John Heche ataka Tundu Lissu aachiliwe bila masharti

Tundu Lissu amekuwa mahabusu kwa siku 307 akikabiliwa na kesi ya uhaini ambapo leo ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania

Muhtasari

Moja kwa moja

Mariam Mjahid & Rashid Abdallah

  1. Kwaheri hadi kesho

  2. Boti ya wahamiaji yazama Libya na kusababisha vifo vya watu 53

    p

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wahamiaji hao walikuwa wakisafiri katika boti ya mpira wakati ilipozama karibu na pwani ya Libya.

    Boti ya mpira iliyokuwa imebeba abiria 55, wakiwemo watoto wawili wachanga, imepinduka karibu na pwani ya Libya, limesema shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa.

    Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza Jumatatu kuwa manusura pekee ni wanawake wawili raia wa Nigeria, waliokolewa na mamlaka ya Libya siku ya Ijumaa. Boti hiyo ilikuwa imebeba wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

    Boti hiyo ilizama baada ya kuingia maji takriban saa sita baada ya kuondoka kutoka mji wa pwani wa al-Zawiya kaskazini magharibi mwa Libya.

    IOM inasema karibu wahamiaji 500 wameripotiwa kufariki au kutoweka wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kutoka Libya hadi sasa mwaka 2026.

  3. Waliofanyiwa unyanyasaji na Epstein wataka faili zote zitolewe

    ;ll

    Chanzo cha picha, World Without Exploitation

    Waliofanyiwa unyanyasaji na wa mhalifu wa ngono marehemu Jeffrey, Epstein, wameonekana katika tangazo linalotaka kutolewa kwa faili zaidi zinazohusiana na kesi hiyo.

    Katika video ya sekunde 40 kutoka kwa kundi la World Without Exploitation, iliyotolewa nchini Marekani kwenye Super Bowl Sunday, wanawake hao waliinua picha zao za ujanani na kusema "sote tunastahili ukweli."

    Wizara ya Sheria ya Marekani (DOJ) ilitakiwa kisheria kutoa faili zote kwa umma mwezi Desemba mwaka jana. Hata hivyo, ni baadhi tu zilizoachiliwa - nyingi zikiwa zimawekewa vino.

    Naibu Mwanasheria Mkuu wa Marekani Todd Blanche alisema mwezi uliopita kutolewa kwa faili tarehe 30 Januari, "kunaashiria mwisho wa mchakato wa kutoa hati hizo.”

    Epstein alipatikana amekufa katika seli yake ya gereza mwaka 2019 wakati akisubiri kesi yake kwa mashtaka ya biashara haramu ya ngono, huku maafisa wakisema kifo ni kutokana na kujiua.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Wanasiasa Uingereza wamtaka Waziri Mkuu ajiuzulu

    L

    Chanzo cha picha, PA Media

    Kiongozi wa chama cha Labour cha Scotland Anas Sarwar ametoa wito kwa waziri mkuu wa Uingereza, Keir Starmer ajiuzulu.

    Sarwar ameitisha mkutano na waandishi wa habari huko Glasgow leo ambapo ameeleza msimamo wake kuhusu uongozi wa Keir Starmer.

    "Mvurugano unapaswa kuisha kwa uongozi wa Downing Street kuondoka," amewaambia waandishi wa habari.

    Wiki iliyopita, Sarwar alisema Peter Mandelson hakupaswa kamwe kuteuliwa kuwa balozi wa Uingereza huko Washington kwa sababu ya uhusiano na Jeffrey Epstein.

    Naye kiongozi wa chama cha Scottish National Party, Stephen Flynn amemtaka Keir Starmer "kufanya jambo zuri kwa kujiuzulu".

    Flynn anasema ni "wazi" kwamba wapiga kura "wamepoteza imani" na Starmer, akidai Waziri Mkuu "amekuwa kiongozi mlegevu ambaye hana mamlaka yanayohitajika kuleta mabadiliko".

    Ofisi ya Waziri Mkuu ilipoulizwa kama Starmer atajiuzulu, imesema: "Hapana. Waziri mkuu anaendelea na kazi iliyopo mikononi mwake."

    Kiongozi wa chama cha Conservative, Kemi Badenoch, anasema Starmer amepoteza udhibiti wa chama chake.

    Polisi wa Uingereza wanachunguza madai kwamba Mandelson alimpa taarifa nyeti Jeffrey Epstein akiwa serikalini.

    Pia unaweza kusoma:

  5. John Heche ataka Tundu Lissu aachiliwe bila masharti

    P;

    Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani Tanzania Chadema, John Heche, amesema chama chao hatutakubali Tundu Lissu kuachiwa kwa masharti yoyote, kwani alikamatwa kwa uongo, na aachiwe bila masharti yoyote."

    Tundu Lissu amekuwa mahabusu kwa siku 307 akikabiliwa na kesi ya uhaini ambapo leo ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam na kuahirishwa,

    Kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), itasikilizwa tena Jumatano, Februari 11, 2026, ambapo Mahakama itatoa uamuzi juu ya mapingamizi yaliyowasilishwa.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, leo Februari 9, 2026 upande wa Jamhuri uliwasilisha majibu ya mapingamizi yaliyowasilishwa na mshtakiwa Novemba 12, 2025, yanayohusu matumizi ya shahidi wa siri wa Jamhuri pamoja na uwepo wa kizimba maalum cha kutolea ushahidi wa siri ndani ya chumba cha mahakama.

    Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

    Ni takriban miezi kumi imepita tangu mwanasiasa huyo wa chama cha upinzani Tanzania, kuanza kusota rumande.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Jinsi China ilivyotoka kwenye umaskini na kuwa taifa tajiri duniani

    .

    DENG XIAOPING, ni kiongozi ambaye mwishoni mwa miaka ya 1970 alibadilisha uchumi wa China na kuufanya hadi kuwa uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Je alifanyaje mpaka kufanikiwa?

    Bonyeza hapo chini utazame kwa utuao

    Ruka YouTube ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazo

    Mwisho wa YouTube ujumbe

  7. Wandaaji wa Olimpiki kuchunguza kwa nini medali zinavunjika

    o

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Breezy Johnson alifichua kuhusu medali yake ya dhahabu iliyovunjika baada ya kushinda mbio za wanawake

    Waandalizi wa mashindano ya Olimpiki ya Milan-Cortina 2026 wanasema "wanachunguza" kwa nini medali za Olimpiki zinavunjika baada ya wanariadha kadhaa kupata tatizo hilo.

    Wawili kati ya walioshinda medali za dhahabu kutoka Marekani, Breezy Johnson na Alysa Liu, walifichua kwamba utepe umeondoka kwenye medali muda mfupi baada ya kupokea zawadi zao.

    Johnson, ambaye alishinda medali ya dhahabu katika mchezo wa wanawake wa kuteleza kwenye theluji kwenye milima ya alpine, alionyesha medali yake iliyovunjika katika mkutano na vyombo vya habari baada ya tukio hilo.

    Liu alifichua suala kama hilo katika video kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kushinda dhahabu kama sehemu ya kikosi cha Marekani katika shindano la la kuteleza kwenye theluji.

    Suala hilo pia limeikumba timu ya Ujerumani iliyoshinda medali ya shaba. Video ya Instagram inaonyesha medali ikianguka kutoka kwenye utepe wa mmoja wa wanariadha aliporuka kusherehekea katika hoteli.

    Andrea Francisi, afisa mkuu wa uendeshaji wa michezo wa Milan-Cortina 2026, amesema waandaaji wanachunguza suala hilo.

    Msemaji wa Kamati ya Olimpiki na Paralimpiki ya Marekani aliiambia BBC Sport wanasubiri waandaaji watatue suala hilo.

    Bado haijathibitishwa kama wanariadha watapokea medali nyingine.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Afisa aliyependekeza 'kuagiza' wanawake kutoka nje ili kuongeza kuzaliana afukuzwa na chama chake

    p;

    Chanzo cha picha, Bloomberg via Getty Images

    Maelezo ya picha, Korea Kusini ina kiwango cha chini zaidi cha kuzaliana duniani

    Afisa wa Korea Kusini aliyependekeza nchi hiyo "kuingiza wanawake vijana" kutoka "Vietnam au Sri Lanka" ili kuongeza kiwango cha kuzaliana amefukuzwa kutoka chama chake.

    Kim Hee-soo, mkuu wa Kaunti ya Jindo kusini, alisema wiki iliyopita kuwa wanawake hao wanaweza kuolewa na "vijana wa kiume katika maeneo ya vijijini.”

    Pendekezo hilo linakuja huku Korea Kusini ikiendelea kukabiliana na viwango vya chini zaidi vya kuzaliana duniani, ambapo idadi ya watu milioni 50 nchini humo inaweza kupungua kwa nusu katika kipindi cha miaka 60.

    Lakini kauli ya Kim, ambayo ilitolewa kwenye televisheni, haikupokelewa vyema - na kusababisha ukosoaji wa kidiplomasia kutoka Vietnam, hasira za umma na kufukuzwa kwake kutoka Chama tawala cha Democratic.

    Jaribio la Kim ya kutuliza hasira kwa kuomba msamaha siku moja baadaye limeonekana kushindwa kufanya kazi.

    Kim alisema maoni yake yalikusudia kuangazia masuala ya idadi ya watu katika maeneo ya vijijini lakini alikiri lugha aliyotumia haikuwa "sahihi," vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Mkoa wa Jeolla Kusini pia ulitoa taarifa rasmi ya kuomba radhi kwa "matamshi yasiyofaa" ya Kim, ambayo ilisema "yamesababisha maumivu makali kwa watu wa Vietnam na wanawake," vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Ubalozi wa Vietnam huko Seoul ulilaani matamshi ya Kim, katika taarifa yake kwenye Facebook.

    Baraza Kuu la Chama cha Democratic lilipiga kura kwa kauli moja kumfukuza Kim, msemaji wa chama hicho aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu.

    Wakati huo huo, wanaharakati wa haki za wanawake na wahamiaji wanaripotiwa kupanga kufanya mkutano mbele ya Ofisi ya Kaunti ya Jindo Jumanne kuhusu maoni ya Kim.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Eritrea yakana tuhuma za Ethiopia kwamba wanajeshi wake wamevuka mpaka

    k
    Maelezo ya picha, Kuna hofu kwamba mzozo kati ya Ethiopia na Eritrea unaweza kuzuka tena

    Eritrea imejibu shutuma kutoka kwa jirani yake Ethiopia ikielezea madai kwamba wanajeshi wake wako katika eneo la Ethiopia kuwa ni "ya uwongo".

    Siku ya Jumapili, barua iliyotumwa kutoka waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia kwa mwenzake wa Eritrea inawataka wanajeshi hao waondoke.

    Pia iliishutumu Eritrea kwa "uchokozi wa wazi" ikisema inashirikiana na waasi wa Ethiopia kaskazini na kuwapa silaha. Katika jibu lake, Eritrea imesema kauli hiyo ni sehemu ya "mzunguko wa kampeni za uadui dhidi ya Eritrea kwa zaidi ya miaka miwili."

    Kwa muda mrefu kumekuwa na historia ya mvutano kati ya Ethiopia na Eritrea, ambayo ilijitenga na Ethiopia miongo mitatu iliyopita, na kuna hofu ya mgogoro mpya.

    Nchi hizo zilipigana vita vya mpakani kati ya 1998-2000 ambapo zaidi ya watu 100,000 walifariki. Mkataba wa amani haukutekelezwa kikamilifu lakini uhusiano uliimarika baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambaye baadaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa juhudi zake, kusafiri hadi mji mkuu wa Eritrea, Asmara, mwaka 2018.

    Wawili hao walishirikiana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya hivi karibuni vya Ethiopia wakati Eritrea ilipounga mkono jeshi lake dhidi ya vikosi vya Tigray, lakini mambo yameharibika tena.

    Mojawapo ya mambo yanayoleta mvutano ni wito kutoka Ethiopia isiyo na bandari wa kupata bahari, na Abiy amesema ni jambo la lazima. Alisema kupoteza bandari kutokana na uhuru wa Eritrea lilikuwa "kosa.”

    Katika barua yake, waziri wa mambo ya nje alisema ikiwa wanajeshi wa Eritrea wataondoka basi nchi hizo mbili zinaweza kuanza mazungumzo ikiwemo kuhusu "suala la ufikiaji wa bahari kupitia bandari ya Assab."

    Wiki iliyopita Abiy alisema kwa mara ya kwanza kwamba wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2020-2022 huko Tigray, wanajeshi wa Eritrea waliwaua watu wengi katika mji wa Aksum wa Ethiopia.

    Haya ni madai ambayo Eritrea imeyakanusha hapo awali kufuatia ripoti za mauaji ya halaiki yaliyotokea katika mji huo wa kihistoria mnamo Novemba 2020.

    Ethiopia sasa inasema Eritrea inawaunga mkono waasi huko Tigray wanaopinga makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    Mwezi uliopita, polisi wa Ethiopia walisema walikamata maelfu ya silaha zilizotumwa na Eritrea kwa waasi.

    Eritrea ilikanusha madai hayo na kuishutumu Ethiopia kwa "uongo ili kuhalalisha vita ambavyo imekuwa ikivitaka kwa miaka miwili."

  10. Maelfu waandamana Australia kupinga ziara ya rais wa Israel

    LLL

    Chanzo cha picha, ABC

    Maelfu ya watu wamehudhuria maandamano kote nchini Australia kupinga ziara ya Rais wa Israel Isaac Herzog.

    Rais Herzog ameweka shada la maua na mawe mawili kutoka Jerusalem katika Ufuo wa Bondi, eneo ambalo wanaume wawili walifanya shambulizi katika sherehe ya Wayahudi mwezi Desemba.

    Kuna uwepo mkubwa wa polisi takriban maafisa 3,000 waliowekwa kote jijini. Mamia ya maafisa wamepelekwa katika eneo la katikati mwa jiji la Sydney, ambapo maandamano dhidi ya ziara ya Herzog yalianza Jumatatu jioni.

    Usalama umekuwa mkali kwa ziara hiyo ya siku nne ambapo pia atasafiri hadi Canberra na Melbourne na kukutana na Waziri Mkuu Anthony Albanese.

    Viongozi wakuu wa Kiyahudi wamesema safari hiyo itafariji jamii inayoomboleza, lakini wengine wamesema hapaswi kualikwa kutokana na madai kwamba amechochea mauaji ya halaiki huko Gaza.

    Rais huyo alialikwa na Albanese baada ya shambulio la risasi huko Bondi, ambapo watu 15 waliuawa, akiwemo msichana wa miaka 10, katika hafla ya kusherehekea Hanukkah.

    Alex Ryvchin, mwenyekiti mwenza wa baraza kuu la Wayahudi nchini Australia, Baraza Kuu la Wayahudi wa Australia, siku ya Jumatatu alisema ziara ya Herzog inakaribishwa kwa uchangamfu.

    Lakini makundi mengine, ikiwa ni pamoja na Baraza la Kiyahudi la Australia (JCA), lililoanzishwa mwaka 2024 ili kupinga chuki dhidi ya Wayahudi na kuunga mkono uhuru wa Palestina, na Baraza la Kitaifa la Maimamu la Australia, wamesema Herzog hakupaswa kualikwa.

    "Kumwalika mkuu wa nchi anayehusika katika mauaji ya kimbari yanayoendelea kama mwakilishi wa jamii ya Wayahudi ni jambo la kukera sana," amesema afisa mtendaji wa JCA Sarah Schwartz wiki iliyopita.

    Siku ya Jumatatu, barua iliyoandaliwa na JCA na kusainiwa na Wayahudi 600 wa Australia ilichapishwa katika gazeti la Sydney Morning Herald and the Age, ikisema Herzog "hazungumzi kwa niaba yetu na hakaribishwi hapa".

    Nasser Mashni, rais wa Mtandao wa Utetezi wa Palestina wa Australia, alisema katika chapisho kwenye X ziara hiyo ni "kidonge kichungu sana cha kumeza" na "siku ya giza".

    Tume ya Umoja wa Mataifa mwaka jana ilihitimisha kwamba Herzog alikuwa miongoni mwa viongozi wa Israeli ambao "walichochea kuanzishwa kwa mauaji ya kimbari" katika hotuba na matamshi yao.

    Alisema "ni taifa zima linahusika" na shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israeli, na pia amepigwa picha akisaini kombora ambalo lingeshambulia Gaza.

    Kauli yake ni sehemu ya kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikiishutumu Israel kwa mauaji ya kimbari huko Gaza.

    Baadhi ya wabunge wa shirikisho pia wamepinga ziara hiyo, huku baadhi ya wabunge wa chama cha Labour wakisema watajiunga na maandamano ya Sydney.

    Herzog alisema Jumatatu asubuhi kwamba, “ni muhimu kwangu kusema kwamba nimekuja hapa kwa nia njema.”

    Pia unaweza kusoma:

  11. Watu 14 wafariki baada ya jengo kuporomoka Lebanon

    p

    Chanzo cha picha, Reuters

    Idadi ya vifo kutokana na kuanguka kwa majengo mawili ya makazi katika mji wa Tripoli kaskazini mwa Lebanon imeongezeka hadi 14, vimesema vyombo vya habari vya serikali.

    Watu wanane waliokolewa wakiwa hai, amesema mkurugenzi mkuu wa Ulinzi wa Raia, Imad Khreiss.

    Khreiss amesema majengo mawili yaliyopakana yalikuwa makazi ya wakazi 22, na manispaa ya eneo hilo imesema huenda watu wengine bado wamekwama.

    Hili ni jengo la tano la makazi kuporomoka huko Tripoli msimu huu wa baridi, na kuongeza wasiwasi kuhusu majengo ya zamani na yasiyofanyiwa matengenezo katika jiji maskini zaidi la Lebanon.

    Tripoli ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Lebanon na umeshuhudia kuporomoka mara kwa mara kwa majengo huku kukiwa na miaka mingi ya mgogoro wa kiuchumi, ukosefu wa matengenezo, na udhibiti dhaifu.

    Mwezi uliopita, serikali ilisema zaidi ya majengo 100 katika jiji hilo yanapaswa kuhamwa.

    Majengo mengi ya makazi kote Lebanon yalijengwa kinyume cha sheria au bila vibali, hasa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1975-1990, huku mengine yakipanuliwa zaidi bila usimamizi sahihi, mamlaka yanasema, na kuwaacha maelfu katika hatari, hasa wakati wa miezi ya baridi na mvua.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Wanachama 14 wa genge linalodaiwa kuwanyanyasa watoto kingono wakamatwa

    =[

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Maelezo ya picha, Polisi wa Senegal wameahidi kufuatilia na kuvunja mitandao kama hiyo ya uhalifu

    Polisi wa Senegal wanasema wamewakamata watu 14 na kuvunja genge la wabakaji linalofanya kazi kati ya nchi hiyo na Ufaransa.

    Waliokamatwa, ambao wote ni Wasenegali, walikuwa sehemu ya kundi la wahalifu "wa kimataifa" ambalo limekuwa likifanya kazi tangu 2017, kulingana na taarifa ya polisi.

    Kundi hilo linashutumiwa kwa "kupanga unyanyasaji wa kijinsia, ulawiti, ubakaji wa watoto walio chini ya umri wa miaka 15, na uambukizaji wa VVU/UKIMWI kwa makusudi."

    Inadaiwa waliwalazimisha wavulana kufanya "ngono bila kinga" na wanaume ambao wengi wao wana maambukizi ya VVU na walirekodi kwa video.

    Washtakiwa wanne wanasemekana kutenda hayo "kwa maagizo" ya Mfaransa aliyekamatwa nchini Ufaransa Aprili 2025 ambaye alikuwa akiwapa pesa.

    Washtakiwa 14 walifikishwa mbele ya jaji siku ya Ijumaa kufuatia upekuzi katika vitongoji kadhaa huko Dakar, na jiji la Kaolack, kilomita 200 (maili 124) kusini-mashariki mwa mji mkuu.

    Taarifa ya polisi iliyotolewa Jumapili ilisema uvamizi umefanywa katika nyumba za washukiwa mbalimbali, huku vitu vinavyoaminika kuhusishwa na uhalifu vilikamatwa.

    Kitengo cha Upelelezi wa Jinai (DIC) kimesema operesheni hiyo ilifanywa kupitia ushirikiano kati ya Senegal na Ufaransa, huku maafisa wa Ufaransa wakihusika katika misheni hiyo.

    Pia unaweza kusoma:

  13. Mzungu aliyeua watu 51 katika misikiti miwili akata rufaa dhidi ya kifungo cha maisha

    k
    Maelezo ya picha, Brenton Tarrant raia wa Australia anatumikia kifungo cha maisha jela bila msamaha

    Mwanaume mmoja Mzungu mwenye misimamo mikali ya kibaguzi aliyewaua watu 51 katika misikiti miwili huko New Zealand amefika mahakamani kutaka mahakama iondoe hatia kwa kukiri makosa.

    Brenton Tarrant raia wa Australia anatumikia kifungo cha maisha jela bila msamaha baada ya kukiri kuwaua watu 51 na kujaribu kuwaua wengine 40 katika shambulio la Machi 2019 dhidi ya waumini wakati wa sala ya Ijumaa huko Christchurch.

    Awali alikana mashtaka hayo, lakini alikiri kosa mwaka mmoja baada ya shambulio hilo.

    Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye pia alikiri shtaka moja la ugaidi, sasa amekata rufaa akisema hakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wakati huo kwa sababu ya "mateso na hali isiyo ya kibinadamu" gerezani.

    Pia anataka kukata rufaa dhidi ya hukumu yake. Kesi hiyo katika Mahakama ya Rufaa ya New Zealand huko Wellington imepangwa kufanyika wiki nzima, huku Tarrant akitarajiwa kutoa ushahidi kupitia video.

    OL
    Maelezo ya picha, Wengi wa waathiriwa walikuwa wamehamia New Zealand kufanya kazi au kusoma, na baadhi walikuwa wakimbizi

    Mauaji katika msikiti wa Al Noor na Kituo cha Kiislamu cha Linwood – ambayo aliyarusha mubashara - yalisababisha sheria kali za udhibiti wa bundki nchini New Zealand.

    Wakati wa hukumu hiyo Agosti 2020, Waziri Mkuu wa New Zealand wa wakati huo, Jacinda Ardern, alisema kifungo cha maisha bila msamaha kinamaanisha Tarrant hatakuwa na "jukwaa la kusikilizwa ... na hatuna sababu ya kumfikiria, kumwona au kumsikia tena."

    Ikiwa majaji watatu wa mahakama ya rufaa wataamua kuondoa kukiri kwake makosa, kesi hiyo inaweza kusikilizwa tena kwa mashtaka yote.

    Tarrant alizaliwa New South Wales, Australia, lakini alihamia New Zealand mwaka 2017 - ambapo, waendesha mashtaka walisema, ndipo alipoanza kupanga mashambulizi yake dhidi ya jamii ya Waislamu.

    Pia unaweza kusoma:

  14. Urusi na Oman wasisitiza hitaji la kuendeleza mazungumzo kuzuia mgongano wa kijeshi wa Iran na Marekani

    Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araqchi

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araqchi

    Urusi na Oman zimesema kuwa mazungumzo kati ya Iran na Marekani yanapaswa kuendelea.

    Kwenye taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi baada ya mazungumzo ya simu kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Saeedi, na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, imeelezwa kuwa Moscow na Muscat zilisisitiza hitaji la kuendeleza mazungumzo ili kuzuia mgongano wa kijeshi kati ya Iran na Marekani na kuhakikisha uthabiti wa kieneo.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi pia imesema kuwa Sergei Lavrov alithamini jitihada za Oman katika muktadha huu.

    Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani iliandaliwa Ijumaa, Februari 6, mjini Muscat, mji mkuu wa Oman, kwa lengo la kutafuta suluhisho la mgogoro wa nyuklia wa Tehran.

    Kikundi cha Iran kiliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araqchi, huku kikundi cha Marekani kiliongozwa na mjumbe maalum wa Donald Trump, Steve Witkoff.

    Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, mazungumzo ya kina yalifanyika kati ya makundi ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, na pande zote zilirudia kiapo chao cha kuendelea na mazungumzo hayo.

    Soma zaidi:

  15. Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, afikishwa Mahakamani

    Tundu Lissu akiwa mahakamani leo
    Maelezo ya picha, Tundu Lissu akiwa mahakamani leo

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Tundu Lissu, inayojulikana kama Criminal Session Case No. 19605/2025, inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

    Mahakama imepanga kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo kwa mfululizo kuanzia leo tarehe 09 Februari 2026 hadi 6 Machi 2026.

    Kesi inasikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, likiwa na, Mheshimiwa Jaji Ndunguru, Mheshimiwa Jaji J. Karayemaha na Mheshimiwa Jaji Kiwonde.

    Kwa sasa, kesi ipo katika hatua ya usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa Jamuhuri, ambapo ushahidi unatolewa kwa kina na kwa mujibu wa taratibu rasmi za kisheria.

    CHADEMA imetoa wito kwa wanachama na wananchi kwa ujumla kufuatilia kwa umakini muendelezo wa kesi hii, wakiitaja kuwa kesi hiyo ni taswira muhimu ya demokrasia na haki nchini Tanzania.

    Mawakili
    John Heche
    Wafuasi na Umma wafuatilia kesi hiyo mahakamani
    Maelezo ya picha, Wafuasi na Umma wafuatilia kesi hiyo mahakamani

    Soma Pia:

  16. Kenya: Wanandoa 327 wafunga ndoa kwenye harusi ya pamoja siku chache kabla ya mfungo wa Ramadhan

    Ndoa za jumla nchini Kenya

    Chanzo cha picha, KNA

    Maelezo ya picha, Ndoa za jumla nchini Kenya

    Wanandoa 327 kutoka kaunti za Kwale, Mombasa, na Kilifi nchini Kenya wamefanya harusi zao katika sherehe ya pamoja iliyofanyika Kwale Baraza Park, Kaunti ya Kwale.

    Tukio hili la kila mwaka, ambalo limefanyika kwa mwaka wa 6 mfululizo, liliendeshwa na Kadhi Mkuu wa Muda, Sukyan Omar Hassan.

    Harusi ya pamoja, iliyofanyika siku chache kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni mpango ulioanzishwa na Mbunge wa Matuga, wa kaunti hiyo.

    Mbunge huyo alisema harusi ya pamoja inalenga kupunguza gharama kubwa za sherehe za ndoa, ambapo wazazi wa wake huweka sharti la kiasi kikubwa cha mahari kabla ya kuruhusu binti zao kuolewa.

    Sheikh Athman, alipokuwa akijumuika na wanandoa hao katika ndoa takatifu alifichua kuwa hadi wanandoa watakapounganishwa katika ndoa, wanahesabika kuwa wanaishi pamoja jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa Uislamu kuwa ni dini.

    Kiongozi wa kidini ambaye pia ni afisa katika mahakama Kenya alisema ni makosa kwa wanandoa kuishi pamoja kwa jina la nyakati ngumu za kiuchumi na kuwataka wasomi wa Kiislamu na wazazi kuwahimiza watoto wao kufanya yaliyo sawa.

    "Huu ni mpango mzuri wa kuwasaidia wanandoa wachanga ambao hawana uwezo wa kuandaa sherehe zao za harusi," alisema Sheikh Athman.

    Kadhi Mkuu alisema usajili wa ndoa unafuata mafundisho ya kidini ili kuzuia changamoto zozote zinazoweza kutokea kutokana na ndoa zisizosajiliwa kisheria.

    Soma Pia:

  17. Wachimbaji migodi 11 wafariki, 6 kujeruhiwa baada ya mgodi kuporomoka DRC

    Wachimbaji migodi hukabiliwa na uhaba wa mashine zinazofaa na salama

    Chanzo cha picha, Hassan Lali / BBC

    Maelezo ya picha, Wachimbaji migodi hukabiliwa na uhaba wa mashine zinazofaa na salama

    Mgodi umeanguka katika eneo la uchimbaji Tilwizembe, kilomita 25 kutoka Kolwezi, Mkoa wa Lualaba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

    Kulingana na nyaraka kutoka Huduma ya Usaidizi, Usimamizi na Uendeshaji wa Uchimbaji Madini Madogo na ya Kiasili (SAEMAPE), ambazo BBC imezipata leo, ajali hiyo ilitokea takriban saa 9 asubuhi Jumamosi, ikafunika wachimbaji wadogo waliokuwa wakifanya kazi kinyume cha sheria.

    Kwa sasa, idadi ya vifo imesalia 11 huku wengine 6 wakijeruhiwa.

    Mabaki ya marehemu yameopolewa na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Lualaba-Mupandja.

    SAEMAPE, huduma ya kiufundi inayohusiana na Wizara ya Madini ya DRC, imesema sababu za ajali ni pamoja na: kazi isiyo halali usiku, hitilafu katika mfumo wa mifereji ya maji, na kushirikiana kwa baadhi ya walinzi wa eneo hilo.

    Hususan, msiba huu unajiri baada ya ajali kadhaa zinazofanana mwaka 2024, ambapo wachimbaji 17 wa madini wadogo walipoteza maisha katika eneo hilo.

    Mamlaka za mkoa zinapendekeza kusitishwa mara moja kwa shughuli zote za uchimbaji, tathmini ya kiufundi ya maeneo yasiyo thabiti, na ukaguzi wa maeneo yote ya hatari kubwa ya uchimbaji.

    Soma Pia:

  18. Mshindi wa Tuzo ya Nobel kutoka Iran aongezewa kifungo cha jela, asema wakili

    Narges Mohammadi alikamatwa mwezi Disemba kwa kutoa "maneno ya uchochezi" kwenye hafla ya mazishi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Narges Mohammadi alikamatwa mwezi Disemba kwa kutoa "maneno ya uchochezi" kwenye hafla ya mazishi

    Mostafa Nili, wakili wa Narges Mohammadi, ametangaza kuwa Mahakama ya Mapinduzi ya Mashhad imemhukumu mteja wake kifungo cha muda mrefu gerezani pamoja na miaka miwili ya uhamisho.

    Bw. Nili aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X kwamba Bi. Mohammadi amehukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani kwa kosa la “kukusanyika na kupanga njama,” na kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani kwa kosa la “shughuli za propaganda.”

    Kama adhabu ya ziada, amepigwa marufuku ya kusafiri nje ya nchi kwa miaka miwili na kuhamishwa hadi Wilaya ya Khusf kwa miaka miwili.

    Khusf ni mji uliopo katika mkoa wa Khorasan Kusini.

    Katika mahojiano na BBC Persian, mume wa Bi. Mohammadi, Taghi Rahmani, aliitaja hukumu hiyo kuwa “katili” na kusema kuwa mahakama ya ngazi ya chini “ilitoa hukumu hii nzito kwa tuhuma pekee ya kuhudhuria mazishi na kutoa hotuba.”

    Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Narges Mohammadi, pamoja na wanaharakati wengine kadhaa, walikamatwa mwezi Desemba mwaka jana katika hafla ya saba ya kumuenzi wakili wa haki za binadamu, Khosrow Alikurdi.

    Bw. Rahmani alisema: “Ni siku 59 sasa tangu Narges Mohammadi akamatwe, na aliruhusiwa kuwasiliana na familia yake siku ya pili tu baada ya kukamatwa. Hata hivyo, katika simu hiyo pia, mara tu Mohammadi alipogusia hali ya gerezani, simu ilikatizwa.”

    Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Binadamu lenye makao yake Marekani limesema limehesabu zaidi ya watu 50,000 waliokamatwa kuhusiana na maandamano hayo, na limethibitisha vifo visivyopungua 6,961.

    Ombi hilo lilitaka kufunguliwa mashtaka dhidi ya wale waliotekeleza maagizo ya Khamenei, pamoja na kukomeshwa kwa Jamhuri ya Kiislamu.

    Wanaharakati wanne mashuhuri wa Iran, waliotambuliwa kama Abdollah Momeni, Mehdi Mahmoudian, Vida Rabbani na Ghorban Behzadian-Nejad pia wamekamatwa tangu tarehe 31 Januari kwa mchango wao katika ombi hilo.

    Taghi Rahmani ametoa wito wa kuachiliwa kwa “wafungwa wote wa kisiasa nchini Iran.”

    Soma Pia:

  19. Mahakama ya Hong Kong yamfunga anayeunga mkono demokrasia Jimmy Lai miaka 20 jela

    Lai ni miongoni mwa watu mashuhuri walioshtakiwa chini ya sheria tata ya usalama wa taifa ya Hong Kong

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Lai ni miongoni mwa watu mashuhuri walioshtakiwa chini ya sheria tata ya usalama wa taifa ya Hong Kong

    Mahakama ya Hong Kong imemhukumu bilionea anayefahamika kwa kuunga mkono demokrasia, Jimmy Lai, kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya ukiukaji wa usalama wa taifa mwezi Desemba.

    Hukumu hiyo ndiyo kali zaidi kuwahi kutolewa chini ya sheria tata ya usalama wa taifa, ambayo China inadai ni muhimu kwa uthabiti wa jiji hilo.

    Lai, mwenye pasipoti ya Uingereza, alikuwa miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa Beijing, akitumia mara kwa mara gazeti lake la kidemokrasia Apple Daily kama chombo cha kupinga utawala huo.

    Wakuu sita wa zamani wa gazeti hilo pia wamehukumiwa kifungo cha jela siku ya Jumatatu, kati ya miaka sita na miezi tisa hadi miaka 10.

    Kwa wanaharakati wa demokrasia, Lai anaonekana kama shujaa, lakini kwa Beijing anachukuliwa kuwa msaliti.

    Amekuwa akikanusha mashtaka yote dhidi yake, akisema alitetea kile alichoamini kuwa ni maadili ya Hong Kong, ikiwemo utawala wa sheria na uhuru wa kujieleza.

    Hukumu hiyo ina maana kuwa huenda akawa na umri wa miaka 96 atakapoachiliwa huru mwaka 2044.

    Serikali ya Taiwan imeitaka China na Hong Kong kusitisha mara moja mateso ya kisiasa na kumuachilia Lai.

    Binti yake, Claire Lai, ameieleza hukumu hiyo kuwa ya “kikatili na ya kuvunja moyo,” akiongeza kuwa afya ya baba yake imezorota katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

    “Atakufa shahidi akiwa gerezani,” amesema.

    Pia Unaweza Kusoma:

  20. Hisa za Japan zapanda kiwango cha juu baada ya Takaichi kushinda uchaguzi kwa kishindo

    Takaichi ni mwanamke wa Kwanza kuwa Waziri Mkuu Japan

    Chanzo cha picha, Pool/Getty Images

    Maelezo ya picha, Takaichi ni mwanamke wa Kwanza kuwa Waziri Mkuu Japan

    Muungano unaoongozwa na Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, umepata ushindi mkubwa wa kihistoria katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, hatua inayotarajiwa kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini humo.

    Ushindi huo unaipa serikali nafasi ya kutekeleza sera zake muhimu, zikiwemo ahadi za kupunguza kodi pamoja na kuimarisha matumizi ya kijeshi ili kukabiliana na changamoto za kiusalama, hususan kuhusiana na China.

    Takaichi, mwanasiasa wa mrengo wa kihafidhina na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan, ameweka wazi kuwa anavutiwa na falsafa ya uongozi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Margaret Thatcher, aliyefahamika kama “Iron Lady”.

    Chama chake cha Liberal Democratic Party (LDP) kimepata viti 316 kati ya 465 katika Baraza la Wawakilishi, matokeo bora zaidi kuwahi kupatikana katika historia ya chama hicho.

    Rais wa Marekani Donald Trump alimpongeza Takaichi kwa ushindi huo kupitia mitandao ya kijamii, akimtakia mafanikio katika kutekeleza ajenda yake ya kihafidhina na sera ya kudumisha amani kupitia nguvu za kijeshi.

    Trump pia alieleza kuwa uamuzi wa Takaichi wa kuitisha uchaguzi ulikuwa wa busara na umezaa matokeo chanya, akithibitisha kuwa atampokea katika Ikulu ya White House mwezi ujao.

    Takaichi mwenye umri wa miaka 64 aliitisha uchaguzi huo wa nadra wakati wa majira ya baridi akilenga kutumia kiwango kikubwa cha uungwaji mkono kutoka kwa wananchi, ambacho kimeongezeka tangu alipoteuliwa kuongoza LDP mwishoni mwa mwaka jana.

    Umaarufu wake umetokana na taswira ya uongozi thabiti, mtazamo wa kusema mambo kwa uwazi na kujituma katika utendaji.

    Hata hivyo, mwelekeo wake wa uzalendo mkali na msisitizo katika masuala ya usalama wa taifa umeibua changamoto katika uhusiano wa Japan na jirani yake mwenye ushawishi mkubwa, China.

    Wakati huohuo, ahadi zake za kupunguza kodi zimeibua wasiwasi katika masoko ya fedha.

    Soma Pia:

Trending Now