikuwa Qatar.

    Iwapo Iran itaishambulia tena Qatar, Trump anatishia kwamba Marekani "italipua kwa kiasi kikubwa eneo lote la Uwanja wa Gesi wa Pars Kusini kwa kiasi cha nguvu na uwezo ambao Iran haijawahi kuona au kushuhudia hapo awali".

    Anaongeza kuwa hataki kuidhinisha "kiwango hiki cha vurugu na uharibifu kwa sababu ya athari za muda mrefu" kwa Iran, "lakini ikiwa LNG ya Qatar itashambuliwa tena, sitasita kufanya hivyo."

  17. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja

Trending Now